Kafulila amefanya jumla ya mihadhara 44 kati ya hiyo 34 ni ya kiuchumi -Dkt Kaihoza

Kafulila anahitaji kutumiwa vizuri na Watanzania ili kuwaletea manufaa zaidi.
 

Hongera sana David Kafulila kwa kazi kubwa na yenye kuonekana. Mihadhara 44, huku 34 ikiwa ya kiuchumi, si jambo dogo; ni ushahidi wa juhudi za kueneza maarifa na kujenga mjadala mpana kuhusu uchumi na maendeleo ya Taifa.

Kinachostahili pongezi zaidi ni kuona kiongozi akitumia nafasi yake si kukaa ofisini pekee, bali kwenda kwa wananchi, vyuo, wafanyabiashara na wadau mbalimbali kueleza fursa za uwekezaji, PPP na namna sekta binafsi inaweza kuwa injini ya maendeleo.

Hongera Kafulila kwa kuifanya elimu ya uchumi kuwa sehemu ya kazi ya uongozi. Tanzania inahitaji viongozi wanaojenga uelewa, wanaochochea fikra mpya na wanaothubutu kuibua mijadala mikubwa ya maendeleo. Endelea kuchapa kazi matokeo ndiyo yatakayokuwa ushahidi mkubwa zaidi.
 
Mwanga wa Jua , Uelekeo555 Bibianna CM 1774858 Chai na Uji ni zak9 haijalishi ni mpya au za zamani bado ni wewe.

Hoja yako kwamba kila ID inayomuunga mkono Kafulila lazima iwe ni Kafulila mwenyewe haina msingi bila ushahidi. Kuwa na ID zaidi ya moja pekee hakuthibitishi kwamba akaunti fulani ni ya mtu unayemtuhumu; hata mijadala ya JF kuhusu multiple IDs imeonyesha kuwa madai hayo yanahitaji ushahidi zaidi kuliko kufanana kwa mitazamo.

Halafu jiulize: hata ukisema hizo ID zote ni zake, vipi kuhusu maelfu ya viewers wanaosoma mijadala hiyo bila hata kuchangia? Hao wote pia ni Kafulila? Ukweli ni kwamba mtu mwenye historia ndefu kwenye siasa, uchumi na mijadala ya kitaifa ni kawaida kuwa na watu wanaomuunga mkono, wanaompinga na wanaofuatilia anachosema.

Kwa hiyo tusifikie hatua ya kudhani kila anayesema “Kafulila ana hoja” basi huyo ni Kafulila. Huo si mjadala wa hoja tena. Kama hoja yake ni mbaya, ipinge kwa takwimu na hoja mbadala. Kama ni nzuri, ukubali ubora wake hata kama humpendi mhusika. Umaarufu wa Kafulila na kuwa na followers wengi si kosa; kinachopaswa kujadiliwa hapa ni hoja zake, si kuwageuza wote wanaomuunga mkono kuwa mtu mmoja.

So punguza tabia za kishoga.
 

Akili za kitumbili hapo umeswitch ID ila mwandiko ule ule.

Jinga kabisa.
 
Hongera sana David Kafulila. Mihadhara 44, huku 34 ikiwa imejikita kwenye masuala ya uchumi, ni mchango mkubwa katika kujenga uelewa wa wananchi kuhusu uchumi na maendeleo. Taifa linahitaji viongozi wanaotumia majukwaa mbalimbali kuelimisha, kuchochea mijadala na kutoa mawazo yanayoweza kusaidia kutatua changamoto za kiuchumi. Endelea kutoa elimu na kuchochea fikra mpya kwa maendeleo ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…