Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

Kafulila awalipua mawaziri akaunti ya Escrow

Mnapata tabu nyie mnao taka kumwelewa!! Mimwezenu siku nyingi nilishagundua kuwa KAFULILA siyo mzima wa akili.

Kafulila ni mchumia tumbo tu then anataka kuwaaminisha watanzania uongo wake kwasababu ya fedha tu alizopewa na mafisadi wa nchi hii,kiukweli inaniwia vigumu sana kuona kiongozi kijana kama kafulila anakubali kurubuniwa kirahisi na kupokea fedha ili akaseme vitu vya uongo bungeni na kuwadanganya watanzania,na wasiwasi sana na huyu mtu anaweza ata kuuza nchi kwa tamaa ya fedha.
 
kafulila.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila akichangia mjadala bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

KWA UFUPI

  • Asema kashfa ya Fedha za Akaunti ya Escrow ni kubwa kuliko ya EPA, ataka iundwe tume ya Bunge, Pinda kutoa majibu leo

Dodoma. Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilichotwa katika Akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Katika tuhuma hizo, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.

Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.

Kafulila alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.

Mbunge huyo alisema fedha zilizoibwa katika Akaunti ya Escrow ni nyingi kuliko zile zilizoibwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT mwaka 2005.

“Pamoja na hilo, Watanzania wamekuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tanesco wakati ilipokuwa na mgogoro na IPTL walifika mahali wakafungua akaunti ya Escrow,” alisema.

Mbunge huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2004 na hadi jana, akaunti ile ilishafikia Dola za Marekani 122 milioni,” alisema Kafulila.

Alisema fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwapo kati ya IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.

Alitaka jambo hilo liingie kwenye rekodi kwa kuwa linahusu BoT na vigogo akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na pia Waziri wa Fedha.

Alisema wakati Tanesco ikidaiwa madeni zaidi ya Sh400 bilioni, viongozi hao wameidhinisha kugawanywa kwa fedha hizo kihuni jambo alilosema halivumiliki hata kidogo.

Kafulila alisema fedha hizo zilichotwa na Kampuni ya PAP aliyosema ya “Singasinga na ya kitapeli” ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu. Alisema fedha hizo hazikupaswa kuchukuliwa kwa

kuwa kulifanyika udanganyifu mkubwa kwamba PAP ilikuwa imenunua IPTL wakati jambo hilo si la kweli.
Alisema IPTL ilikuwa na makubaliano ya kufanya kazi kwa kampuni mbili ambazo ni VIP Engineering ya Tanzania iliyokuwa na hisa asilimia 30 na Mecmer ambayo ilikuwa na asilimia 70 ya hisa.

Hata hivyo, alidai kuwa anao ushahidi kuwa PAP ilikuwa imenunua hisa za VIP na hakukuwa na vielelezo vya kununua Mecmer kwa kuwa kampuni hiyo tayari ilishapoteza uhalali wake kwa kuwa ilikuwa chini ya muflisi nchini Malaysia.

Aliliambia Bunge kuwa wakati wa uchukuaji wa fedha hizo kutoka BoT, ilipaswa kulipiwa kodi lakini zilichukuliwa kinyemela bila hata ya kulipiwa kodi.

Alisema TRA iliiandikia Hazina na nakala kwa BoT kwamba wakati wa kulipa fedha hizo lazima kodi ikatwe, lakini cha ajabu hilo halikufanyika licha ya kukumbushwa.

“Kwa mfano, tulimwita Gavana katika kikao chetu cha Kamati ya Uchumi pale Bagamoyo na alikiri kuwa alibanwa na viongozi wa juu kiasi cha kushindwa kufurukuta, kwa hali kama hiyo Naibu Spika unategemea nini?” alihoji.

Kafulila alisema, Gavana katika kikao hicho alikiri kuwa, kulikuwa na presha (shinikizo) ambazo asingeweza kuzizuia na kuwa alikuwa amejitahidi kwa kiasi kikubwa hadi kufikia alipofika.

Alisema ISCID lilitoa hukumu ndogo Februari, mwaka huu kuwa Tanesco na IPTL wakae pamoja na kupitia hesabu zao namna watakavyogawanya fedha hizo na walipewa siku 60 ambazo mwisho wake ulikuwa jana.

