Kafulila: Mitatu ya Rais Samia Uchumi ulikua kutoka US$67bil hadi US$85bil sawa na Ongezeko la TZS 46.8T mnaoshangaa deni la TZS 42T someni hii

Kafulila: Mitatu ya Rais Samia Uchumi ulikua kutoka US$67bil hadi US$85bil sawa na Ongezeko la TZS 46.8T mnaoshangaa deni la TZS 42T someni hii

Ukimsikiliza huyu chizi Kafulila unaweza kudhani nchi imepata uhuru 2021 na wakati muda wote wapo kwenye system
 
Serikali ya awamu ya sita uwazi ni mkubwa sana hivyo rushwa Iko chini sana
Hakika, hapa umenena vema.
Labda kwa awamu zilizopita wananchi hawakuona kwa uwazi wa kiwango hiki matumizi sahihi ya kodi zao, na humo wapigaji pia walipita!
 

View attachment 3109280

Kwa unyenyekevu sana naomba kupitia tweet hii ya Mhe David Zacharia Kafulila.

Nawaomba mnaoshangaa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu kukopa sana niwaombe pia kupitia tweet hii mshangae pia namna Rais Samia anavyokuza Uchumi kwa kiwango ambocho hakijawahi kushuhudiwa kwa miaka mingi.

Hebu nisaidieni ni Rais gani wa Tanzania tangu tupate Uhuru alikuza Uchumi kwa US$ 18bilioni ndani ya miaka Mitatu kama alivyofanya Rais Samia l eo?

Kama kweli kuna jambo mnaweza kumlalamikia Rais Samia kamwe haliwezi kuwa ni jambo la Ukopaji na ukuzaji wa Uchumi Tanzania.

Pia soma Deni La Taifa; Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete na Magufuli kwa pamoja walikopa Trillioni 56.5. Samia kwa miaka 3 amekopa Trillioni 42
Kwanza kukopa hakuna shida,deni la takribani Trilioni 99 ni dogo sana kulinganisha na Ukubwa wa Uchumi wa Tanzania wenye zaidi ya Trilioni 221 za GDP
 
Nashauri tuu si Kwa ubaya lakini
Kafulia arekebishe kwanza ndoa yake na mkewe mmoja ndipo aje kurekebisha uchumi wa linchi looote hili😁
 
Kutoka 65 hadi 85 ni ongezeko la asilimia 27. Tunaweza kusema uchumi wetu ulikuwa unakua kwa asilimia 9 kwa mwaka? Mbona data zinasomaga 5%?
 
mh! tunaona namba tu ila huku mifukoni uchumi unatuchumu!,halina maana hilo ongezeko sasa!.
Ungekuwa haauna mifukoni ngekuwa na smartphone na data za kuja kujibu ujinga humu?
 
Wangetumia hizo nguvu kufanya vitu vinavyoonekana wala wasingehitaji ku convice watu kwamba mambo yapo vizuri wakati wenyewe wanajijua.... Kipimo Halisi Kitaa

  1. Je gharama za maisha (bidhaa) zimepanda au zimeshuka ?
  2. Disposable income je ?
In short watu kitaa wamepigika leo afadhari ya Jana
 
Back
Top Bottom