Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Dodoma. Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilichotwa katika Akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Katika tuhuma hizo, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.

Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.

Kafulila alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.

Mbunge huyo alisema fedha zilizoibwa katika Akaunti ya Escrow ni nyingi kuliko zile zilizoibwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT mwaka 2005.

"Pamoja na hilo, Watanzania wamekuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tanesco wakati ilipokuwa na mgogoro na IPTL walifika mahali wakafungua akaunti ya Escrow," alisema.

Mbunge huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2004 na hadi jana, akaunti ile ilishafikia Dola za Marekani 122 milioni," alisema Kafulila.

Alisema fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwapo kati ya IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.

Alitaka jambo hilo liingie kwenye rekodi kwa kuwa linahusu BoT na vigogo akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na pia Waziri wa Fedha.

Alisema wakati Tanesco ikidaiwa madeni zaidi ya Sh400 bilioni, viongozi hao wameidhinisha kugawanywa kwa fedha hizo kihuni jambo alilosema halivumiliki hata kidogo.

Kafulila alisema fedha hizo zilichotwa na Kampuni ya PAP aliyosema ya "Singasinga na ya kitapeli" ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu. Alisema fedha hizo hazikupaswa kuchukuliwa kwa

kuwa kulifanyika udanganyifu mkubwa kwamba PAP ilikuwa imenunua IPTL wakati jambo hilo si la kweli.
Alisema IPTL ilikuwa na makubaliano ya kufanya kazi kwa kampuni mbili ambazo ni VIP Engineering ya Tanzania iliyokuwa na hisa asilimia 30 na Mecmer ambayo ilikuwa na asilimia 70 ya hisa.

Hata hivyo, alidai kuwa anao ushahidi kuwa PAP ilikuwa imenunua hisa za VIP na hakukuwa na vielelezo vya kununua Mecmer kwa kuwa kampuni hiyo tayari ilishapoteza uhalali wake kwa kuwa ilikuwa chini ya muflisi nchini Malaysia.

Aliliambia Bunge kuwa wakati wa uchukuaji wa fedha hizo kutoka BoT, ilipaswa kulipiwa kodi lakini zilichukuliwa kinyemela bila hata ya kulipiwa kodi.

Alisema TRA iliiandikia Hazina na nakala kwa BoT kwamba wakati wa kulipa fedha hizo lazima kodi ikatwe, lakini cha ajabu hilo halikufanyika licha ya kukumbushwa.

kafulilal.png

"Kwa mfano, tulimwita Gavana katika kikao chetu cha Kamati ya Uchumi pale Bagamoyo na alikiri kuwa alibanwa na viongozi wa juu kiasi cha kushindwa kufurukuta, kwa hali kama hiyo Naibu Spika unategemea nini?" alihoji.

Kafulila alisema, Gavana katika kikao hicho alikiri kuwa, kulikuwa na presha (shinikizo) ambazo asingeweza kuzizuia na kuwa alikuwa amejitahidi kwa kiasi kikubwa hadi kufikia alipofika.

Alisema ISCID lilitoa hukumu ndogo Februari, mwaka huu kuwa Tanesco na IPTL wakae pamoja na kupitia hesabu zao namna watakavyogawanya fedha hizo na walipewa siku 60 ambazo mwisho wake ulikuwa jana.

Aliituhumu Tanesco kuwa katika makubaliano hayo ilikataa kukaa meza moja na kufanya hesabu za namna ya kulipana jambo alilosema linaonyesha ilidhamiria kufanya hivyo.

"Kwa sababu wanajua kuwa fedha ile ilishaliwa na wajanja wachache, Mheshimiwa Waziri Mkuu, hili kwa vyovyote halikubaliki na halivumiliki kwa sababu Dola122 milioni ni zaidi ya Sh200 bilioni ambazo ni nyingi kuliko za EPA, lazima litoke na mtu."

Alisema hayuko tayari kuona fedha hizo zikitafunwa bila ya utaratibu na akashangazwa kuona Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), akishindwa kuchukua hatua.

Akikoleza moto jioni katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu alimwita tena Kafulila kutoa ufafanuzi wa hoja yake aliyoitoa mchana, ambayo iliombewa mwongozo na Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina kwamba Gavana alishinikizwa kutoa fedha hizo.

