Kadogosa: Tumetumia umeme wa 336,000 kwenda na kurudi Dar - Morogoro

Naona unatoka nje ya mada BTW, hawawezi kutumia umeme wa 336,000, Kwa 178KM from Dar to Moro, haipo na haitokuwepo.
 
Kama kwa bei hiyo basi nauli haitakiwi kuzidi elfu 10 na dar dodoma haitakiwi kuzidi elfu 20.
 
Basi kama hivyo, nauli ziwe chini zaidi, sababu wameenda na kurudi kwa laki 3 na ushehe, that means kwenda tu ni umeme wa laki na 60 na kitu hivi.
kama hiyo ni kweli hajatudanganya, aisee mbona inatumia umeme mdogo sana? watapata faida kubwa. tuangalie, umejaza wese V8 kwenda na kurudi morogoro utatumia mafuta ya shilingi ngapi? au tuseme scania limejaza kontena huma huko kwenda na kurudi moro utatumia wese la 330,000?
 
Hii ni habari njema kwa matumizi ya umeme wa 333k, sasa mtupunguzie nauli ya 25k. Tunawasihi sana!
 
Sasa mnataka aseme wametumia wa milioni 2 ili kukufurahisha wewe? Majitu mengine mkoje?
Usipanick mkuu,ni kitu kigeni na lazima kila MTU awe na mtazamo wake. Train ya umeme kibongobongo wengine tunaishangaa.
Binafsi nilidhani dar Moro ni less than an hour,pia nilijua umeme umeungwa moja Kwa moja hakuna tena kuhesabiana gharama.
Yaani Mambo ni mengi so tuelimisheni sio Kwa matusi na masimango Bali Kwa upole na upendo.
 
Asante mkuu nimekuelewa! Twende taratibu. Umeme lazima ulipwe haiwezi kwenda bure!
 
Tusingeweza kutoa maelezo hayo kutoka na hadhira.hayo mengine ataelezwa CAG kwa niaba yako na wengine, wewe tosheka na ulichoambiwa kwa Sasa.
taarifa nusu nusu zinakuja kufanyaje hadharani?, siwezi tosheka bila ufafanuzi zaidi, tumezoea gari ikiwa na mzigo mkubwa speed yake hushuka/hupungua, mafuta hutumika mengi zaidi n.k..tunahitaji kujua kwenye treni huku vipi?
 
Yale yale ya mwendo kasi...kutoka mwendo kasi mpaka mwendo wa haraka.
Hii nchi hii..[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sasa ikawaje nauli walizopendekeza hazikamatiki kama gharama za uendeshaji zipo chini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…