Aliituhumu Tanesco kuwa katika makubaliano hayo ilikataa kukaa meza moja na kufanya hesabu za namna ya kulipana jambo alilosema linaonyesha ilidhamiria kufanya hivyo.

“Kwa sababu wanajua kuwa fedha ile ilishaliwa na wajanja wachache, Mheshimiwa Waziri Mkuu, hili kwa vyovyote halikubaliki na halivumiliki kwa sababu Dola122 milioni ni zaidi ya Sh200 bilioni ambazo ni nyingi kuliko za EPA, lazima litoke na mtu.”

Alisema hayuko tayari kuona fedha hizo zikitafunwa bila ya utaratibu na akashangazwa kuona Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), akishindwa kuchukua hatua. Akoleza moto jioni Katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu alimwita tena Kafulila kutoa ufafanuzi wa hoja yake aliyoitoa mchana, ambayo iliombewa mwongozo na Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina kwamba Gavana alishinikizwa kutoa fedha hizo.
Wakati wa mwongozo huo, Kafulila hakuwapo na ndiyo sababu ya Mwenyekiti kumpa nafasi ya kufuta kauli yake kuwa Gavana alishinikizwa. Hata hivyo, Kafulila alikazia akisema alishinikizwa kutoa fedha hizo.

“Gavana aliwahi kuniambia, mnanionea bure. Kulikuwa na presha kubwa sana kuhusu fedha hizi… ukweli ni kwamba IPTL inabadilishwa tu rangi na watendaji ni walewale.”

Baada ya Kafulila kuzungumza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kusema: “Tuhuma dhidi ya Gavana wa Benki Kuu zinatolewa kwa kuwa hawezi kuingia bungeni kujitetea.

“Lakini Gavana tulimuuliza na akakanusha kuwa aliwahi kuyatamka hayo maneno na kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni atakuja kufafanua jambo hili kesho (leo) katika hotuba yake,” alisema Lukuvi.

Hata hivyo, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisimama kuomba mwongozo akisema: “Kamati ya Bunge iundwe ili tuchunguze fedha hizi za Escrow zimekwenda wapi? Kafulila ana ushahidi wa kutosha, kwa nini hamtaki athibitishe?

“Vikao vyote vya kamati vinawekewa kwenye kumbukumbu rasmi (hansard) ili kujua kama Gavana alitoa maneno hayo ama hakutoa, iundwe kamati ijulikane mbivu na mbichi na wezi wa fedha za Escrow tunao humu ndani ya Bunge.”

Chanzo:
Mwananchi

Kafulila ni mchumia tumbo tu then anataka kuwaaminisha
watanzania uongo wake kwasababu ya fedha tu alizopewa na
mafisadi wa nchi hii,kiukweli inaniwia vigumu sana kuona
kiongozi kijana kama kafulila anakubali kurubuniwa kirahisi
na kupokea fedha ili akaseme vitu vya uongo bungeni na
kuwadanganya watanzania,na wasiwasi sana na huyu mtu
anaweza ata kuuza nchi kwa tamaa ya fedha.
 
Hizi ni dalili mbaya kuwa Kafulila anataka kuyakataa matokeo
ya uchunguzi kama yatakuwa hayajarinda interest zake!
Hata jana tumemkoti alivyoeleza wasiwasi wake kuwa ripoti
inaweza isijadiriwe bungeni, mbona yeye tu anaye
tapatapa?kunanini kafulila mbona ni wewe tu ndio umelivalia njuga
suala hili la IPTL/ESCROW?Je kunanii...kafulila wewe?
 
Kafulila azidi kukomaa na Escrow.

kafulila.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.PICHA|MAKTABA.

KWA UFUPI
“Ninasisitiza, Singasinga Sethi (Singh Sethi, Mkurugenzi wa Pan Africa Power Limited) aache kampeni za kupotosha umma wa Watanzania kwa nguvu ya fedha.

Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema atawasilisha bungeni hoja binafsi ya kutokuwa na imani na Serikali, iwapo ripoti za uchunguzi wa mabilioni ya fedha za Escrow zilizotochotwa kifisadi haitajadiliwa Bunge lijalo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kafulila (NCCR Mageuzi) alisema amechukua uamuzi huo kutokana na ubabaishaji wa makusudi kuiweka wazi ripoti hiyo. “Nasisitiza kwamba fedha za Escrow, Dola za Marekani 270 milioni, zimetolewa kifisadi na ndio sababu kwa muda sasa umekuwapo mkakati wa kuzuia ripoti za uchunguzi zisijadiliwe Bunge lijalo. Wito wangu kwa Serikali, iwapo ripoti hii haitaletwa, Bunge lijalo halitakalika. Nitapeleka hoja ya kutokuwa na imani na Serikali,” alisema.