Wakati wa mwongozo huo, Kafulila hakuwapo na ndiyo sababu ya Mwenyekiti kumpa nafasi ya kufuta kauli yake kuwa Gavana alishinikizwa. Hata hivyo, Kafulila alikazia akisema alishinikizwa kutoa fedha hizo.

"Gavana aliwahi kuniambia, mnanionea bure. Kulikuwa na presha kubwa sana kuhusu fedha hizi… ukweli ni kwamba IPTL inabadilishwa tu rangi na watendaji ni walewale."

Baada ya Kafulila kuzungumza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kusema: "Tuhuma dhidi ya Gavana wa Benki Kuu zinatolewa kwa kuwa hawezi kuingia bungeni kujitetea.

"Lakini Gavana tulimuuliza na akakanusha kuwa aliwahi kuyatamka hayo maneno na kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni atakuja kufafanua jambo hili kesho (leo) katika hotuba yake," alisema Lukuvi.

Hata hivyo, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisimama kuomba mwongozo akisema: "Kamati ya Bunge iundwe ili tuchunguze fedha hizi za Escrow zimekwenda wapi? Kafulila ana ushahidi wa kutosha, kwa nini hamtaki athibitishe?

"Vikao vyote vya kamati vinawekewa kwenye kumbukumbu rasmi (hansard) ili kujua kama Gavana alitoa maneno hayo ama hakutoa, iundwe kamati ijulikane mbivu na mbichi na wezi wa fedha za Escrow tunao humu ndani ya Bunge."

Chanzo: Mwananchi

===================================================

SOMA PIA:

JANUARY - AUGUST 2014
SEPTEMBER - OCTOBER 2014
NOVEMBER 2014
DECEMBER 2014
JANUARY - MARCH 2015
APRIL - JUNE 2015
JULY - DECEMBER 2015
JANUARY - JUNE 2016
JULY - DECEMBER 2016

2017
2018
2019
2020
2021
2022 - 2025
 
HIvi kwanini viongozi wakumbwa wa serikali wany'any'anie swala hili lichunguzwe na takukuru pamoja na CAG kwanini hawataki iundwe kamati maalumya bunge kuchunguza kisanga hichi kuna nini hapa wanachoficha..wakti cc wote ni mashaidi ya kuwa Takukuru huwa c wa kweli kwenye ripoti zao mf..kashfa ya Richmond,Epa na nk na pia upo zipo ripoti kadhaa za uchunguzi zilizotupwa kwenye droo za ofcn serikrini bila ya wananchi kujua ukweli....!!!
 
Mimi kama mtanganyika nina machungu sana juu ya ubadhirifu uliofanyika IPTL,nashauri serikali sikivu kama inavyoitwa iundwe tume mchanganyiko ukweli ujulikane na fedha zirudishwe mara moja
 
Nyinyi hamuielewi salakata la IPTL na ESCROW account, aliyeruhusu ESCROW account ifungwe ni Mahakama ambapo jaji Utamwa wa Mahakama Kuu ndiye aliyetoa hukumu hiyo na kudai fedha zote alipwe IPTL na kuanzia September mwaka jana IPTL itakuwa chini ya Kampuni ya Pan Africa Power Solution na mwenye madai yeyote aende PAP (PAn Africa Power Solution). SASA huyu Kafulila anabisha na kuupinga uamuzi wa Mahakama mbona ule uamuzi wa Mahakama wa kumrejeshea ubunge wake hakuukataa au kwa sababu fedha za Nimrod Mkono alizochota TANESCO katika kesi ya IPTL isiyokwisha amemgawia kidogo na Kafulila kaamua kulewa kabisa na kufunga macho na masikio. kama Kafulila hata kusikia basi Watanzania namba mjue kwamba sisi Wafanyakazi wa TANESCO tumechoshwa na Nimrod Mkono kutufilisi fedha za Shirika huku akiwahonga wakubwa huko nyuma aendelee kubaki TANESCO lakini Muhongo amemuondoa ndiyo ameanza kuwatumia akina Zitto, Kafulila na Mnyika ili waichafue Wizara mnafikiri hawa ni wale Mawaziri goi goi mliowazoea kuwagonga, safari hii mmegonga mwamba!!!!! Muhongo hahongeki ng'ooo na Maswi pia

WATANZANIA AMKENI ACHENI KULALA TUSIKUBALI KINA MKONO NA ZITTO WAENDELEE KUTUDANGANYA.
 
