Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

Ni Sababu zipi zilizosababisha Kikwete asimuongozee CAG miezi mitatu kabla ya kustaafu ili amalizie ripoti hii? Je, huyo atayechukua nafasi hii CAG atateuliwa lini? Je, kama atateuliwa hivi karibuni atapewa maagizo na Kikwete kwamba kipaumbele chake cha kwanza kama CAG ni kukamilisha ripoti hiyo ya wizi wa shilingi bilioni 200 za ESCROW au ataambiwa ripoti hiyo haina umuhimu na hivyo kuendelea na "kazi nyingine" ambazo hazina kipaumbele kikubwa kama wizi huu wa pesa za ESCROW?
mkuu naoana umeingilia mpaka kazi za raisi
ongera kwa kujipa majukumu ambayo c yako
 
Kafulila anafahamu kuwa iptl ndio kampuni pekee
inayookoa fedha za watanzania kwenye nishati kwasababu ya
kuwauzia umeme kwa bei nafuu kuliko kampuni anayoipigia
debe na iliyomtuma kuichafua iptl yaani symbioon ambayo
inaiuzia tanesco umeme unit moja kwa zaidi ya elfu moja
wakati iptl inaiuzia umeme tanesco chini ya shiling mia tano
kwa unit na imeanza mazungumzo kushusha umeme hadi sh 90
kwa unit,je haoni anatumika vibaya na kampuni yenye wivu
wa kibiashara kuchafua iptl ambayo ni mkombozi wa tanzania

mimi naic jamaa anajitoa fahamu kabisaa
Mkuu kafulila anajitaidi kupambana kupitia mitandao ili ajisafishe kwa ajapewa pesa na kina mkono na rostam
ila mkuu kafulila ngoma ngumu nibora kujiepusha mapema na hili sakata mkuu litakuchafua kabisa kisiasa
 
Kustaafishwa kwa mkaguzi na mthibiti wa pesa za serikali na umma ni mwendelezo wa kufunika kile alichokiibuka katika uchunguzi na atakayechateuliwa sasa ni yule atakayaficha madhambi yanayotendwa na serikali ya CCM.

mkuu weka ushaidi mbele sio unaongea tu kama mbayuwayu
 
Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

kafulila.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila akichangia mjadala bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Na Habel Chidawali na Sharon Sauwa, Mwananchi

Posted Ijumaa,Mei9 2014 saa 9:15 AM

Kwa ufupi

  • Asema kashfa ya Fedha za Akaunti ya Escrow ni kubwa kuliko ya EPA, ataka iundwe tume ya Bunge, Pinda kutoa majibu leo.

Dodoma: Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilichotwa katika Akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Katika tuhuma hizo, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.

Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.

Kafulila alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.

Mbunge huyo alisema fedha zilizoibwa katika Akaunti ya Escrow ni nyingi kuliko zile zilizoibwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT mwaka 2005.

“Pamoja na hilo, Watanzania wamekuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tanesco wakati ilipokuwa na mgogoro na IPTL walifika mahali wakafungua akaunti ya Escrow,” alisema.

Mbunge huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2004 na hadi jana, akaunti ile ilishafikia Dola za Marekani 122 milioni,” alisema Kafulila.

Alisema fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwapo kati ya IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.

Alitaka jambo hilo liingie kwenye rekodi kwa kuwa linahusu BoT na vigogo akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na pia Waziri wa Fedha.

Alisema wakati Tanesco ikidaiwa madeni zaidi ya Sh400 bilioni, viongozi hao wameidhinisha kugawanywa kwa fedha hizo kihuni jambo alilosema halivumiliki hata kidogo.

Kafulila alisema fedha hizo zilichotwa na Kampuni ya PAP aliyosema ya “Singasinga na ya kitapeli” ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu.

Alisema fedha hizo hazikupaswa kuchukuliwa kwa kuwa kulifanyika udanganyifu mkubwa kwamba PAP ilikuwa imenunua IPTL wakati jambo hilo si la kweli.

