Kadogosa: Tutaanzisha tozo za barabara, watu walipie matumizi yake

tuwe kama southafrica barabara wanajitahidi kufanya repair kila siku na wanajenga mikeka ya viwango hata kuchangia unasikia raha kwa huduma unayopata
Tunashindwa nini kutumia fedha za tozo ya barabara inayokatwa kwenye kila lita ya mafuta? viongozi wa nchi hii ni wabinafsi, hebu tuambie fedha ya tozo za simu imekusaidia nini mpaka leo tangu ianzishwe
 
Siyo lazima kuwaiga majirani, huo ni utumwa na ufinyu wa kufikiri, kwanini tusifikirie namna nyingine ili hao majirani waje kujifunza kwetu?
ili serikali yoyote duniani ijiendeshe na itoe huduma kwa wananchi lazima kodi na tozo ziwepo, mtu ana magari karibia mia ndani halafu anajaza foleni na kutumia barabara, lazima achangie ili ziweze kuwa bora kila siku ,thats very basic sasa unataka kutumia barabara na magari yako huku hutaki kuchangia matengenezo yake? Na katika nchi ambayo watu wanalipa tozo na kodi kidogo ukanda huu wa afrika ni tanzania ,tupunguze kulalamika road tolls ni muhimu ili kila mtu awajibike na matumizi ya barabara, kama hutaki panda public transport
 
Hatujakataa, hizo tozo zipo kitambo, lakini je zinafanya nini?
 
Mkuu huoni barabara zinazojengwa kila kona, na ile hela makandarasi wa ndani wakilipwa inarudi kwenye mzunguko inatufikia mimi na wewe, ukitoka nje ya tanzania ukatembea ndio utagundua tanzania inaendelea kwa kasi na atleast kuna accountability kulinganisha na nchi nyingine, hizi lami na barabara za zege mitaani hela umetoa wewe? Si ndio tozo zako zinajenga, lakini ili tuweze kujenga zaidi na kuzikarabati lazima anayetumia achangie kadri anavyotumia
 
Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amesema Serikali inaweza kuanzisha tozo za matumizi ya barabara na madaraja ili kukabiliana na mahitaji makubwa ya matengenezo na kuhimili athari za ongezeko la matumizi ya miundombinu hiyo. Kadogosa ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, wakati akizungumza Bungeni, akieleza kuwa Serikali italazimika kufanya baadhi ya maamuzi magumu kutokana na mahitaji makubwa ya maendeleo nchini.

Amesema uharibifu wa barabara unaochangiwa na magari kuzitumia mara kwa mara, pamoja na kuongezeka kwa uzito wa magari yanayopita, ni miongoni mwa changamoto zinazohitaji hatua za ziada za kifedha. “Msije mkashangaa, Waheshimiwa Wabunge, tuna-introduce road tolls, watu walipie barabara, watu walipie madaraja. Ndiyo vitu ambavyo tutaweza kuhimili haya mabadiliko,” amesema Kadogosa.

Ameongeza kuwa barabara kuonekana kuelemewa kunahusiana pia na kuongezeka kwa shughuli za maendeleo na matumizi ya miundombinu, akitoa wito kwa wabunge kushirikiana na Serikali katika maamuzi yatakayochukuliwa.

CCM hawana kumbukumbu sijui au akili ni shida, zamani ulikuwa na road licence kila gari linalipa kwa kutumia barabara.
Wakasema hicho kiwango ni kidogo hayo malipo yahamishiwe kwenye mafuta ( petrol na diesel), sasa hiyo Kodi itaondolewa ije Kodi mpya au hajui anaongea nini?
 
Waziri wa Ujenzi, Masanja Kadogosa, amesema Serikali inaweza kuanzisha tozo za matumizi ya barabara na madaraja ili kukabiliana na mahitaji makubwa ya matengenezo na kuhimili athari za ongezeko la matumizi ya miundombinu hiyo. Kadogosa ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, wakati akizungumza Bungeni, akieleza kuwa Serikali italazimika kufanya baadhi ya maamuzi magumu kutokana na mahitaji makubwa ya maendeleo nchini.

Amesema uharibifu wa barabara unaochangiwa na magari kuzitumia mara kwa mara, pamoja na kuongezeka kwa uzito wa magari yanayopita, ni miongoni mwa changamoto zinazohitaji hatua za ziada za kifedha. “Msije mkashangaa, Waheshimiwa Wabunge, tuna-introduce road tolls, watu walipie barabara, watu walipie madaraja. Ndiyo vitu ambavyo tutaweza kuhimili haya mabadiliko,” amesema Kadogosa.

Ameongeza kuwa barabara kuonekana kuelemewa kunahusiana pia na kuongezeka kwa shughuli za maendeleo na matumizi ya miundombinu, akitoa wito kwa wabunge kushirikiana na Serikali katika maamuzi yatakayochukuliwa.

Ile road toll kwenye mafuta imekwenda wapi? Haitoshi au Mweshimiwa hajui kuwa ipo,au mbanga za kazi aonekane.
 
Siku zijazo kutakuwa na tozo za tendo la ndoa, unataka kumgegeda mkeo unalipa tozo kwanza ndio ugegede... tutafungiwa camera, askari wa jiji watakuwa wanazunguka kwemye madirisha ya watu usiku kucha..
Hii nchi viongozi sijui wanawaza nini yarabi
 
Wazo la majimbo Lina mashiko ili sehemu kubwa ya mapato yabaki jimboni kushughulikia kero zao.serikali kuu kulipia gharama za maendeleo kwa nchi kubwa kama Tanganyika ni mzigo
 
Uzuri wa Kadogosa anaonhea ukweli kisha anawaacha mnabishana yeye kimya. Mfano Reli ya SGR alisema itachukua miaka 15 kukamilika, watu wakampiga sana.. Na hapa amesema kwenye barabara bila tozo mipango yote haitawezekana. Watu wanapinga tena. Lakini tunaweza kuona jinsi barabara zilivyochoka. Yaani barabara haimalizi miaka 2 sababu hakuna hela ya kujenga barabara imara
 
Back
Top Bottom