Kafulila amefanya jumla ya mihadhara 44 kati ya hiyo 34 ni ya kiuchumi -Dkt Kaihoza

Kafulila amefanya jumla ya mihadhara 44 kati ya hiyo 34 ni ya kiuchumi -Dkt Kaihoza

Kafulila aka Tumbili kwenye moja ta IDs zako 12. Unatupotezea muda kujisifia badala ya kufanya kazi.

Uwingi wa mijadala uliyoifanya siyo kipimo cha utendaji. Utendaji wako utapimwa kwa idadi ya miradi YA PPP uliyoisajili na kama ime take off.

Acha upumbavu Kafulila
Hahaha sasa turudi kwenye hoja zake achana na huu umbea wako
 
Huyu tumbili ana matatizo ya akili hata abadili ID mara 100 bahati nzuri anaacha pattern za kujulikana.
Daaah nadhani tujadili hoja sio mtoa hoja haiwezekani kila ID inayomzungumza Kafulila ni yake
 
Hahaha sasa turudi kwenye hoja zake achana na huu umbea wako
Hakuna cha kujadili hapa. CEO anapimwa kwa deliverables kupitia KPIs alizopewa na boss wake. Isijekuwa hata TaiPei ni ID ya Kafulila
 
Daaah nadhani tujadili hoja sio mtoa hoja haiwezekani kila ID inayomzungumza Kafulila ni yake

Kuna hoja gani hapo ya kujadili kwanza?

Umekuja na ID nyingine tumbili, naona huu uzi unabadili tu ID kujisifia uzi umejaa maoni ya aina moja kama robots unafikiri wote hawajuo michezo yako ya multiple IDs.
 
Kuna hoja gani hapo ya kujadili kwanza?

Umekuja na ID nyingine tumbili, naona huu uzi unabadili tu ID kujisifia uzi umejaa maoni ya aina moja kama robots unafikiri wote hawajuo michezo yako ya multiple IDs.
Kwani umekosa kabisa hoja??
 
Hakika
Wasalaam Jf.

Record hii ya David Kafulila inanivutia kuwa mchumi,


Akimkaribisha Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Ubia Tanzania, Bwana David Zacharia Kafulila, mchumi mahiri Dkt. Bravios Kaihoza alisisitiza umuhimu wa taasisi za kiuchumi katika safari ya maendeleo ya Taifa lolote lile Duniani. Anasema,

Kwanza, katika historia ya uchumi wa Tanzania, taasisi kuu zilizotambuliwa ni Benki Kuu ya Tanzania, Tume ya Uwekezaji Tanzania (TIC), Tume ya Mipango na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa hivi karibuni, orodha hiyo imeongezeka na sasa tunazo taasisi tano muhimu, ikiwemo Kituo cha Ubia Tanzania (PPP Center).

Pili, ni muhimu kumwelezea mtu huyu ambaye leo tunamkaribisha. Tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Center takribani miaka miwili na nusu iliyopita, Bwana Kafulila amekuwa mstari wa mbele katika kutoa hotuba na mihadhara ya kiuchumi yenye uzito wa kitaifa.

Kwa takwimu, ameshiriki jumla ya mihadhara na majadiliano 44 katika vyuo vikuu, makongamano na vyombo vya habari. Kati ya hiyo, 34 zimechukuliwa kama hotuba za kiuchumi, kwa kuwa zaidi ya asilimia 60 ya maudhui yake yalihusu masuala ya uchumi. Ndani ya hotuba hizo, 18 zimehusu miundombinu ya kiuchumi kama barabara na nishati, 7 miundombinu ya kijamii ikiwemo elimu, afya na maji, 2 kilimo, 2 vijana, 1 wanawake, 2 umasikini, na 1 diplomasia.

Kwa hivyo, mchango wa Kafulila katika mjadala wa uchumi wa taifa ni mkubwa na wa kudumu, ukibeba dira ya maendeleo na nafasi ya kipekee ya PPP Center kama taasisi ya msingi katika mustakabali wa uchumi wa Tanzania. Ni wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano wa mtendaji huyu katika kulisaidia taifa kusonga mbele kiuchumi na kijamii.

View: https://www.instagram.com/reel/DeZsuSmADKD/?dlrf=MWh6eGZ2bjhpZmwzMg==
 
Back
Top Bottom