Kafulila: Hata Ulaya ilijengwa kwa Mikopo toka Marekani Marshall Plan si dhambi kukopa ili kujenga miradi ya maendeleo kama SGR au JNHP

Nadhani hilo la Makampuni yao limekatiliwa kwa Sasa hata wazawa wanaruhusiwa
 
Mwanafunzi aliyesoma History (II) hawezi kulinganisha Marshal Plan na mikopo tunayoingia leo.
Marshal Plan walikuwa very strategic
 
Ndio maana pesa ya mkopo wa IMF au WB huwezi kuichezea kwa sababu hiyo miradi inasimamiwa na wao
 
Kumbe mmnajua aise
 
Ndio maana pesa ya mkopo wa IMF au WB huwezi kuichezea kwa sababu hiyo miradi inasimamiwa na wao
Miradi yake si ya kuendeleza nchi. Huwezi kuta wamekukopesha ujenge kiwanda cha chuma au irrigation scheme. Utasikia kukuza demokrasia na blah blah nyingine zinazokufunga na madeni bila kufanyia kitu cha maana.
 
Vijana machawa ni kutetea TU bila reasoning yoyote...nadhani...nafikiri....nenda kasome mwenyewe, wakibamwa maswali ya msingi vinajikesha na emoj zaidi ya tatu ujue vimechemka kujibu hoja za msingi.mnatetea vitu hamna uhakika navyo kisa Nini?😳
 
Hebu tiriirika tukusikie mwana historia
Mpango wa Marshall ulikuwa ni mpango wa Marekani wa kuijenga upya Ulaya baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Ilitangazwa mnamo 1947 na kutekelezwa hadi mwaka wa 1951, na lengo lake lilikuwa kuimarisha uchumi, kuzuia kuenea kwa ushawishi wa Kikomunisti, na kukuza amani na ushirikiano kati ya mataifa ya Ulaya. Mpango huu ulihusisha misaada ya kiuchumi na kiufundi kwa nchi zilizoathiriwa zaidi na vita hivyo.

Upekee wa Mpango wa Marshall ulikuwa katika mbinu yake ya kipekee ya kutoa misaada kwa nchi za Ulaya zilizohitaji ujenzi upya baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Badala ya kutoa misaada kwa nchi hizo kwa njia ya mikopo, Marekani iliamua kutoa misaada hii kwa njia ya misaada ya moja kwa moja, ambayo ilikuwa na masharti maalum. Hii ilisaidia kuhakikisha kwamba misaada hiyo haikuwa na mzigo wa deni kwa nchi husika na badala yake iliongeza uwezo wao wa kujenga upya uchumi wao na kuimarisha utulivu katika eneo hilo. Hii ilikuwa tofauti na mbinu nyingine za misaada ambazo zilijumuisha mikopo ambayo ilikuwa na gharama kubwa za kurejesha na ilikuwa na hatari ya kuongeza mzigo wa deni.
 
Mwaka 2005 kulikuwa na concert ( Live 8) London ya kushinikiza nchi tajiri kusamehe madeni ya nchi maskini kama sisi kwa sababu yalituelemea. Tukasamehewa. Tumesahau yote haya. Sasa hivi tunakopa katika mabenki ya kibiashara ili kununua ndege ambazo zinatutoa kamasi kuziendesha. Wakati huo huo tunasaidiwa kujenga vyoo.

Halafu huyu jamaa anataka tuwasifie!

Amandla...
 
Marshall plan haukuwa mkopo wa kuendesha serikali za ulaya na kulipana posho.
 
Marshall Plan ilitiwa Saini mwaka 1948 na ilikuwa ni mikopo sio grant,

Sasa kama Ulaya imejengwa kwa Mikopo why not Tanzania?
 
Marshall Plan ilitiwa Saini mwaka 1948 na ilikuwa ni mikopo sio grant,

Sasa kama Ulaya imejengwa kwa Mikopo why not Tanzania?
Motive behind Marshal Plan ni tofauti na tunachokifanya, hivi vitu havilingani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…