Alisema IPTL ilikuwa na makubaliano ya kufanya kazi kwa kampuni mbili ambazo ni VIP Engineering ya Tanzania iliyokuwa na hisa asilimia 30 na Mecmer ambayo ilikuwa na asilimia 70 ya hisa.

Hata hivyo, alidai kuwa anao ushahidi kuwa PAP ilikuwa imenunua hisa za VIP na hakukuwa na vielelezo vya kununua Mecmer kwa kuwa kampuni hiyo tayari ilishapoteza uhalali wake kwa kuwa ilikuwa chini ya muflisi nchini Malaysia.

Aliliambia Bunge kuwa wakati wa uchukuaji wa fedha hizo kutoka BoT, ilipaswa kulipiwa kodi lakini zilichukuliwa kinyemela bila hata ya kulipiwa kodi.

Alisema TRA iliiandikia Hazina na nakala kwa BoT kwamba wakati wa kulipa fedha hizo lazima kodi ikatwe, lakini cha ajabu hilo halikufanyika licha ya kukumbushwa.

“Kwa mfano, tulimwita Gavana katika kikao chetu cha Kamati ya Uchumi pale Bagamoyo na alikiri kuwa alibanwa na viongozi wa juu kiasi cha kushindwa kufurukuta, kwa hali kama hiyo Naibu Spika unategemea nini?” alihoji.

Kafulila alisema, Gavana katika kikao hicho alikiri kuwa, kulikuwa na presha (shinikizo) ambazo asingeweza kuzizuia na kuwa alikuwa amejitahidi kwa kiasi kikubwa hadi kufikia alipofika.

Alisema ISCID lilitoa hukumu ndogo Februari, mwaka huu kuwa Tanesco na IPTL wakae pamoja na kupitia hesabu zao namna watakavyogawanya fedha hizo na walipewa siku 60 ambazo mwisho wake ulikuwa jana.

Aliituhumu Tanesco kuwa katika makubaliano hayo ilikataa kukaa meza moja na kufanya hesabu za namna ya kulipana jambo alilosema linaonyesha ilidhamiria kufanya hivyo.

“Kwa sababu wanajua kuwa fedha ile ilishaliwa na wajanja wachache, Mheshimiwa Waziri Mkuu, hili kwa vyovyote halikubaliki na halivumiliki kwa sababu Dola122 milioni ni zaidi ya Sh200 bilioni ambazo ni nyingi kuliko za EPA, lazima litoke na mtu.”

Alisema hayuko tayari kuona fedha hizo zikitafunwa bila ya utaratibu na akashangazwa kuona Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), akishindwa kuchukua hatua.

Akoleza moto jioni

Katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu alimwita tena Kafulila kutoa ufafanuzi wa hoja yake aliyoitoa mchana, ambayo iliombewa mwongozo na Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina kwamba Gavana alishinikizwa kutoa fedha hizo.

Wakati wa mwongozo huo, Kafulila hakuwapo na ndiyo sababu ya Mwenyekiti kumpa nafasi ya kufuta kauli yake kuwa Gavana alishinikizwa. Hata hivyo, Kafulila alikazia akisema alishinikizwa kutoa fedha hizo.

“Gavana aliwahi kuniambia, mnanionea bure. Kulikuwa na presha kubwa sana kuhusu fedha hizi… ukweli ni kwamba IPTL inabadilishwa tu rangi na watendaji ni walewale.”

Baada ya Kafulila kuzungumza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kusema: “Tuhuma dhidi ya Gavana wa Benki Kuu zinatolewa kwa kuwa hawezi kuingia bungeni kujitetea.

“Lakini Gavana tulimuuliza na akakanusha kuwa aliwahi kuyatamka hayo maneno na kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni atakuja kufafanua jambo hili kesho (leo) katika hotuba yake,” alisema Lukuvi.

Hata hivyo, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisimama kuomba mwongozo akisema: “Kamati ya Bunge iundwe ili tuchunguze fedha hizi za Escrow zimekwenda wapi? Kafulila ana ushahidi wa kutosha, kwa nini hamtaki athibitishe?

