Kafulila: Anayetaka kuwekeza TANESCO na aje,Tanzania inajengeka kwa Kasi mno mwaka 2050 tutahitaji zaidi ya Megawatt 60K wakati leo tuna Megawatt 4K

Vision ipi tofauti na visio ya Taifa 2050?

Hayo yote anayoongea Yako kwenye Vision ya Nchi ya 2050 hawezi.kija na vision yake na hakuna Nchi ya kuendeshwa na mawazo binafsi ya mtu mmja,haipo na hatutakiwi.kurudi zama za Mwendazake
Hiyo ni vision ya taifa au ya ccm?
 
Kafulila ana ndoto hizo,ni kweli umeme tulionao kibindoni,kwa miaka 5 ijayo hautatosha kabisa ukuzaji viwanda vikubwa.

Lakini Mungu aja tutupa kwa kutumia rasilimali zetu tuna uwezo wa kufua hata Mega Watt 200,000 na zaidi kwa vyanzo hivi.:-
1.Kufua umeme kwa kujenga mitambo midogo midogo ya nuclear kutokana na utitili wa madini ya uranium yanayopatikana maeneo mbali mbali nchini kwetu.
Serikali ya Uganda inayoongozwa na Museveni imeishatenga eneo mahususi la kujenga mitambo ya kufua umeme wa nuclear.
Mradi huu PPP hatumuhitaji kwa maslahi mapana ya taifa letu.
Bila kumungunya maneno bingwa wa kujenga mitambo salama na bila masharti magumu ni France.

2.Solar power,Wind turbine Power,Geothermal power,Battery Power n.k serikali na taasisi binafsi wanaweza kuzalisha nishati ya kututosheleza sisi na hata majirani zetu kuwaunganisha kwenye grid ya taifa.
Lakini bado tuna machungu ya makampuni binafsi za Richmond, IPTL,Songas.
Ni bora kwanza kuunda sheria,au kanuni zenye kumlinda mtumiaji asinyonywe kama huku nyuma.

Mwisho Kafulila tumia muda huu kuishawishi serikali kujenga uwezo wa wananchi waweze kusimamia na kumiliki miradi mikubwa mikubwa.
 
Ndio JNHPP pekee tuna 2,100
Kabla tuliokuwa na Megawatt zaidi ya 1,000 bado kule Maragalasi etc
Kwa uhalisia wa mambo na endapo bwawa la Nyerere litakamisha uzalishaji tutakuwa na up to ~3,500 MW.
 
Sio swala la Mungu kukutupa au hapana Bali matumizi ya akili kwenye Rasilimali zilizopo.

Tanzania haijawahi kuwa na ushamba wa vyanzo vya Nishati hata siku Moja Wala watu wa kutekeleza hayo.

As we speak miradi kadhaa ya vyanzo vipya inaendelezwa na mingine Iko kwenye hatua za maandalizi.
 
Richmond, Songas, IPTL kwa ufupi ni aibu kubwa,just to refresh your memory.
Miradi mingine inayoendelea ni midogo sana .Mtoa hoja alisema unatoa 4,000 MW,reference to SA anazalisha by today 60,000 MW.na akasema by 2050 tumejipanga kuwa na uchumi mkubwa kuliko SA ya leo inayozalisha 60,000 MW.
Kwa lugha nyepesi to move from 4000 to above 60,000 inataka akili ya ziada.
Kusema tu miradi mingine in progress bila angalau kuonyesha ina capacity gani hujajibu swali la mleta hoja.
 
Hata Zambia, Mozambique,Zimbabwe wote wanazalisha megawatt nyingi kushinda Tanzania,Kenya nk achilia mbali South Africa.

Ukija kwenye Uchambuzi huyo Jamaa yenu ni mzinguzi.Hizo Nchi nimetaja hapo ni Mining superpowers hivyo extractive sectors zake ni high energy consumption ukilinganisha na viwanda vya kawaida so sio lazima na Wala sio realistic kwamba eti lazima tuwe na umeme kama huo Kwa sababu Tanznaia sio mining giant Wala sioni ikiwa hivyo.

Hata hivyo narudia kusema kinachotakiwa ni umeme upatikane swala la Ukubwa wa mradi sio big issue,tukikusanya miradi kidogo kidogo Mingi itazalisha tuu megawatts zinazotakiwa.

Sasa hivi Serikali inajaribi kuwa engage private sector lakini hawawezi kuja kama hakuna soko.
 
Tuna Megawatt 4K ?!!!!! Yaani huyu mtu ambaye hata basics anakosea ndio tunampa udalali wa kuuza moyo wa nchi (NISHATI)?!!!!

Ni kwamba Bwawa lingekamilika tunge double capacity na kama wangekuwa na akili na busara badala ya kuendelea kuwa madalali wa LPG inayotoka ughaibuni hizo hizo double capacity zingesaidia watu kupikia umeme kuliko kuchukua Kodi zao ili kununua gesi kutoka Nje...


Na kwa kufanya hivyo watu wangebakia na pesa za kutumia kwa shughuli nyingine

Na kama ni issue ya kuwekeza wangeweza kumtumia Mtanzania mwenyewe kila mtu mwenye makazi ili achangie uzalishaji na hivyo kuweza kupikia kwa kutumia gharama ya 0
 
Jambo la muhimu ni usimamizi wa miradi ya umeme kama serikali ikiamua kujenga miradi hii bila kushirikiana na sekta binafsi. Ila kama kuna uwezekano wa kutafuta muwekezaji kwenye suala la umeme basi iwe kampuni kutoka nchi ambayo Tanzania ina mahusiano mazuri. Sekta ya umeme ni nyeti sana na huenda ikaleta changamoto endapo nchi ngeni ikiamua kuiwekea Tanzania vizuizi vya kiuchumi kwasababu ya mahusiano yasiyo imara
 
Umeongea vema mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…