Pesa imeshaenda kwenye uchaguzi.

Tuachane nayo.
 
&&&&&&&&&&DON'T CRY ME FOR ME TANZANIAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!
THE TRUTH'S THEY'VE ALREADY LEFT YOU..

Ahsanteeni.....!!
 
Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

kafulila.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila akichangia mjadala bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Na Habel Chidawali na Sharon Sauwa, Mwananchi

Posted Ijumaa,Mei9 2014 saa 9:15 AM

Kwa ufupi

  • Asema kashfa ya Fedha za Akaunti ya Escrow ni kubwa kuliko ya EPA, ataka iundwe tume ya Bunge, Pinda kutoa majibu leo.

Dodoma: Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilichotwa katika Akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Katika tuhuma hizo, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.

Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.

Kafulila alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.

Mbunge huyo alisema fedha zilizoibwa katika Akaunti ya Escrow ni nyingi kuliko zile zilizoibwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT mwaka 2005.

"Pamoja na hilo, Watanzania wamekuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tanesco wakati ilipokuwa na mgogoro na IPTL walifika mahali wakafungua akaunti ya Escrow," alisema.

Mbunge huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2004 na hadi jana, akaunti ile ilishafikia Dola za Marekani 122 milioni," alisema Kafulila.

Alisema fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwapo kati ya IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.

Alitaka jambo hilo liingie kwenye rekodi kwa kuwa linahusu BoT na vigogo akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na pia Waziri wa Fedha.

Alisema wakati Tanesco ikidaiwa madeni zaidi ya Sh400 bilioni, viongozi hao wameidhinisha kugawanywa kwa fedha hizo kihuni jambo alilosema halivumiliki hata kidogo.

Kafulila alisema fedha hizo zilichotwa na Kampuni ya PAP aliyosema ya "Singasinga na ya kitapeli" ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu.

Alisema fedha hizo hazikupaswa kuchukuliwa kwa kuwa kulifanyika udanganyifu mkubwa kwamba PAP ilikuwa imenunua IPTL wakati jambo hilo si la kweli.

Alisema IPTL ilikuwa na makubaliano ya kufanya kazi kwa kampuni mbili ambazo ni VIP Engineering ya Tanzania iliyokuwa na hisa asilimia 30 na Mecmer ambayo ilikuwa na asilimia 70 ya hisa.

Hata hivyo, alidai kuwa anao ushahidi kuwa PAP ilikuwa imenunua hisa za VIP na hakukuwa na vielelezo vya kununua Mecmer kwa kuwa kampuni hiyo tayari ilishapoteza uhalali wake kwa kuwa ilikuwa chini ya muflisi nchini Malaysia.

Aliliambia Bunge kuwa wakati wa uchukuaji wa fedha hizo kutoka BoT, ilipaswa kulipiwa kodi lakini zilichukuliwa kinyemela bila hata ya kulipiwa kodi.

Alisema TRA iliiandikia Hazina na nakala kwa BoT kwamba wakati wa kulipa fedha hizo lazima kodi ikatwe, lakini cha ajabu hilo halikufanyika licha ya kukumbushwa.

"Kwa mfano, tulimwita Gavana katika kikao chetu cha Kamati ya Uchumi pale Bagamoyo na alikiri kuwa alibanwa na viongozi wa juu kiasi cha kushindwa kufurukuta, kwa hali kama hiyo Naibu Spika unategemea nini?" alihoji.

Kafulila alisema, Gavana katika kikao hicho alikiri kuwa, kulikuwa na presha (shinikizo) ambazo asingeweza kuzizuia na kuwa alikuwa amejitahidi kwa kiasi kikubwa hadi kufikia alipofika.

Alisema ISCID lilitoa hukumu ndogo Februari, mwaka huu kuwa Tanesco na IPTL wakae pamoja na kupitia hesabu zao namna watakavyogawanya fedha hizo na walipewa siku 60 ambazo mwisho wake ulikuwa jana.