“Vikao vyote vya kamati vinawekewa kwenye kumbukumbu rasmi (hansard) ili kujua kama Gavana alitoa maneno hayo ama hakutoa, iundwe kamati ijulikane mbivu na mbichi na wezi wa fedha za Escrow tunao humu ndani ya Bunge.”

CC: Tized, Mr Rocky, sifongo, Elly B, MziziMkavu, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, M ANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, joka Kuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, August, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Daudi Mchambuzi

Taarifa zaidi kuhusu akaunti ya Escrow

TAARIFA zaidi zimezidi kupatikana kuhusu sakata la Escrow, linalohusisha makubaliano baina ya serikali, Kampuni ya kufua umeme ya Independet Power Tanzania Limited (IPTL) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama wakala wa Escrow kuwa yalikuwa ni makubaliano ya kisheria.

Makubaliano hayo yalilenga kumaliza mgogoro wa kimaslahi baina ya wabia, ambao ni Kampuni ya VIP na Mechmar kutoka nchini Malaysia, ambapo VIP ilikuwa inamlalamikia mbia mwenzake kuhusu thamani ya hisa zake.

Hali hiyo ilisababishwa na mkataba wao, ambao ulikuwa ikimtaka kampuni ya VIP kufanya kazi za utekelezaji ikiwemo misamaha ya kodi, ofisi itakayofungwa mtambo huo wa uzalishaji umeme megawati 100, ambapo mtambo huo ulifungwa Tegeta.

Taarifa zaidi kuhusu mkataba huo, ilieleza kazi zitazofanywa na Kampuni ya VIP ni asilimia 30 ya
hisa zote huku Mechmar ikibaki na hisa ya asilimia 70 kutokana na kutoa mtaji wa uzalishaji umeme.

Kutokana na hali hiyo, VIP haikuwa tayari kuanzisha mgogoro wa kimaslahi baina yake na Mechmar, wakati kesi yao ikiendelea Mahakama Kuu ndipo VIP ikatoa pendekezo la kuzuia kulipwa kwa IPTL hadi mgogoro wao utakapoisha.

Pendekezo liliungwa mkono na serikali, ambaye ni mnunuzi wa umeme kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), na kutengeneza makubaliano kisheria ya pamoja yaliyoitwa ‘Escrow Agreement’ yaliyosainiwa na pande zote tatu ikiwemo serikali, IPTL na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ilikuwa kama wakala wa Escrow Julai 5, 2006.

Ilisema makubaliano hayo ya kisheria ilipelekea kufunguliwa kwa akaunti maalumu ya pamoja baina ya serikali, IPTL na BoT ili kutunza fedha zote za malipo ambazo IPTL walipaswa kulipwa kutokana na mauzo ya umeme waliokuwa wakiyafanya Tanesco kipindi chote cha mgogoro.

Katika makubaliano hayo, serikali iliingia kama mnunuzi wa umeme kupitia Tanesco na ilikuwa na wajibu wa kupeleka fedha katika akaunti ya Escrow badala ya kuwalipa IPTL moja kwa moja kama ilivyokuwa awali.

Ilieleza zaidi BoT wao walikuwa wakala wa Escrow na kazi yao ni kupokea, kutunza fedha na kutoa taarifa kwa pande zote zilizosaini makubaliano hayo huku IPTL yenyewe ikiwa ndio wazalishaji wa umeme.

Makubaliano hayo yalieleza kwamba, pindi mgogoro utakapoisha BoT itapaswa kutoa fedha hizo kwa IPTL ndani siku 60, baada ya pande zote kuafikiana.

Akizungumzia kuhusu Escrow, Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa IPTL/PAP, Joseph Makandege alisema wapo mbioni kuweka kila kitu katika wazi ili Watanzania wapate ukweli kuhusu Escrow.

Alisema Escrow lilikuwa jambo la kisheria baina ya wabia na serikali kama mpokea huduma, ambalo walilimaliza wao wenyewe kwa makubaliano yao ya kisheria.

