Sijui Mbunge Zitto Kabwe alicomment nini wakati anapost hizi files kwenye facebook account yake, lakini kama dhamira yake ilikuwa kutaka kutuendelezea ule mchezo mchafu basi kwenye hili mimi binafsi na mpuuza nakumwona kama kibaraka wa mabeberu, sababu ya kusema hivi ni moja kwakumbukumbu inaonyesha pia ushiriki wa ZITTO kwenye kuwapotosha wananchi huku akitumia karata yake ya imani ambayo wananchi wanayo juu yake.
Hili sakata la IPTL kabla kina ZITTO na KAFULILA kulidakia,ilikuwa nikampeni ya mabeberu kuilazimisha serikali kuwapa dili ya kuuza umeme kupitia kampuni yao ya SONGAS. Hawakulidhishwa na serikali kutoa dili kwa nchi ya malaysia, mwendelezo wa hili sakata ulipamba moto baada ya watu wenye interest tofauti kudakia na kuanza kuishambulia serikali kuwa kuna ufisadi kwenye mradi wa IPTL,lakini ikumbukwe kuwa hivi nilini mabeberu walifanya kitu kwamaslahi ya nchi maskini na ndio maana Tanzania kwa mara ya kwanza tulipotaka kampuni binafsi ya kwaajiri ya kuzalisha umeme suruhisho letu kama nchi lilikuwa Malaysia kupitia South-south Commision.
Mabeberu kupitia BRIAN COOKSEY walianza kutuandama kwa lugha chafu sababu tu IPTL imeiside line SONGAS:
View attachment 189515
Malalamiko yanayotengenezwa na BRIAN COOKSEY yanabase kwenye kutaka kuimbua serikali kuwahaikufanya uamuzi mzuri ilipokubari kuipadili IPTL. Lakini je dili ya SONGAS ingekuwa na tofauti kweli naingelinda maslahi ya wazalendo kweli?? nimataifa mangapi ya kibeperi yamewekeza kwenye sekta kubwakubwa lakini bado wazalendo tunalia na mikataba yao??
View attachment 189516
Lakini tunaona sasa kwamba pamoja na ubungo gas turbines kufanya kazi bado tunawahitaji IPTL,na BRIAN COOKSEY yupo kimya kabisa toka atoe chapisho lake, hii yote nisababu anajua mabeberu wamepata walichokuwa wanahitaji SONGAS kuwa operational.
Lakini IPTL waliliona hizi hila za BRIAN COOKSEY:
In a long letter to the African (1 June 1998) titled ‘Brian's phobia against South-South Commission', I am dubbed a racist with a ‘pathological hatred of South-South cooperation', with ‘derogatory tendencies towards African governments, leaders and its people.' In a letter to Minister of Planning, Nassoro Malocho, IPTL copied an article that appeared in East African Alternatives, and accuse me of having vested interests in Songas. I am referred to as a ‘dangerous underground advisor,' ‘an academic and business crook,' with ‘prejudices against African and Asian leaders'.
Kilichofuata wote tunajua, waandishi waudaku wakina MIHANGWA wakatafsiri maandishi ya udaku ya BRIAN nakuyasambaza. Nasasa tunamuona ZITTO na KAFULILA wakiyabeba maneno yaleyale na kuyasambaza kwa umma, mfano ZITTO anarudiarudia sana kusema "Wapinzani, vyombo vya habari na civil society vimelikalia kimya sakata hili" nikitu kilekile alichokindika BRIAN kwenye udaku wake:
""
View attachment 189517
Watanzania wenzangu hapa tunachokiona ni mchuano mkali wa kibiashara ambao ndani yake mafisadi wakubwa wa taifa hili wamenunua kesi aliyoiacha BRIAN kibaraka wa mabeberu, na sasa ndugu zetu wenyewe wakina MKONO, MENGI na ROSTAM wanatugawanya kwa maslahi yao wakimtumia mbunge wa KIGOMA KUSINI, DAVID KAFULILA.
Upotoshaji unaofanywa na KAFULILA niwawazi kabisa, niwamakusudi kwa maslahi yake binafsi na ndio maana Katibu Mkuu wa NISHATI ndugu MASWI alisema tena hadharani kuwa KAFULILA na ZITTO wanatumika na wamepewa fedha na MKONO. Sababu nyingine za kutengeneza skendo ya IPTL;
(i) Nikukweli uliowazi hawa wabunge huu nimchezo wao wa siku nyingi kuanda zengwe ambalo mwisho wasiku wanafaidika nalo kwa kupozwa nawahusika, hii nimichezo inachezwa nakamati nyingi za bunge.
(ii) Masakata makubwa kama haya husaidia kuwapa kick wanasiasa tunakumbuka sakata la EPA na RICHMOND. ZITTO na mabilioni ya uswis
Watanzania tusikubali kuwa madaraja yawatu binafsi kujipatia umaarufu wakisiasa na kujiongezea ukwasi walionao.
View attachment 189518