Kafulila: Kama kuna mtu au kampuni wameona kuna mradi serikali inauendesha kwa hasara na wana mbinu za kuifanya serikali na wao kupata faida waje

Hayo mambo anayoengelea Kafulila ili mtu kuomba kazi lazima apate financial statement.

Kwa kifupi anaropoka tu, investors hawaamki tu na kutaka venture bila ya kuelewa hesabu zake kwanza.

Financial statement sio number tu unazoona, kwa mwenye uelewa wa kuisoma inampa picha nzima ya biashara na uwezo wa management given the market size and competition.

Sasa kusema watu waandike proposals za kuchukua biashara kama hazina faida wakati hawajaona hesabu za biashara (ni kielelezo cha kiwango cha ujinga wa watu wenye nafasi serikalini).

Ujinga mtupu
Ujinga upi kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha
 
Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP-Centred) Bw. David Kafulila ametoa wito kwa sekta na watu binafsi wenye utafiti kwenye miradi yoyote ya Serikali kwenye ngazi yoyote ya kiserikali na wamebaini serikali inapoteza mapato na wao wako tayari kuisaidia Serikali kuepuka hasara na kupata faida kwaajili yao na kwa Serikali yao wanakaribishwa kwa majadiliano na PPP.

Kafulila ameyasema hayo katika kituo cha runinga cha Clouds Media wakati akifafanua maana halisi ya UBIA, WABIA na aina zake.

Msikilize mpaka mwisho.
Nataka kuongoza TRA niwaonesha kwa dakika tu
 
IMG-20240822-WA0052.jpg
 
Ukimsoma 'between lines', hilo ni tangazo la 'kugawa miradi' ya serikali. Mambo yanafanywa very technical
Hayo ni maandalizi, ukisikia Mwrndokadi, SGR, JNHPP, wamepewa akina nani wa bara lile usishtuke.
Tumbili ovyo kabisa.
Yaani mradi wa serikali, serikali yenyewe haioni kama unaendeshwa kwa hasara, mimi mtu binafsi niione hiyo hasara halafu nikaishawishi serikali hiyo hiyo isiyoona kuna hasara kwenye hiyo miradi inipe mimi niendeshe kwa faida! Hiyo ni akili au matope?
'b
 
Ukimsoma 'between lines', hilo ni tangazo la 'kugawa miradi' ya serikali. Mambo yanafanywa very technical
Hayo ni maandalizi, ukisikia Mwrndokadi, SGR, JNHPP, wamepewa akina nani wa bara lile usishtuke.

'b
Tunagawanaje miradi ya Serikali?
 
mawazo haya sio mapya yalikuwepo wakati wa utawala wa mwinyi na mkapa tukaua mashirika yetu yote zaidi ya mianne, falsafa hizi zilianzishwa wakati wa tume ya Poul Bomani ya kurekebisha uchumi, yakatekelezwa na waziri wa fedha wa wakati ule Cleopas Msuya, wakati mwl anasatafu mashirika manne yaliingia mikataba hii ikiwemo TBL TCC NBC General tyre, utawala uliofata ukaja na mawazo ya kafulila tukavurunda hujapata ona, sasa huyu mtoto wa juzi kasoma kabrasha moja ofisini kwake, au kapiga story sijui na mstaafu gani anatuletea as if ni mawazo mapya kabisa.

hebu atuambie haya mawazo yalistafanyika wapi na yakaleta mafanikio maana kwetu wakati wa mwinyi mkapa yalidondokea ugoko
 
Kitu nafahamu hii Sheria ya UBIA imeanzishwa rasmi 2022 baada ya kufanyiwa marekebisho makubwa,
Hayo yote unayoyataja yamefanyika kwa Sheria ipi?
 
umesema imefanyiwa marekebisho yaani ilikuwepo, hayo yalifanyika chini ya tume ya ubinafsishaji mashirika ya umma
 
Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP-Centred) Bw. David Kafulila ametoa wito kwa sekta na watu binafsi wenye utafiti kwenye miradi yoyote ya Serikali kwenye ngazi yoyote ya kiserikali na wamebaini serikali inapoteza mapato na wao wako tayari kuisaidia Serikali kuepuka hasara na kupata faida kwaajili yao na kwa Serikali yao wanakaribishwa kwa majadiliano na PPP.

Kafulila ameyasema hayo katika kituo cha runinga cha Clouds Media wakati akifafanua maana halisi ya UBIA, WABIA na aina zake.

Msikilize mpaka mwisho.

Naiomba Tanesco fasta 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Tanesco sio mradi wa hasara
Tanesco hata kama siyo hasara lakini tanesco ni janga sana kwa taifa, haiwezekani wameshindwa kusambaza umeme nchi nzima kisa tu hawana nguzo na ukienda kwenye vituo vyao nguzo ziko chini zimerundikwa na kutafunwa na mchwa. Lakini pale Tanesco kuna magenge ya wezi ya kutisha. Tanesco bora ibinafsishwe maana watanzania wameshindwa kuendesha shirirka hilo. Tanesco haina tofauti na jeshi la polisi kwa kupokea hongo.
 
Huyu Mheshimiwa ni hazina kubwa sana tena sana kwa Taifa letu ambaye kama Taifa tunapaswa kumtumia vizuri.Ni akili kubwa , ni mtu mwenye maono na uwezo mkubwa sana wa kiuongozi.anaelezea jambo na kulifafanua vizuri ambapo hata mtu mwenye elimu ndogo anakuwa na uwezo wa kumuelewa vizuri kabisa na kwa urahisi .
Umeandika comment mpaka nimebubujikwa na machozi.
 
Tanesco hata kama siyo hasara lakini tanesco ni janga sana kwa taifa, haiwezekani wameshindwa kusambaza umeme nchi nzima kisa tu hawana nguzo na ukienda kwenye vituo vyao nguzo ziko chini zimerundikwa na kutafunwa na mchwa. Lakini pale Tanesco kuna magenge ya wezi ya kutisha. Tanesco bora ibinafsishwe maana watanzania wameshindwa kuendesha shirirka hilo. Tanesco haina tofauti na jeshi la polisi kwa kupokea hongo.
Sometimes uwe unaangalia pia what will happens next, sio kusema tu tubinafsishe
 
Back
Top Bottom