“Hakuna kitu chochote ovu hapa, mengi yanayozungumzwa katika mitandao ni ya zamani na si mapya, ambayo yamemalizika kisheria,’’ alisema.

Hivyo, alisema IPTL/PAP ni kampuni makini isiyokuwa na chembe ya kifisadi na imefika hapo baada ya kupita hatua zote za kisheria, ikiwemo kununua hisa za VIP na Mechmar.

Alisema wanazidi kuwaomba watanzania, wawaamini na kuendelea kuwaamini kwa kuwa hakuna vitendo vya ufisadi.
 
  • [h=2]
    icon1.png
    Tuhuma za ufisadi ESCROW account, ukweli wote wawekwa wazi[/h]

    You, Pasco, massange and 1 others like this.

    Send PM

Ni Sababu zipi zilizosababisha Kikwete asimuongozee CAG miezi mitatu kabla ya kustaafu ili amalizie ripoti hii? Je, huyo atayechukua nafasi hii CAG atateuliwa lini? Je, kama atateuliwa hivi karibuni atapewa maagizo na Kikwete kwamba kipaumbele chake cha kwanza kama CAG ni kukamilisha ripoti hiyo ya wizi wa shilingi bilioni 200 za ESCROW au ataambiwa ripoti hiyo haina umuhimu na hivyo kuendelea na "kazi nyingine" ambazo hazina kipaumbele kikubwa kama wizi huu wa pesa za ESCROW?

Escrow lilikuwa jambo la kisheria baina ya wabia na serikali kama mpokea huduma, ambalo walilimaliza wao wenyewe kwa makubaliano yao ya kisheria.

“Hakuna kitu chochote ovu hapa, mengi yanayozungumzwa katika mitandao ni ya zamani na si mapya, ambayo yamemalizika kisheria.

Hivyo,IPTL/PAP ni kampuni makini isiyokuwa na chembe ya kifisadi na imefika hapo baada ya kupita hatua zote za kisheria, ikiwemo kununua hisa za VIP na Mechmar.
 
Litakosa wapi kufifia wakati CAG anasema amestaafu ripoti atakuja kumalizia CAG mpya ambaye hajulikani atateuliwa lini. Kikwete angeona umuhimu wa kuzungumzia kuhusu hili basi hata angesema kwamba kuna kipaumbele kikubwa kwa yeye kumteua CAG mpya ili amalizie ripoti hii haraka na kutufahamisha Watanzania kuhusu wizi huu mkubwa kuliko wa EPA au Meremeta, lakini wapi kauchuna kimyaaaaa!....HAYAMHUSU!!!!!

Basi Sawa
 
Kustaafishwa kwa mkaguzi na mthibiti wa pesa za serikali na umma ni mwendelezo wa kufunika kile alichokiibuka katika uchunguzi na atakayechateuliwa sasa ni yule atakayaficha madhambi yanayotendwa na serikali ya CCM.

Kwahyo weulitaka afanye kazi milele, achavisingizio vya kikafulila mara CAG kastaafu, mara ripoti imekabidhiwa ikulu. Sasahivi analazimisha nafasi ya CAG apewe yeye sababu kaibua sakata la iptl!! huyu si kichaa kwahyo hicho ndio kigezo cha kupata uCAG. Toeni maneno yenu mbofumbofu.
 
Tumeshasikia kashfa nyingi sana katika Nchi hii na tutaendelea kuzisikia ikiwa tu sisi tunaokashifiwa hatutafanya maamuzi magumu ya kubadili huu utaratibu wa kulalama na kuwa utaratibu wa kutenda, imefikia sehemu viongozi wetu hawana huruma tena na wanaowaongoza na sisi tunaoongozwa tubadilike.

Ipo hivi, mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu kutakuwa na picha za wagombea kila kona, jamani nani hajui picha na majina ya mafisadi hapa?.......tuachane nao.

