===
Mkurugenzi wa Ubia nchi Bwana David Kafulila ameiambia ARIDHIO ya TBC kuwa Sasa ni rasmi mtu au kikundi chochote chenye Uwezo na nia ya kununua na kuendesha vichwa na treni za SGR wanakaribishwa kufanya hivyo Kwa sharti la Ubia na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kafulila anasema kama ilivyo kwa miundombinu ya usafiri na usafirishaji ya Serikalí akitolea mfano wa barabara kuna watu wamenunua Mabasi na wanayaendesha na Serikali inapata kodi lakini kubwa ni Wananchi kupata huduma Bora huduma nzuri na kwa wakati ndivyo itakavyokuwa kwa SGR huku akitolea mfano wa mradi mkubwa kati ya DART na Mbia ambao kwa kiwango kikubwa uko tayari na mabasi zaidi 170 yanaletwa kwa kuanzia.
Kafulila anasema Serikali inafanya haya ili kuchachusha Uchumi wa nchi ( economic stimulus ) ambayo ndio hasa sera za Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na kwa sera hizi ndio zinaifanya Tanzania kuendelea kusalia kileleni kwenye nchi zote za maziwa makuu.
View attachment 3057496