Kafulila: Milango iko wazi kwa mtu au kikundi kununua vichwa na mabehewa ya SGR kisha kuyaendesha kwa miundombinu ya serikali kwa sharti la ubia

Wahenga wanasema "Kuchamba kwingi mwishowe utatoka na kinyesi".

Hebu tuipe muda hii SGR iwe stable kwanza tuache huku kuchambachamba, angalau tufanye 5yrs with close competent supervision
Ni wazi zuri pia
 
Ni TUMBILI, hulka yake kuruka ruka Toka tawi hili mpaka lile
 
Sema wangeanza na UDA maana Serikali kuendesha hii miradi ni changamoto sana kwa sababu watu hatuna Uzalendo wa Mwalimu Nyerere.
 
DART mchakato unaendelea kama walivyokwambia,SGR ndio milango imefunguliwa hapo tatizo ni wapi?
Unafungua milango kwa PPP ya SGR ya nini, wakati hata hiyo ya DART hujaanza..? una uhakika gani PPP ya DART itafanikiwa? na hivyo hata PPP ya SGR pia itafanikiwa..
 

tuache PPP wakati dunia nzima nchi zinazojenga uchumi wa kisasa wanatumia PPP. Kenya, Botswana, Vietnam, Malaysia, India, China wacha Ulaya na America.TUJIPE MUDA MKUU
 
Kwani huwezi kufungua milango yote?
Mimi nadhani kama Taifa tunahitaji kusimama pamoja kwenye hili
Unafungua milango kwa PPP ya SGR ya nini, wakati hata hiyo ya DART hujaanza..? una uhakika gani PPP ya DART itafanikiwa? na hivyo hata PPP ya SGR pia itafanikiwa..
 
Kwani huwezi kufungua milango yote?
Mimi nadhani kama Taifa tunahitaji kusimama pamoja kwenye hili
Nadhani nimeeleza awali umuhimu wa kufanya majaribio ili kupata uhakika wa matokeo unayotaka..si sahihi kufanya mambo bila kujali matokeo yanaweza kuwa si yale unatarajia..ķwani kuna haja gani kuharakisha kufanya miradi na PPP? Km tumefanya miradi/uwekezaji hapo awali bila PPP haraka ya nini sasa hivi..?
 
Majaribio yalishafanywa Kenya, Botswana, Vietnam, Malaysia, India, China wacha Ulaya na America.
 
Mkuu kuna kitu kimenishtua hapo, unasema bakhressa ni mwekezaji mkubwa Uganda railway? Kivipi?

Pia unasema mo kaomba kuleta treni ya utalii? Treni ya utalii ni nini? Ni ya abiria au ya utalii kivipi?
 
Majaribio yalishafanywa Kenya, Botswana, Vietnam, Malaysia, India, China wacha Ulaya na America.
Sasa mbona unataka kuonyesha km vile hujui unalotetea..ni sawa kulinganisha Tanzania na Botswana? Kitu gani kinakupa uhakika kwamba jambo lililofanywa Botswana likafanikiwa likifanywa Tanzania litafanikiwa pia, au jambo lilifanywa Tanzania likafeli Likifanywa Botswana litafeli pia..mfano Botswana na Tanzania kunapatikana Almasi, lakini mbona Pato na biashara ya Almasi Botswana ni ya tija zaidi kuliko Tanzania..hivyo si sahihi kudhani majaribio ya PPP Botswana yatatoa matokeo yale yale kwa Tanzania, mazingira ya kufanya PPP yanayofautiana kwa kila nchi..watu(idadi), sera, uchumi, tabia na utamaduni, nk nk..matokeo ya majaribio ya PPP Kenya si ya Tanzania! Kuna nini Kenya ambacho Tanzania hakipo? Mbona uchumi wao ni bora kuliko wa Tanzania..?
 
Mkuu kuna kitu kimenishtua hapo, unasema bakhressa ni mwekezaji mkubwa Uganda railway? Kivipi?

Pia unasema mo kaomba kuleta treni ya utalii? Treni ya utalii ni nini? Ni ya abiria au ya utalii kivipi?
Bahkhesa kawekeza treni uganda Kwa ajili ya mizigo yake, treni luxury yà kitalii inayosimama kila eneo na kushusha watalii watalii maeneo ya vivutio vya utalii iwasubiri hata masaa manne kuendelea na safari au kigeuza Mo Dewji ndio kaomba kuendesha hiyo treni ya kitalii

Watalii waweza ishia hata ubungo tu au pugu au mlimba au morogoro na wakageuza muda wao wanataka wenyewe kuanzia muda wa kuondoka au kurudi sio Kwa ratiba ya TRC tu kuona mandhari au wao wakijipangia wenyewe sisi tunataka kuondoka muda huu hatutaki ratiba ya TRC
Ni sawa tu na kukodi gari ya tours au taxi ikupeleke utakako Kwa muda wako
 
Kila jambo likishafanyiwa majaribio maeneo mengi kinatengenezwa Standard Unit, PPP sio jambo geni hata hapa Tanzania kwa mfano SONGAS ni mradi wa PPP sijui kama unafahamu hili
 
Kama Mo kaomba nadhani hakuna haja ya kumnyima
 
Kwaniní tusiwape JWTZ waendeshe hii Biashara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…