Nakubaliana nawewe mkuu Nasisi wa jimbo la Kigoma Kusini tunaanza na David Kafulila maana kasahau tulichomtuma wanakigoma kusini anafanya aliyotumwa na Mkono, Mengi na Rostam sasa kama hao ndio wapiga kula waKIgoma Kusini tutaona.
 
Kustaafishwa kwa mkaguzi na mthibiti wa pesa za serikali na umma ni mwendelezo wa kufunika kile alichokiibuka katika uchunguzi na atakayechateuliwa sasa ni yule atakayaficha madhambi yanayotendwa na serikali ya CCM.

Hivi amestaafishwa , au amestaaf kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma?
 
Ni Sababu zipi zilizosababisha Kikwete asimuongozee CAG miezi mitatu kabla ya kustaafu ili amalizie ripoti hii? Je, huyo atayechukua nafasi hii CAG atateuliwa lini? Je, kama atateuliwa hivi karibuni atapewa maagizo na Kikwete kwamba kipaumbele chake cha kwanza kama CAG ni kukamilisha ripoti hiyo ya wizi wa shilingi bilioni 200 za ESCROW au ataambiwa ripoti hiyo haina umuhimu na hivyo kuendelea na "kazi nyingine" ambazo hazina kipaumbele kikubwa kama wizi huu wa pesa za ESCROW?

Mkuu ndo "imetoka" hiyo!!!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Si rahisi kupambana na mafisadi, hata hivyo mwisho wa siku ufisadi hushindwa kwa nguvu ya uma na baadaye utaanza kujijenga tena na mapambano huanza tena. Hakuna mwisho wa mapambano dhidi ya ufisadi.
Raia wema wanatakiwa kuendeleza mapambano dhidi ya mafisadi na mbwa wao!
Kwa kipindi hiki uzao wa mbwa wa mafisadi (vibaraka) umeongezeka sana, wapo wanaofugwa na wa kujitolea. Mtandao wao ni mkubwa, kuanzia ofisi za uma, taasisi binafsi na hata mitandao ya jamii.
 
Ni Sababu zipi zilizosababisha Kikwete asimuongozee CAG miezi mitatu kabla ya kustaafu ili amalizie ripoti hii? Je, huyo atayechukua nafasi hii CAG atateuliwa lini? Je, kama atateuliwa hivi karibuni atapewa maagizo na Kikwete kwamba kipaumbele chake cha kwanza kama CAG ni kukamilisha ripoti hiyo ya wizi wa shilingi bilioni 200 za ESCROW au ataambiwa ripoti hiyo haina umuhimu na hivyo kuendelea na "kazi nyingine" ambazo hazina kipaumbele kikubwa kama wizi huu wa pesa za ESCROW?

Wasiwasi ulionyesha unakosa mashiko kabisa, Kwani CAG ni one man Institution? Hakuna aliyekaimu? hakuna watumishi wengine waliochini ya CAG? JF senior member? Ndio mawazo yako kwamba kazi yenye kipaumbele ni iptl tu, basi wakimaliza ukaguzi wa iptl ofisi zifungwe!!!!!!
 
Nakubaliana nawewe mkuu. Mwisho ufisadi hushindwa/huumbuka, tumeone jinsi watanzania tulivyong'amua hila za mafisadi kupitia kibaraka wao Kafulila/ Tumbili. Pamoja tuunganishe nguvu kupambana na hawa wanaotutumia watanzania kama daraja la mafanikio yao yakiuchumi kwa hongo/fedha chafu za mafisadi kama Mbunge David Kafulila
 
TEAM KAFULILA, TEAM CAPTAIN "Bak" tunawatemesha buku 10 za mafisadi. Mnaitumia kinga ya bunge vibaya eehh! mnachukua hela za mafisadi wakina MKONO, MENGI na ROSTAM alafu mnaenda kuchefua watu bungeni. Mmetumika miaka mingi humu JF kufanikisha hila za kina MKONO sasa basi KAMANDA. teh teh teh teh kwi kwi kwi kwi, tunatia mchanga kitumbua chako mkuu BAK
 
si tuliambiwa kuwa ripoti hiyo ya pesa za ESCROW ilikabidhiwa kwa Kikwete? au ni ripoti ipi unaongelea?