Aliituhumu Tanesco kuwa katika makubaliano hayo ilikataa kukaa meza moja na kufanya hesabu za namna ya kulipana jambo alilosema linaonyesha ilidhamiria kufanya hivyo.

"Kwa sababu wanajua kuwa fedha ile ilishaliwa na wajanja wachache, Mheshimiwa Waziri Mkuu, hili kwa vyovyote halikubaliki na halivumiliki kwa sababu Dola122 milioni ni zaidi ya Sh200 bilioni ambazo ni nyingi kuliko za EPA, lazima litoke na mtu."

Alisema hayuko tayari kuona fedha hizo zikitafunwa bila ya utaratibu na akashangazwa kuona Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), akishindwa kuchukua hatua.

Akoleza moto jioni

Katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu alimwita tena Kafulila kutoa ufafanuzi wa hoja yake aliyoitoa mchana, ambayo iliombewa mwongozo na Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina kwamba Gavana alishinikizwa kutoa fedha hizo.

Wakati wa mwongozo huo, Kafulila hakuwapo na ndiyo sababu ya Mwenyekiti kumpa nafasi ya kufuta kauli yake kuwa Gavana alishinikizwa. Hata hivyo, Kafulila alikazia akisema alishinikizwa kutoa fedha hizo.

"Gavana aliwahi kuniambia, mnanionea bure. Kulikuwa na presha kubwa sana kuhusu fedha hizi… ukweli ni kwamba IPTL inabadilishwa tu rangi na watendaji ni walewale."

Baada ya Kafulila kuzungumza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kusema: "Tuhuma dhidi ya Gavana wa Benki Kuu zinatolewa kwa kuwa hawezi kuingia bungeni kujitetea.

"Lakini Gavana tulimuuliza na akakanusha kuwa aliwahi kuyatamka hayo maneno na kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni atakuja kufafanua jambo hili kesho (leo) katika hotuba yake," alisema Lukuvi.

Hata hivyo, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisimama kuomba mwongozo akisema: "Kamati ya Bunge iundwe ili tuchunguze fedha hizi za Escrow zimekwenda wapi? Kafulila ana ushahidi wa kutosha, kwa nini hamtaki athibitishe?

"Vikao vyote vya kamati vinawekewa kwenye kumbukumbu rasmi (hansard) ili kujua kama Gavana alitoa maneno hayo ama hakutoa, iundwe kamati ijulikane mbivu na mbichi na wezi wa fedha za Escrow tunao humu ndani ya Bunge."

CC: Tized, Mr Rocky, sifongo, Elly B, MziziMkavu, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, M ANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, joka Kuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, August, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Daudi Mchambuzi
 
Ni Sababu zipi zilizosababisha Kikwete asimuongozee CAG miezi mitatu kabla ya kustaafu ili amalizie ripoti hii? Je, huyo atayechukua nafasi hii CAG atateuliwa lini? Je, kama atateuliwa hivi karibuni atapewa maagizo na Kikwete kwamba kipaumbele chake cha kwanza kama CAG ni kukamilisha ripoti hiyo ya wizi wa shilingi bilioni 200 za ESCROW au ataambiwa ripoti hiyo haina umuhimu na hivyo kuendelea na "kazi nyingine" ambazo hazina kipaumbele kikubwa kama wizi huu wa pesa za ESCROW?
 
FaizaFoxy - Jf senior expert member " Hapo Zittoanaongelea Tax, tena ya Capital gain".

Zitto anaelewa sana kuhusu Tax evasion na Tax avoidance lakini hilo anajifanyakama halijui. Ananshangaza!

Hapo jamaa hawakufanya Tax evasion hapo ni simply Tax avoidance, kisheria.

Hakuna ujanja hapo, kama hawakufanya evasion ni halali kabisa.

Zitto anachoshindwa kueleza ni kuwa IPTL ilikuwa na mgogoro na kampuni yaKitanzania, kaingia Singasinga kaiona opportunity na kajuwa vipi atatatuwa huomgogoro, kaongea nao wamekubalina kawanunua kawalipa, kavuta fedha walizokuwawalipwe wao.

