Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

Mpuuzi wewe!!! Rudi shule ukajifunze kuandika badala ya kukubali kutumiwa na hao mafisadi waliokuokota Kariakoo ulikokuwa ukiuza bangi na kukulipa ujira mdogo ili kuja kuandika pumba hapa jamvini. Hapa tunaongelea wizi wa bilioni 200 za ESCROW hatuongelei mambo ya kuoana mpumbavu mkubwa wee. Jifunze kusoma na kuelewa kilichoandikwa badala ya kukurupuka na kuanza kuropoka pumba. Mxciuuuuuuuuuuuuu

Acha ujinga wewe! yaani minakutia uelevu alafu bado unakakamaa, Kwani Barozi wa UK ndio kitugani? Acha fikra fupi kama SISIMIZI. Barozi wa UK alituletea misisimamo wa nchi yake kuwa tuoane ndio watupe misaada, kwahyo nalo tulisikilize. Acha kupigia magoti mabeberu, sikuzote wanasimamia maslahi yao.
 
Hakuna sheria yoyote ile nchini inayokataza Watanzania kuhoji maamuzi ya Rais, kama ipo hebu tuwekee hapa na utufahamishe pia sheria hii ilipitishwa lini.

umemkimbiza .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Unajua Mkuu Erythrocyte hawa wapumbavu wanaotumiwa na mapanya na mafisi wa chama cha wahuni wanajua wakija hapa na kutukana watu wakati mwingine hata matusi ya nguoni basi watawanyamazisha watu wote wanaoandika hapa kuhoji mambo mbali mbali yanayofanywa na hii Serikali dhalimu. Miaka ya nyuma posts kama hizo ulikuwa ukigusa kitufe cha "REPORT ABUSE" inafutwa mara moja na muhusika kupewa onyo au hata kufungiwa, siku hizi utagusa hicho kitufe hata mara milioni post haifutwi. Hivyo ustaarabu na uungwana ni kwa wale ambao wanauthamini vinginevyo ni jicho kwa jicho lakini kamwe siwezi kutumia matusi ya nguoni hapa.

umemkimbiza .
 
Last edited by a moderator:
Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

kafulila.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila akichangia mjadala bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Na Habel Chidawali na Sharon Sauwa, Mwananchi

Posted Ijumaa,Mei9 2014 saa 9:15 AM

Kwa ufupi

  • Asema kashfa ya Fedha za Akaunti ya Escrow ni kubwa kuliko ya EPA, ataka iundwe tume ya Bunge, Pinda kutoa majibu leo.

Dodoma: Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilichotwa katika Akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Katika tuhuma hizo, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.

Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.

Kafulila alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.

Mbunge huyo alisema fedha zilizoibwa katika Akaunti ya Escrow ni nyingi kuliko zile zilizoibwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT mwaka 2005.

“Pamoja na hilo, Watanzania wamekuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tanesco wakati ilipokuwa na mgogoro na IPTL walifika mahali wakafungua akaunti ya Escrow,” alisema.

Mbunge huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2004 na hadi jana, akaunti ile ilishafikia Dola za Marekani 122 milioni,” alisema Kafulila.

Alisema fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwapo kati ya IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.

Alitaka jambo hilo liingie kwenye rekodi kwa kuwa linahusu BoT na vigogo akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na pia Waziri wa Fedha.

Alisema wakati Tanesco ikidaiwa madeni zaidi ya Sh400 bilioni, viongozi hao wameidhinisha kugawanywa kwa fedha hizo kihuni jambo alilosema halivumiliki hata kidogo.

Kafulila alisema fedha hizo zilichotwa na Kampuni ya PAP aliyosema ya “Singasinga na ya kitapeli” ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu.

Alisema fedha hizo hazikupaswa kuchukuliwa kwa kuwa kulifanyika udanganyifu mkubwa kwamba PAP ilikuwa imenunua IPTL wakati jambo hilo si la kweli.

Alisema IPTL ilikuwa na makubaliano ya kufanya kazi kwa kampuni mbili ambazo ni VIP Engineering ya Tanzania iliyokuwa na hisa asilimia 30 na Mecmer ambayo ilikuwa na asilimia 70 ya hisa.