Ni Sababu zipi zilizosababisha Kikwete asimuongozee CAG miezi mitatu kabla ya kustaafu ili amalizie ripoti hii? Je, huyo atayechukua nafasi hii CAG atateuliwa lini? Je, kama atateuliwa hivi karibuni atapewa maagizo na Kikwete kwamba kipaumbele chake cha kwanza kama CAG ni kukamilisha ripoti hiyo ya wizi wa shilingi bilioni 200 za ESCROW au ataambiwa ripoti hiyo haina umuhimu na hivyo kuendelea na "kazi nyingine" ambazo hazina kipaumbele kikubwa kama wizi huu wa pesa za ESCROW?
 
Acha upumbavu wako wewe mpiga debe wa mapanya na mafisi ndani ya chama chenu cha wahuni. Umeona huyo balozi wa UK kasema hadharani kwamba nchi za Wafadhili zimekataa kutoa pesa zao mpaka hatima ya hizi bilioni 200 ijulikane ukitilia maanani hii Serikali inayopiga kwamba haina pesa hata imefikia kukopa katika mabenki ya biashara ambayo riba zao ni kubwa sana kufikia IMF na WB kuionya Serikali kuachana na kukopa kwenye benki hizo kwani deni la Taifa linaongezeka kwa kasi ya kutisha. Upumbavu wako wapelekee hao walafi ndani ya chama chenu cha wahuni.

Wasiwasi ulionyesha unakosa mashiko kabisa, Kwani CAG ni one man Institution? Hakuna aliyekaimu? hakuna watumishi wengine waliochini ya CAG? JF senior member? Ndio mawazo yako kwamba kazi yenye kipaumbele ni iptl tu, basi wakimaliza ukaguzi wa iptl ofisi zifungwe!!!!!!
 
Hakuna sheria yoyote ile nchini inayokataza Watanzania kuhoji maamuzi ya Rais, kama ipo hebu tuwekee hapa na utufahamishe pia sheria hii ilipitishwa lini.

mkuu naoana umeingilia mpaka kazi za raisi
ongera kwa kujipa majukumu ambayo c yako
 
Nakubaliana nawewe mkuu Nasisi wa jimbo la Kigoma Kusini tunaanza na David Kafulila maana kasahau tulichomtuma wanakigoma kusini anafanya aliyotumwa na Mkono, Mengi na Rostam sasa kama hao ndio wapiga kula waKIgoma Kusini tutaona.
Mkuu umenifurahisha unasema Mkono,Rostam na Mengi ndio wamemtuma mbunge wako.................haya bhana ila kuumbuana kwao si unaona ni faida kwetu tunajua rangi zao.
 
Acha upumbavu wako wewe mpiga debe wa mapanya na mafisi ndani ya chama chenu cha wahuni. Umeona huyo balozi wa UK kasema hadharani kwamba nchi za Wafadhili zimekataa kutoa pesa zao mpaka hatima ya hizi bilioni 200 ijulikane ukitilia maanani hii Serikali inayopiga kwamba haina pesa hata imefikia kukopa katika mabenki ya biashara ambayo riba zao ni kubwa sana kufikia IMF na WB kuionya Serikali kuachana na kukopa kwenye benki hizo kwani deni la Taifa linaongezeka kwa kasi ya kutisha. Upumbavu wako wapelekee hao walafi ndani ya chama chenu cha wahuni.

Acha ujinga wewe! yaani minakutia uelevu alafu bado unakakamaa, Kwani Barozi wa UK ndio kitugani? Acha fikra fupi kama SISIMIZI. Barozi wa UK alituletea misisimamo wa nchi yake kuwa tuoane ndio watupe misaada, kwahyo nalo tulisikilize. Acha kupigia magoti mabeberu, sikuzote wanasimamia maslahi yao.
 
Back
Top Bottom