Ukubwa wa nchi na wingi wa weledi unaousema kungekuwa na failures zote hizo almost ktk kila sekta..wapi serikali inafanya vzr? Taja..kilimo? Mifugo? Uvuvi je? wapi..elimu? miaka zaidi ya 60 tulioanza nao baada ya kupata uhuru..unajua wao walipo? Malaysia, Singapore, South Korea..hata Kenya, Ghana..nk mnadangayana serikalini kuna wenye uwezo wa kubuni na kusimamia, tungekuwa hapa? Kafulila ndiyo think tank ya serikali..r you serious!
Maswali yote nimekuuliza hujajibu hata moja..
1. Taja PPP pilot project yoyote iliyopo kwa sasa..
2. Kuna ulazima gani ku-invite PPP pasina kuwa na mradi wa majaribio..
3. Kuna haraka gani kufanya PPP kwa sasa..
4. Kuna tatizo gani Botswana Almas zao zinawapa faida hapa Tanzania ni tofauti..
5. Kuna nini zaid kilichopo Kenya kufanya uchumi wao uwe imara zaid ya Tanzania..
Waulize hao weledi unaowasema tusikie..
Kuna mentality ya hovyo ndani ya serikali kudhani kuna monopoly ya brain na creativity..which s very wrong! Hata Rais Samia mara kadhaa amesema..inaonekana mambo mengi yanayosemwa nje ya serikali ni bora zaidi ya yanayofanyika au kutoka ndani ya serikali..which s true!
Pole kwa kuchelewa kukujibu nilikuwa busy kidogo.
Sasa iko hivi,
Kenya, Ghana na Tanzania zipo ligi moja kwenye viwango vya kimataifa kiuchumi.
Tena nashangaa kusikia mtu anaitaja Ghana kama mfano bora kiuchumi kulinganisha na Tanzania.
Kifupi Ghana inakabiliwa na matatizo makubwa kiuchumi kuliko Tanzania.
Ni moja ya mataifa yenye mgogoro mkubwa wa madeni. Hata Singapore ni special case ambayo huwezi kuifananisha sio tu na na Tanzania bali nchi yoyote ya Africa ,
Asia na hata Ulaya labda kwa mifano ya kukariri maana leo Singapore ni miongoni mwa nchi10 zenye maisha bora duniani. Imezipita nchi za ulaya zaidi ya 20 sembuse Tanzania.. kwaiyo kuihukumu Tanzania kwa ulinganisho wa Singapore ni kutofahamu vzr kwamba Singapore ni exceptiona case duniani.
Sasa unauliza eti taja mfano 1 tu wa PPP, haya ni maswali ya mtu asiejua maana ya PPP, au hajui kinachoendelea Serikalini.
Haya,
Mkataba wa Songas ni PPP, Mkataba wa TICS ulikuwa PPP, na hata mkataba wa sasa bandari na Adan ni PPP, Mkataba wa DPW ni PPP, TANESCO ina mikataba lukuki ya IPPP kwa kusaini PPA zote zile ni PPP.
kifupi IPP ni PPP. labda urudi shule kidogo utaelewa hili.
Siumesikia Juzi tu mamlaka ya DDC hapo Kariakoo imesaini mkataba wa PPP wa 37bn na kampuni ya TOSH kwa ujenzi na uendeshaji wa Business Complex.
Ukisema Tanzania imefeli kila sekta a wakati leo taasisi zinazofanya credit rating kama Moodys zinaipa daraja la juu kuliko nchi yoyote Afrika mashariki sijui unamaanisha hizo nchi zingine zina hali gani? World Economic Forum wanasema Tanzania inaongoza kwa uchumi jumuifu afrika kusini ya jangwa la sahara afu unasema hakuna inachokiweza.
Ni vema tusijadili kwa mizuka jukwaa la Great Thinker kama JF. Muhimu kujenga hoja kwa facts na reference na kama hujui unauliza badala ya kuhitimisha utadhan unajua. Maswali yote 5 nadhan hayana msingi baada ya hapa.