Kafulila: Milango iko wazi kwa mtu au kikundi kununua vichwa na mabehewa ya SGR kisha kuyaendesha kwa miundombinu ya serikali kwa sharti la ubia

Tunatumiaje zaidi ya 27trilioni pesa za Watanzania kisha Watanzania wachache wanufaike na mradi?
Kumbe Kuna kitu hukielewi, Serikali itaendelea na SGR yake kama kawaida na wabia wataendelea na Biashara zao kama kawaida
 
Kila jambo likishafanyiwa majaribio maeneo mengi kinatengenezwa Standard Unit, PPP sio jambo geni hata hapa Tanzania kwa mfano SONGAS ni mradi wa PPP sijui kama unafahamu hili
Sina hakika kiwango cha uelewa ulicho nacho km kinaweza kupambanua tofauti ya mambo zaid ya mawili..nimekupa mifano biashara ya Almasi kwa mfano kwa nini Botswana inafanya vzr Tanzania haifanyi vzr..nani anaweka hizo standard unit, kwenye maeneo gani? Economic Parameters haziko sawa kwa nchi na nchi, unawekaje standard unit..maelezo yako ni ya jumla jumla tu, wewe umewahi sikia serikali hata kusema sekta zenye potential ya PPP ikizitaja? unadhani mambo ya gas ni sawa na biashara ya DART? ukifanikiwa PPP biashara ya gas then ni principle utafanikiwa PPP kwenye usafirishaji..ndio hivyo? Uonavyo wewe mambo hayo mawili yanalingana?
 
Watakuwepo waliotumia nauli na posho za serikali kupiga oda za injini na mabehewa kwani baadhi waliporudi walisikika wakitoa mchongo huo, sasa nimeelewa kwanini wanataka majina yao yaandikwe.
 
Swala la uelewa wangu halina maana zaidi ya Majibu ya hoja zako,

1. Unamaanisha Tanzania ilipoamua kuanzia hii Sheria ya PPP hawakufanya research?

2. miradi mikubwa kama hiyo ya SONGAS ya PPP hata kama gas unafikiri terms of agreement zinatofautia ?

3. Nadhani utambue tu kuwa hii nchi ni kubwa kuliko Mimi na wewe na inaweledi wengi kuliko Mimi na wewe,

Then, truest the process.
 
Ukubwa wa nchi na wingi wa weledi unaousema kungekuwa na failures zote hizo almost ktk kila sekta..wapi serikali inafanya vzr? Taja..kilimo? Mifugo? Uvuvi je? wapi..elimu? miaka zaidi ya 60 tulioanza nao baada ya kupata uhuru..unajua wao walipo? Malaysia, Singapore, South Korea..hata Kenya, Ghana..nk mnadangayana serikalini kuna wenye uwezo wa kubuni na kusimamia, tungekuwa hapa? Kafulila ndiyo think tank ya serikali..r you serious!
Maswali yote nimekuuliza hujajibu hata moja..
1. Taja PPP pilot project yoyote iliyopo kwa sasa..
2. Kuna ulazima gani ku-invite PPP pasina kuwa na mradi wa majaribio..
3. Kuna haraka gani kufanya PPP kwa sasa..
4. Kuna tatizo gani Botswana Almas zao zinawapa faida hapa Tanzania ni tofauti..
5. Kuna nini zaid kilichopo Kenya kufanya uchumi wao uwe imara zaid ya Tanzania..
Waulize hao weledi unaowasema tusikie..
Kuna mentality ya hovyo ndani ya serikali kudhani kuna monopoly ya brain na creativity..which s very wrong! Hata Rais Samia mara kadhaa amesema..inaonekana mambo mengi yanayosemwa nje ya serikali ni bora zaidi ya yanayofanyika au kutoka ndani ya serikali..which s true!
 
Kuna hii PPP ya Mwendokasi, tuone itakavyokuwa.
 
Huna chochote unachojua, Simply hujitambui
 
Bakhressa kawekeza treni Uganda kwa ajili ya mizigo yake? Kawekeza au ni mteja?
Namaanisha anatumia treni kusafirisha mizigo yake?, mwekezaji yeye anafanya operations. Kuna kitu unachanganya maana ya kuwekeza na kuwa mteja, mfano mm ni natumia bandari ya dar kujngiza mizigo yangu hiyo haimaanishi mm ni mwekezaji wa bandari
Hata hivyo shirika la reli Uganda halina mwekezaji.

Hiyo treni ya utalii nadhani jiridhishe tena na hiyo taarifa, au naomba uniwekee hiyo taarifa nione. Maana SGR ni njia moja tu haiwezi treni hiyo unayosema kusimama hata masaa hayo manne kusubiri mtalii aliyeshuka kufanya utalii
 
Bakresa ni mteja sio mwekezaji Uganda, nadhani ni option nzuri Bakresa kubakia kuwa mteja tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…