Alisema ni wazi Kampuni ya Ufuaji Umeme ya IPTL na ya Pan African Power Solution (PAP), zimejipanga kuwapotosha Watanzania wasijadili masuala ya biashara ndani ya IPTL, wakati mauziano yao yana utata wenye masilahi ya Taifa kwa kuwa yanaambatana na kodi, hasa kitendo cha kuripoti kuwa asilimia 70 za hisa za IPTL ziliuzwa kwa Sh6 milioni, ikimaanisha ukwepaji mkubwa wa kodi.

“Ninasisitiza, Singasinga Sethi (Singh Sethi, Mkurugenzi wa Pan Africa Power Limited) aache kampeni za kupotosha umma wa Watanzania kwa nguvu ya fedha.

“Mkakati unaoendelea kuhakikisha ripoti haziji Bunge lijalo, usitishwe mara moja kwa sababu nchi inaumia, hakika sitakubali agenda niliyoanzisha ihujumiwe,” alisema.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa katika suala hilo lazima ‘vigogo’ waliohusika waondolewe. chanzo.Kafulila azidi kukomaa na Escrow - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Kafulila azidi kukomaa na Escrow.

kafulila.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.PICHA|MAKTABA.

KWA UFUPI
"Ninasisitiza, Singasinga Sethi (Singh Sethi, Mkurugenzi wa Pan Africa Power Limited) aache kampeni za kupotosha umma wa Watanzania kwa nguvu ya fedha.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kafulila (NCCR Mageuzi) alisema amechukua uamuzi huo kutokana na ubabaishaji wa makusudi kuiweka wazi ripoti hiyo. "Nasisitiza kwamba fedha za Escrow, Dola za Marekani 270 milioni, zimetolewa kifisadi na ndio sababu kwa muda sasa umekuwapo mkakati wa kuzuia ripoti za uchunguzi zisijadiliwe Bunge lijalo. Wito wangu kwa Serikali, iwapo ripoti hii haitaletwa, Bunge lijalo halitakalika. Nitapeleka hoja ya kutokuwa na imani na Serikali," alisema.

Alisema ni wazi Kampuni ya Ufuaji Umeme ya IPTL na ya Pan African Power Solution (PAP), zimejipanga kuwapotosha Watanzania wasijadili masuala ya biashara ndani ya IPTL, wakati mauziano yao yana utata wenye masilahi ya Taifa kwa kuwa yanaambatana na kodi, hasa kitendo cha kuripoti kuwa asilimia 70 za hisa za IPTL ziliuzwa kwa Sh6 milioni, ikimaanisha ukwepaji mkubwa wa kodi.

"Ninasisitiza, Singasinga Sethi (Singh Sethi, Mkurugenzi wa Pan Africa Power Limited) aache kampeni za kupotosha umma wa Watanzania kwa nguvu ya fedha.

"Mkakati unaoendelea kuhakikisha ripoti haziji Bunge lijalo, usitishwe mara moja kwa sababu nchi inaumia, hakika sitakubali agenda niliyoanzisha ihujumiwe," alisema.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa katika suala hilo lazima ‘vigogo' waliohusika waondolewe. chanzo.Kafulila azidi kukomaa na Escrow - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Umekula fedha ya MKONO, MENGI , ROSTAM NA STANDARD CHARTERED BANK-HONG KONG, ILI UPOTOSHE UMMA KWA MASLAHI YAO. TUNAJUA HUWEZI ACHA KUROPOKA, RIPOTI YA CAG NDIO ITAKAYO KUNYAMAZISHA.
HUU NDIO UKWELI NA UTABAKI KUWA HIVYO MILELE;