Kinachofata hapo ni uhalali wa tx na ndio anauongelea Zitto, kachimbuwa kakutahakuna tzx evasion kuna tax avoidance ambayo kisheria ni halali.

Sijui msichokielewa anachoongelea Zitto zaidi ya hicho ni nini?

Nadhani, Zitto angekuwa kidogo mjanja asingeongelea hilo la kampuni kuuzwamillion 6, unless anajuwa anachokifanya ila anataka ku divert msimamo, kunakila uwezekano na yeye kavuta au anataka kuvuta kwa singa na IPTL nahuyoMtanzania mwingine ambae hatajwi sana humu, lakini yeye ndio master-mind wahuu mkorogano.

Hapo sasa hivi kuna kila mtu kutaka kuvuta kwa Singa kwa kupiga makelele.

My Take:
Nasema huyo Mtanzania ni mastemind kwa sababu yeye alifikiri akiwabana sanaIPTL watakubali yaishe wachukuwe fedha wagawane halafu mitambo yote atabakinayo yeye aanze kuchuma peke yake kiulaini.

Bahati nzuri au mbaya, Singa kaliona hilo akaingia kati na kuna kila sababukakubaliana na IPTL kuwa wataumizwa, yeye ana njia mbadala watakuwa ni win winsituation, pesa watapata na mitambo haitopotea na wamuamini yeye, na ndichokilichofanyika.

Hapo aliyeumia ni Mtanzania mwenzetu, tena si kaumia kwa kuwa hajapata faida yabure, la hasha, faida kapata ya bure tena kubwa sana, kwani yeye hajatia fedhayake katika hili sakata, yeye alikuwa kama godfather tu waku facilitate mambondani ya Tanzania. Ndiyo norm kwa biashara zote kubwa duniani.

Alichoumia ni pale alipotaka kubana moaka mitambo yote ibaki kwake. Kataka kulakiharamu zaidi, ndipo Singa alipoingia na ku rescue.

Sasa, Mbnde kuona hivyo ni lazima apigane, kwani kwa sasa fedha ya kuwalishawapayukaji hovyo kama akina Tumbili anayo, na afanye nini zaidi? anachofanyakama kukosa tukose wote, lakini amechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Mwisho wa siku, kisheria ataibuka Singa kidedea, labda afanyiwe umafia. NaSinga si mdogo huyo, Tanzania anaijuwa juu chini, kaishi sana pande za Iringa,kama kuna mtu anaikumbuka RCC Iringa, basi ni hao akina Singa si wageni kabisaTanzania hii.

Mengine yote ni kubwabwaja, porojo na kuhororoja, kuna mshiko wa watukunyamazishwa na ndiyo maana unasikia kelele.

Hakuna wizi hapo wa mali ya umma kisheria, kuna "opportunity" naWatanzania kama ujuavyo ni ma "opportunists" kama fisi wanavyongojamifupa au makopangola wanavyoona mzoga, hawachelewi! ndicho kilichopo.

Ni Sababu zipi zilizosababisha Kikwete asimuongozee CAG miezi mitatu kabla ya kustaafu ili amalizie ripoti hii? Je, huyo atayechukua nafasi hii CAG atateuliwa lini? Je, kama atateuliwa hivi karibuni atapewa maagizo na Kikwete kwamba kipaumbele chake cha kwanza kama CAG ni kukamilisha ripoti hiyo ya wizi wa shilingi bilioni 200 za ESCROW au ataambiwa ripoti hiyo haina umuhimu na hivyo kuendelea na "kazi nyingine" ambazo hazina kipaumbele kikubwa kama wizi huu wa pesa za ESCROW?

Muhongo ni mtu makini sana na mpenda maendeleo,kitendo cha kufunga mirija ya kifisadi ndani ya wizara ya nishati na madini waliyokuwa wanatumia kujinufaisha na kuifilisi nchi,sasa kinachofanyika hapa ni kumchafua Mh.waziri kwa jamii ili aonekane si lolote.'NI BORA UTUMWA WA KUJITUMA KULIKO UTUMWA WA KUTUMIWA.
 
Back
Top Bottom