Hata hivyo, alidai kuwa anao ushahidi kuwa PAP ilikuwa imenunua hisa za VIP na hakukuwa na vielelezo vya kununua Mecmer kwa kuwa kampuni hiyo tayari ilishapoteza uhalali wake kwa kuwa ilikuwa chini ya muflisi nchini Malaysia.

Aliliambia Bunge kuwa wakati wa uchukuaji wa fedha hizo kutoka BoT, ilipaswa kulipiwa kodi lakini zilichukuliwa kinyemela bila hata ya kulipiwa kodi.

Alisema TRA iliiandikia Hazina na nakala kwa BoT kwamba wakati wa kulipa fedha hizo lazima kodi ikatwe, lakini cha ajabu hilo halikufanyika licha ya kukumbushwa.

“Kwa mfano, tulimwita Gavana katika kikao chetu cha Kamati ya Uchumi pale Bagamoyo na alikiri kuwa alibanwa na viongozi wa juu kiasi cha kushindwa kufurukuta, kwa hali kama hiyo Naibu Spika unategemea nini?” alihoji.

Kafulila alisema, Gavana katika kikao hicho alikiri kuwa, kulikuwa na presha (shinikizo) ambazo asingeweza kuzizuia na kuwa alikuwa amejitahidi kwa kiasi kikubwa hadi kufikia alipofika.

Alisema ISCID lilitoa hukumu ndogo Februari, mwaka huu kuwa Tanesco na IPTL wakae pamoja na kupitia hesabu zao namna watakavyogawanya fedha hizo na walipewa siku 60 ambazo mwisho wake ulikuwa jana.

Aliituhumu Tanesco kuwa katika makubaliano hayo ilikataa kukaa meza moja na kufanya hesabu za namna ya kulipana jambo alilosema linaonyesha ilidhamiria kufanya hivyo.

“Kwa sababu wanajua kuwa fedha ile ilishaliwa na wajanja wachache, Mheshimiwa Waziri Mkuu, hili kwa vyovyote halikubaliki na halivumiliki kwa sababu Dola122 milioni ni zaidi ya Sh200 bilioni ambazo ni nyingi kuliko za EPA, lazima litoke na mtu.”

Alisema hayuko tayari kuona fedha hizo zikitafunwa bila ya utaratibu na akashangazwa kuona Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), akishindwa kuchukua hatua.

Akoleza moto jioni

Katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu alimwita tena Kafulila kutoa ufafanuzi wa hoja yake aliyoitoa mchana, ambayo iliombewa mwongozo na Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina kwamba Gavana alishinikizwa kutoa fedha hizo.

Wakati wa mwongozo huo, Kafulila hakuwapo na ndiyo sababu ya Mwenyekiti kumpa nafasi ya kufuta kauli yake kuwa Gavana alishinikizwa. Hata hivyo, Kafulila alikazia akisema alishinikizwa kutoa fedha hizo.

“Gavana aliwahi kuniambia, mnanionea bure. Kulikuwa na presha kubwa sana kuhusu fedha hizi… ukweli ni kwamba IPTL inabadilishwa tu rangi na watendaji ni walewale.”

Baada ya Kafulila kuzungumza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kusema: “Tuhuma dhidi ya Gavana wa Benki Kuu zinatolewa kwa kuwa hawezi kuingia bungeni kujitetea.

“Lakini Gavana tulimuuliza na akakanusha kuwa aliwahi kuyatamka hayo maneno na kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni atakuja kufafanua jambo hili kesho (leo) katika hotuba yake,” alisema Lukuvi.

Hata hivyo, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisimama kuomba mwongozo akisema: “Kamati ya Bunge iundwe ili tuchunguze fedha hizi za Escrow zimekwenda wapi? Kafulila ana ushahidi wa kutosha, kwa nini hamtaki athibitishe?

“Vikao vyote vya kamati vinawekewa kwenye kumbukumbu rasmi (hansard) ili kujua kama Gavana alitoa maneno hayo ama hakutoa, iundwe kamati ijulikane mbivu na mbichi na wezi wa fedha za Escrow tunao humu ndani ya Bunge.”

