Kafulila: Anayetaka kuwekeza TANESCO na aje,Tanzania inajengeka kwa Kasi mno mwaka 2050 tutahitaji zaidi ya Megawatt 60K wakati leo tuna Megawatt 4K

Kafulila: Anayetaka kuwekeza TANESCO na aje,Tanzania inajengeka kwa Kasi mno mwaka 2050 tutahitaji zaidi ya Megawatt 60K wakati leo tuna Megawatt 4K

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2021
Posts
2,128
Reaction score
1,896
==
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila akihojiwa katika Kipindi Cha One on One Cha Wasafi TV amesema haya,

" Tanzania katika miaka 25 ijayo inatarajia kujenga Uchumi mkubwa karibu mara mbili ya Uchumi wote wa Africa ya Kusini ya leo mwaka 2025.

Kafulila anaendelea kwa kusema kama Africa ya Kusini ya leo Wanaumeme unaofikia Megawatt 60,000 huku sisi tukitarajia kujenga Uchumi marambili ya Uchumi huo wa Africa Kusini leo maana yake lazima tuwe na Umeme unaozidi umeme wa Africa ya Kusini ya leo ambao ni zaidi ya Megawatt 60,000.

Swali tunaloweza kujiuliza kwa pamoja,

Je, bila kushirikisha uvutaji wa mitaji na Ujuzi toka sekta binafsi PPP tunaweza kujenga Africa ya Kusini ya leo au zaidi?

Je, Tanzania kwa kutumia Kodi na Mikopo pekee tunaweza kufikia kumiliki umeme wa Megawatt zaidi ya elfu 60 ifikapo mwaka 2050 Jibu ni "HAPANA" hivyo lazima PPP ichukue nafasi kwenye ujenzi wa Tanzània kubwa kuliko Africa ya Kusini ya leo na hii ni kwa manufaa ya kizazi hiki na manufaa ya kizazi kijacho.











====
 
Jamaa ana VISION sijui kama utanielewa hapa
Vision ipi tofauti na visio ya Taifa 2050?

Hayo yote anayoongea Yako kwenye Vision ya Nchi ya 2050 hawezi.kija na vision yake na hakuna Nchi ya kuendeshwa na mawazo binafsi ya mtu mmja,haipo na hatutakiwi.kurudi zama za Mwendazake
 
Back
Top Bottom