Kafulila: Anayetaka kuwekeza TANESCO na aje,Tanzania inajengeka kwa Kasi mno mwaka 2050 tutahitaji zaidi ya Megawatt 60K wakati leo tuna Megawatt 4K

Kafulila: Anayetaka kuwekeza TANESCO na aje,Tanzania inajengeka kwa Kasi mno mwaka 2050 tutahitaji zaidi ya Megawatt 60K wakati leo tuna Megawatt 4K

===
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila akihojiwa katika Kipindi Cha One on One Cha Wasafi TV amesema Tanzania katika miaka 25 ijayo inatarajia kujenga Uchumi mkubwa karibu mara mbili ya Uchumi wote wa Africa ya Kusini ya Leo.

Kafulila anaendelea kwa kusema kama Africa ya Kusini ya leo Wana Umeme unaofikia Megawatt 60,000 huku sisi tukitarajia kujenga Uchumi marambili ya Uchumi huo wa Africa Kusini leo maana yake lazima tuwe na Umeme unaozidi umeme wa Africa ya Kusini ya leo ambao ni zaidi ya Megawatt 60,000.

Swali tunaloweza kujiuliza kwa pamoja, ni Je, bila kushirikisha mitaji na Ujuzi toka sekta binafsi PPP Tanzania kwa kutumia Kodi na Mikopo pekee tunaweza kufikia kumiliki umeme wa Megawatt zaidi ya 60 ifikapo mwaka 2050 Jibu ni "HAPANA" lazima PPP ichukue nafasi kwenye hili kwa manufaa ya kizazi hiki na manufaa ya kizazi kijacho.

View attachment 3202423

====
Hiyo Mwegawatt 4 k ilifija lini? Acheni uzindukaye, nchi ina 1.6k Mega watt na hitaji toshelezi ni 2.6+k MW
 
Huyu Kafulila mbona anawaza tofauti kabisa na viongozi wengine wa Serikali hii!!!!!!
Kafulila anakitu Cha ziada TISS mzingatieni huyu jamaa atawafaa sana huko mbeleni
Watanzania hawawapendi wale wasomi wenye ubunifu vichwani wanaishia kuwapiga vipapai.

Lakini huyu kwao Kigoma anayajua masuala hayo ya 'kienyeji'.
 
Katika waongo wabobezi Kafulila yumo

Hivi sisi tawaweza jenga uchumi.mkubwa mara mbili kuliko wa Africa ya kusini kuhitaji umeme mara mbili ya wa Afrika ya kusini?

Uchumi wa Africa kusini ndio mkubwa kwa bara zima la Africa ns sababu uchumi wao ni wa viwanda vikubwa na wamiliki wa hivyo viwanda vikubwa ni wazungu sio waafrika

Makampuni kibao ya ulaya na marekani wana partnerships ns wazungu wa Africa ya kusini na ku export sana Ulaya na Marekani nk

Sisi hapa tuna uchumi gani wa kuizidi Africa kusini ? Huu wa kutegemea viwanda vya Sido vya wahindi,waarabu na wachina? Hadi tuhitaji umeme mara mbili ya wa kwao

Kafulila kaamua kuwa dalali kwa kujenga hata hoja zisizo na akili kabisa
Unajua ukubwa wa rasilimali zilizopo katika ardhi ya Tanzania ambazo bado hazijatumika?. Punguza unyonge wa kujidharau.
 
===
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila akihojiwa katika Kipindi Cha One on One Cha Wasafi TV amesema Tanzania katika miaka 25 ijayo inatarajia kujenga Uchumi mkubwa karibu mara mbili ya Uchumi wote wa Africa ya Kusini ya Leo.

Kafulila anaendelea kwa kusema kama Africa ya Kusini ya leo Wana Umeme unaofikia Megawatt 60,000 huku sisi tukitarajia kujenga Uchumi marambili ya Uchumi huo wa Africa Kusini leo maana yake lazima tuwe na Umeme unaozidi umeme wa Africa ya Kusini ya leo ambao ni zaidi ya Megawatt 60,000.

Swali tunaloweza kujiuliza kwa pamoja, ni Je, bila kushirikisha mitaji na Ujuzi toka sekta binafsi PPP Tanzania kwa kutumia Kodi na Mikopo pekee tunaweza kufikia kumiliki umeme wa Megawatt zaidi ya 60 ifikapo mwaka 2050 Jibu ni "HAPANA" lazima PPP ichukue nafasi kwenye hili kwa manufaa ya kizazi hiki na manufaa ya kizazi kijacho.

View attachment 3202423

====
Nadhani mfanye pia review ya bei ya umeme wa Tanzània kwani ni kubwa
 
Waruhusu unanzishwaji wa kampuni shindani, Tanesco imedumaa ichangamshwe.
 
Back
Top Bottom