CC: Tized, Mr Rocky, sifongo, Elly B, MziziMkavu, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, M ANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, joka Kuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, August, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Daudi Mchambuzi

Hili sakata, bila kumumunya maneno, kutikisa masikio wala kupepesa macho, lazima liende na mtu….haiwezekani hawa panya watafune fedha zote hizi za umma halafu wananchi tukae kimya! Mbivu na mabichi lazima zijulikane…Kafulila anao ushahidi mujarabu lakini WEZI hawataki kumpa nafasi kwa kuwa wanafahamu kwamba atawaumbua mchana kweupe. Hivi ni lini hawa panya wa CCM wataacha kutafuna fedha za watanzania?

magamba  panya road.jpg magamba mlevi.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mpuuzi wewe!!! Rudi shule ukajifunze kuandika badala ya kukubali kutumiwa na hao mafisadi waliokuokota Kariakoo ulikokuwa ukiuza bangi na kukulipa ujira mdogo ili kuja kuandika pumba hapa jamvini. Hapa tunaongelea wizi wa bilioni 200 za ESCROW hatuongelei mambo ya kuoana mpumbavu mkubwa wee. Jifunze kusoma na kuelewa kilichoandikwa badala ya kukurupuka na kuanza kuropoka pumba. Mxciuuuuuuuuuuuuu

Umepanic Kamanda, baada ya kuataki hoja yangu unaniataki mimi. Ila sishangai ni kawaida ya wajinga.
 
View attachment 188972 View attachment 188974

Kafulila kashatoa ushahidi wake kwa PCCB na CAG, Yeah! hili sakata linaondoka na KAFULILA maana anakesi ya madai mahakamani.
 
Muhongo ni mtu makini sana na mpenda maendeleo,kitendo cha kufunga mirija ya kifisadi ndani ya wizara ya nishati na madini waliyokuwa wanatumia kujinufaisha na kuifilisi nchi,sasa kinachofanyika hapa ni kumchafua Mh.waziri kwa jamii ili aonekane si lolote.'NI BORA UTUMWA WA KUJITUMA KULIKO UTUMWA WA KUTUMIWA.

Mkuu, acha kutetea WEZI...kama wanadhani kwamba wanachafuliwa kwanini wasikimbilie mahakamani wakaoge? Nawe umetumwa kuwatetea mafisadi wa CCM ama?
 
Kafulila kashatoa ushahidi wake kwa PCCB na CAG, Yeah! hili sakata linaondoka na KAFULILA maana anakesi ya madai mahakamani.

Linaondoka naye kwa namna gani wakati yeye ndiye anasaidia kuibua WEZI na kuwavua nguo hadharani? Wewe ungetamani hawa PANYA waendelee kuguguna mali za umma mpaka lini?
 
Mpuuzi wewe!!! Rudi shule ukajifunze kuandika badala ya kukubali kutumiwa na hao mafisadi waliokuokota Kariakoo ulikokuwa ukiuza bangi na kukulipa ujira mdogo ili kuja kuandika pumba hapa jamvini. Hapa tunaongelea wizi wa bilioni 200 za ESCROW hatuongelei mambo ya kuoana mpumbavu mkubwa wee. Jifunze kusoma na kuelewa kilichoandikwa badala ya kukurupuka na kuanza kuropoka pumba. Mxciuuuuuuuuuuuuu

JF senior member, Joining Date Febr 2007. umepanic, uliyemtukana alijenga hoja yake juu ya mabeberu (UK) ambao wewe uliwatumia kujenga hoja. Umeshindwa kutetea hoja yako umeamua kumattack. Hakuna anayetetea mafisadi humu ila uzushi kama wakina KAFULILA na MSALITI hatuwezi kubeba.
 
Porojo na wanasiasa kukosa hoja za ukweli tu, hakuna lolote kuhusu IPTL.

Bi kizee, afadhali umekuja....hebu taumbie UKWELI wa hili sakata au nawe umetumwa kutetea WEZI?
 
Siwezi kupanick hata siku moja, rudi shule ukajifunze kusoma na kuandika badala ya kutumiwa na mapanya na mafisadi ili uwapigie debe hapa jamvini kwa ujambazi wao. Kumbuka wakati ni ukuta ukiupiga utaumia mwenyewe, bado hujachelewa kujifunza kusoma na kuandika.

Umepanic Kamanda, baada ya kuataki hoja yangu unaniataki mimi. Ila sishangai ni kawaida ya wajinga.
 
