Kafulila: Kama kuna mtu au kampuni wameona kuna mradi serikali inauendesha kwa hasara na wana mbinu za kuifanya serikali na wao kupata faida waje

Ujinga upi kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha
 
Nataka kuongoza TRA niwaonesha kwa dakika tu
 
Ukimsoma 'between lines', hilo ni tangazo la 'kugawa miradi' ya serikali. Mambo yanafanywa very technical
Hayo ni maandalizi, ukisikia Mwrndokadi, SGR, JNHPP, wamepewa akina nani wa bara lile usishtuke.
'b
 
Ukimsoma 'between lines', hilo ni tangazo la 'kugawa miradi' ya serikali. Mambo yanafanywa very technical
Hayo ni maandalizi, ukisikia Mwrndokadi, SGR, JNHPP, wamepewa akina nani wa bara lile usishtuke.

'b
Tunagawanaje miradi ya Serikali?
 
mawazo haya sio mapya yalikuwepo wakati wa utawala wa mwinyi na mkapa tukaua mashirika yetu yote zaidi ya mianne, falsafa hizi zilianzishwa wakati wa tume ya Poul Bomani ya kurekebisha uchumi, yakatekelezwa na waziri wa fedha wa wakati ule Cleopas Msuya, wakati mwl anasatafu mashirika manne yaliingia mikataba hii ikiwemo TBL TCC NBC General tyre, utawala uliofata ukaja na mawazo ya kafulila tukavurunda hujapata ona, sasa huyu mtoto wa juzi kasoma kabrasha moja ofisini kwake, au kapiga story sijui na mstaafu gani anatuletea as if ni mawazo mapya kabisa.

hebu atuambie haya mawazo yalistafanyika wapi na yakaleta mafanikio maana kwetu wakati wa mwinyi mkapa yalidondokea ugoko
 
Kitu nafahamu hii Sheria ya UBIA imeanzishwa rasmi 2022 baada ya kufanyiwa marekebisho makubwa,
Hayo yote unayoyataja yamefanyika kwa Sheria ipi?
 
Kitu nafahamu hii Sheria ya UBIA imeanzishwa rasmi 2022 baada ya kufanyiwa marekebisho makubwa,
Hayo yote unayoyataja yamefanyika kwa Sheria ipi?
umesema imefanyiwa marekebisho yaani ilikuwepo, hayo yalifanyika chini ya tume ya ubinafsishaji mashirika ya umma
 

Naiomba Tanesco fasta ๐Ÿคฃ ๐Ÿคฃ ๐Ÿคฃ ๐Ÿคฃ ๐Ÿคฃ
 
Tanesco sio mradi wa hasara
Tanesco hata kama siyo hasara lakini tanesco ni janga sana kwa taifa, haiwezekani wameshindwa kusambaza umeme nchi nzima kisa tu hawana nguzo na ukienda kwenye vituo vyao nguzo ziko chini zimerundikwa na kutafunwa na mchwa. Lakini pale Tanesco kuna magenge ya wezi ya kutisha. Tanesco bora ibinafsishwe maana watanzania wameshindwa kuendesha shirirka hilo. Tanesco haina tofauti na jeshi la polisi kwa kupokea hongo.
 
Umeandika comment mpaka nimebubujikwa na machozi.
 
Sometimes uwe unaangalia pia what will happens next, sio kusema tu tubinafsishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