""""Mwaka 2006 serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini, shirika la IPTL na Benki Kuu ya Tanzania (wakala) kutokana na Mkataba wa kuzalisha na kuuza umeme kutoka IPTL kwenda TANESCO kulianzishwa akaunti ya ESCROW.MAtakwa ya makubaliano ya kuanzishwa na kutekelezwa kwa mradi wa kujenga, kuendesha na kuzalisha umeme wa kuuza kati ya kampuni binafsi ya IPTL na TANESCO ni kwa serikali kufungua letters of credit au kufungua akaunti ya ESCROW.
Akaunti hiyo siyo fedha za serikali bali ni fedha ambazo ziliwekwa kutokana na matakwa ya mkataba wa kuuza umeme kwa TANESCO kutoka kampuni binafsi. Katika mkataba wa kufungua akaunti ya ESCROW kuna kifungu kinasomeka, "required amount means the amount in Tshs. That the government of Tanzania shall deposit from time to time in the ESCROW account which equals not less than two months estimated tariff payments under the PPA, provided that such amount shall be adjusted annually by IPTL and TANESCO pursuant in the PPA in the article 11 hereof, and government of Tanzania will be entitled will be entitled to review independently, the calculation of the required amount pursuant to this agreement".
Tafsiri yake kwa Kiswahili ni kwamba "kiasi kinachopaswa kuingizwa na serikali katika akaunti ya ESCROW ni kile ambacho kinalingana na madai ya malipo sawa na miezi miwili ya gharama ya kuuza umeme ambazo IPTL inadai TANESCO, IPTL na TANESCO watafanya marejeo kuhusiana na kiasi cha gharama za umeme kila mwaka. Hayo ni kwa mujibu wa makubaliano ya kuuza na kununua umeme kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa mauzo ya umeme (Power Purchasing Agreement) au kwa kifupi PPA na kama ilivyobainishwa kwenye kifungu cha 11. Serikali itakuwa huru kufanya tathmimini yake kuhusu gharama halisi za uzalishaji na uuzaji wa umeme kwa mujibu wa mkataba wa PPA.
Wakati akaunti ya ESCROW inafunguliwa serikali na IPTL walikuwa katika mahakama ya usuluhishi ya ICSD ambapo suala la gharama za capacity charge lilikuwa linagombewa. IPTL kwa kula njama ilikuwa imedai kwamba gharama za kununua na kuweka mitambo ya kufua umeme na kujenga miundombinu zinafikia dola za kimarekani 150. Lakini kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kutoka Uholanzi na Finland ambapo IPTL ilinunua mitambo ya kufua umeme, serikali ilikuja kugundua kwamba kiasi halisi ambacho kilitumika ni dola za kimarekani milioni 80. Hivyo serikali ya Tanzania ilikataa madai ya kulipa dola za kimarekani milioni 3.6 kwa ajili ya capacity charge.""
Katika Mahakama ya Usuluhishi fedha ambazo zilikubaliwa ni dola za Kimarekani millioni 120 na hivyo gharama za capacity charge kuteremshwa kufikia dola za Kimarekani milioni 2.6. Hivyo mgogoro kati ya serikali na IPTL ukawa umekwisha."""

SOURCE:
http://www.taifaimara.co.tz/?p=410#comment-7
 
Hizi ni dalili mbaya kuwa Kafulila anataka kuyakataa matokeo
ya uchunguzi kama yatakuwa hayajarinda interest zake!
Hata jana tumemkoti alivyoeleza wasiwasi wake kuwa ripoti
inaweza isijadiriwe bungeni, mbona yeye tu anaye
tapatapa?kunanini kafulila mbona ni wewe tu ndio umelivalia njuga
suala hili la IPTL/ESCROW?Je kunanii...kafulila wewe?

Kuna wanaosema kwamba fedha zilizowekwa kwenye akaunti
ya ESCROW ni za serikali na wengine wanakataa na kusema
kwamba fedha hizo kamwe si za serikali bali ni fedha za
wanahisa wa IPTL ambao ni kampuni ya Mechmar ya Malaysia
na VIP Engineering and Marketing ya Tanzania. Hoja za kila upande zimetawala magazetini na malumbano kati na baina ya wanasheria,wabunge na wanasiasa wengine ambao kwa namna moja au nyingine wanarukia mambo bila kujaribu kutafuta undani
wake ili waelewe na waseme kilicho sahihi kuliko kuongea vitu vya uongo na vyakubuni tu.
 
Kafulila azidi kukomaa na Escrow.

kafulila.jpg

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.PICHA|MAKTABA.

KWA UFUPI
“Ninasisitiza, Singasinga Sethi (Singh Sethi, Mkurugenzi wa Pan Africa Power Limited) aache kampeni za kupotosha umma wa Watanzania kwa nguvu ya fedha.

Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema atawasilisha bungeni hoja binafsi ya kutokuwa na imani na Serikali, iwapo ripoti za uchunguzi wa mabilioni ya fedha za Escrow zilizotochotwa kifisadi haitajadiliwa Bunge lijalo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kafulila (NCCR Mageuzi) alisema amechukua uamuzi huo kutokana na ubabaishaji wa makusudi kuiweka wazi ripoti hiyo. “Nasisitiza kwamba fedha za Escrow, Dola za Marekani 270 milioni, zimetolewa kifisadi na ndio sababu kwa muda sasa umekuwapo mkakati wa kuzuia ripoti za uchunguzi zisijadiliwe Bunge lijalo. Wito wangu kwa Serikali, iwapo ripoti hii haitaletwa, Bunge lijalo halitakalika. Nitapeleka hoja ya kutokuwa na imani na Serikali,” alisema.

Alisema ni wazi Kampuni ya Ufuaji Umeme ya IPTL na ya Pan African Power Solution (PAP), zimejipanga kuwapotosha Watanzania wasijadili masuala ya biashara ndani ya IPTL, wakati mauziano yao yana utata wenye masilahi ya Taifa kwa kuwa yanaambatana na kodi, hasa kitendo cha kuripoti kuwa asilimia 70 za hisa za IPTL ziliuzwa kwa Sh6 milioni, ikimaanisha ukwepaji mkubwa wa kodi.

“Ninasisitiza, Singasinga Sethi (Singh Sethi, Mkurugenzi wa Pan Africa Power Limited) aache kampeni za kupotosha umma wa Watanzania kwa nguvu ya fedha.

“Mkakati unaoendelea kuhakikisha ripoti haziji Bunge lijalo, usitishwe mara moja kwa sababu nchi inaumia, hakika sitakubali agenda niliyoanzisha ihujumiwe,” alisema.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa katika suala hilo lazima ‘vigogo’ waliohusika waondolewe. chanzo.Kafulila azidi kukomaa na Escrow - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Kuna wanaosema kwamba fedha zilizowekwa kwenye akaunti
ya ESCROW ni za serikali na wengine wanakataa na kusema
kwamba fedha hizo kamwe si za serikali bali ni fedha za
wanahisa wa IPTL ambao ni kampuni ya Mechmar ya Malaysia
na VIP Engineering and Marketing ya Tanzania. Hoja za kila
upande zimetawala magazetini na malumbano kati na baina ya
wanasheria,wabunge na wanasiasa wengine ambao kwa
namna moja au nyingine wanarukia mambo bila kujaribu
kutafuta undani wake ili waelewe na waseme kilicho sahihi kuliko kuongea vitu vya uongo na vyakubuni tu.
 
Kuna wanaosema kwamba fedha zilizowekwa kwenye akaunti
ya ESCROW ni za serikali na wengine wanakataa na kusema
kwamba fedha hizo kamwe si za serikali bali ni fedha za
wanahisa wa IPTL ambao ni kampuni ya Mechmar ya Malaysia
na VIP Engineering and Marketing ya Tanzania. Hoja za kila upande zimetawala magazetini na malumbano kati na baina ya wanasheria,wabunge na wanasiasa wengine ambao kwa namna moja au nyingine wanarukia mambo bila kujaribu kutafuta undani
wake ili waelewe na waseme kilicho sahihi kuliko kuongea vitu vya uongo na vyakubuni tu.

Toka lini mtu anayepewa uwakala wa kusimamia fedha za watu wanaovutana ili azisimamie akawa mmiliki wa hizo fedha?
 
Toka lini mtu anayepewa uwakala wa kusimamia fedha za watu wanaovutana ili azisimamie akawa mmiliki wa hizo fedha?

tumefika mahali watanzania tumekuwa kama wale watu
wanaogombania bakuli za supu kwa ng'ombe ambaye
hajachinjwa na pengine hajatolewa hata zizini,fikiri kama
ng'ombe atakata kamba au kutoroka zizini itakuaje?
Watanzania inatubidi tuwe makini sana na viongozi wetu
hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu 2015,kuna
viongozi watazuka tu na migogoro hapa na pale ili watafute
jina lake kusikika kwa jamii(kick) kwa vitu vya kweli au
uongo ilimradi tu asikike kwenye vyombo vya habari na
kwenye mitandao ya kijamii.
 
Kafulila njaa inamsumbua ni ujanja ujanja tu hamna lolote anatumiwa na mafisadi ili kuuangusha uongozi wa wizara ya Nishati na madini hilo linajulikana wazi baada ya kupatikana uongozi makini usioongeka wala kutetereka mafisadi wamekosa nafasi ya kula wanatumia mbinu kuhujumu uongozi ili waweke watu wao watengeneze mianya ya kula kaeni mkijua hamtafanikiwa watanzania tunajua janja yenu. anazungumza sana kuhusu hiyo ripoti ya CAG inaonekana anayo mkononi aweke hadharani tuijadili wote kwa pamoja vinginevyo anatuchanganya tu kila kitu kina utaratibu wake tusubiri ripoti itakapotoka yeye kabla ripoti haijatoka ameshaanza kunyooshea watu kidole amejuaje kilichomo kwenye ripoti ni mtu wa kulopoka wala si mvumilivu kwa tabia hii aliyoionyesha Kafulila ndiyo maana chama fulani kilimfukuza ni mbunge masilahi yeye na rafiki yake Nyepesi hawatofautiani kimatendo dili mbele utu nyuma hawa watu hawatufahi hata kidogo tuwe nao makini.Fuatilia sababu za Kafulila na Nyepesi kufukuzwa kwenye vyama vyao utagundua tabia na mienendo ya hawa watu inavyofanana ni viongozi masilahi hawatufahi wameweka ubibafsi mbele utaifa nyuma tena Kafulila mwanzoni alifukuzwa chama fulani akaamia chama alichopo majuzi juzi hicho chama nacho kikamfukuza akaomba sana msamaha akipiga magoti na kulia kwa busara akasamehewa vinginevyo ilikula kwake na huyo mwenzake Nyepesi baada ya kufukuzwa akakimbilia mahakamani ni mbunge wa mahakama vinginevyo nae Kwisha habari yake jamani hawa watu hawafahi tusiwasikilize tuwapuuze ni viongozi masilahi wanatumiwa na mafisadi.
 
Habari wadau, nimeona niileta taarifa hii kwa wadau wenzangu humu. Nilikuwa katika story za kawaida na mtu wa karibu wa Zitto na Kafulila, akanidokeza kuwa Zitto na Kafulila ni watu marafiki sana, ambapo wanashirikiana kwa karibu sana katika kazi za siasa.

Aliniambia issue ya IPTL ni ya Zitto na si Kafulila, Zitto alipata kujua uozo huo wa IPTL akaamua kumpasia Kafulila aanzishe hoja hiyo bungeni akaahidi kumpa kila data inayohitajika.

Aliamua kumpa Kafulila baada ya kuona akiibua yeye atakosa ushirikiano pande zote upinzani na utawala. Mtu huyo aliniuliza huoni mafisadi hawa wanapomshambulia Kafulila lazima zitto ajitokeze?. Hii ndio siri ya wawili hawa.
 
cha kujiuliza kama ni kweli zitto akihamia ACT, kafulila atamfuata?
 
Chamsingi ni hoja yenyewe sio aliyeianzisha! watu wanataka kuijua mbivu na mbichi ili kufahamu TUMBILI ni nani kati ya muraa wetu AG Werema na mh. David Kafulila aliyeibua uozo huo bungeni!!
 
Chamsingi ni hoja yenyewe sio aliyeianzisha! watu wanataka kuijua mbivu na mbichi ili kufahamu TUMBILI ni nani kati ya muraa wetu AG Werema na mh. David Kafulila aliyeibua uozo huo bungeni!!

nikweli kabisa mkuu
 
Duh! Haya majamaa yaliyohusika kuchota Escrow yanma miroho migumu kwelikweli.yaani hadi hatua hii mtu kama Werema, Maswi, Muhongo, na Mboma (M'kiti wa Bodi ya Tanesco) wajajiuzulu? Au pengine ni dharau tu wanawafanyia kwa Watanzania kutokana na kulindwa na utawala dhaifu wa JK?
 
Umeshawasikia fisadi akistaafu wewe.
 
Back
Top Bottom