Kafulila anafahamu kuwa iptl ndio kampuni pekee
inayookoa fedha za watanzania kwenye nishati kwasababu ya
kuwauzia umeme kwa bei nafuu kuliko kampuni anayoipigia
debe na iliyomtuma kuichafua iptl yaani symbioon ambayo
inaiuzia tanesco umeme unit moja kwa zaidi ya elfu moja
wakati iptl inaiuzia umeme tanesco chini ya shiling mia tano
kwa unit na imeanza mazungumzo kushusha umeme hadi sh 90
kwa unit,je haoni anatumika vibaya na kampuni yenye wivu
wa kibiashara kuchafua iptl ambayo ni mkombozi wa tanzania.

Bwana Muhongo, hebu jitetee vizuri, bado siajakupata!
 
Kafulila kashatoa ushahidi wake kwa PCCB na CAG, Yeah! hili sakata linaondoka na KAFULILA maana anakesi ya madai mahakamani.

Check ulivyo na akili,umepost bonge la point hakika wewe ni great thinker,makofii pwaaa pwaaa,haya kalale sasa
 
Siwezi kupanick hata siku moja, rudi shule ukajifunze kusoma na kuandika badala ya kutumiwa na mapanya na mafisadi ili uwapigie debe hapa jamvini kwa ujambazi wao. Kumbuka wakati ni ukuta ukiupiga utaumia mwenyewe, bado hujachelewa kujifunza kusoma na kuandika.

Asante Kamanda ntarudi shule, lakini hatuwezi kuacha kusema ukweli eti sababu ya mihemko yako unayoionesha. Umepanick kamanda , Hakuna wizi kwenye akaunti ya escrow.
 
Ndiyo matatizo ya nchi ikiwa mikononi mwa Majambazi, watakwapua kila wawezacho kukwapua kasha kufanya jitihada kubwa sana ili kupoteza ushahidi wa kuwapandisha kizimbani na wakati mwingine hata sharia za nchi zitapindishwa ili kuwakingia kifua. Kumbuka EPA, "Pesa zote zilizoibiwa zimerudishwa hivyo hakuna haja ya kuwapandisha kizimbani wahusika." Na kauli nyingine, "Wezi wa EPA ni mtajiri wakubwa sana nchini kama wakikamatwa basi nchi itawaka moto." Mxciuuuuuuuuuuu...Halafu wanajiita eti ni viongozi!!!!

Hili sakata, bila kumumunya maneno, kutikisa masikio wala kupepesa macho, lazima liende na mtu….haiwezekani hawa panya watafune fedha zote hizi za umma halafu wananchi tukae kimya! Mbivu na mabichi lazima zijulikane…Kafulila anao ushahidi mujarabu lakini WEZI hawataki kumpa nafasi kwa kuwa wanafahamu kwamba atawaumbua mchana kweupe. Hivi ni lini hawa panya wa CCM wataacha kutafuna fedha za watanzania?

View attachment 188972 View attachment 188974
 
Huujui ukweli wewe ungekuwa unaujua ukweli kamwe usingethubutu kusimama upande mmoja na mafisi na mapanya wanaoiangamiza Tanzania siku zote ungekuwa unasimama mstari wa mbele kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania wenzako badala ya hao majambazi wanaokwapua karibu kila wiki huku nchi ikikosa maendeleo ya kweli.

Asante Kamanda ntarudi shule, lakini hatuwezi kuacha kusema ukweli eti sababu ya mihemko yako unayoionesha. Umepanick kamanda , Hakuna wizi kwenye akaunti ya escrow.
 
Ni Sababu zipi zilizosababisha Kikwete asimuongozee CAG miezi mitatu kabla ya kustaafu ili amalizie ripoti hii? Je, huyo atayechukua nafasi hii CAG atateuliwa lini? Je, kama atateuliwa hivi karibuni atapewa maagizo na Kikwete kwamba kipaumbele chake cha kwanza kama CAG ni kukamilisha ripoti hiyo ya wizi wa shilingi bilioni 200 za ESCROW au ataambiwa ripoti hiyo haina umuhimu na hivyo kuendelea na "kazi nyingine" ambazo hazina kipaumbele kikubwa kama wizi huu wa pesa za ESCROW?

Mkuu tusitegemee mwendelezo wa hili jambo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom