Kafulila: Pato la Kila Mtanzania litafikia TZS 17M kwa mwaka 2050

Mtanzania yupi.? Ukiwa umeshiba usiwadhihaki wenye njaa. Yaani uende kijijini uwaambie kejeli kama hizi kweli si watakuchoma Moto
 
Huyu Kafulila hana utofauti na watu wa Hali ya hewa/wapiga ramli/ motivation speaker
 
Yuko sahihi maana kwa kipindi hicho mfumuko wa bei utakua juu kibiriti kitauzwa 500 ,unga kilo itakua 3000 kwahiyo itakua kama sasahivi tu
 
Tumbili nae amezidi kubwabwaja
Hapana huo ni Uongo ,hakuna!!
Ni sawa na hadithi za kusadikika za mfalme Jesha!
Kwa mtu mwenye akili zake timamu sawa sawa kabisa na ambaye anaijua vizuri nchi hii pamoja na kuujua vizuri aina ya mtindo wa Utawala wa nchi hii jinsi ulivyo, KAMWE hawezi kumsikiliza huyo mtu anayeitwa David Kafulila and the like kuhusiana na masuala ya uchumi wa nchi hii. It's an idiot!
 
Kwa uhalisia hatakuwepo hivyo anaongea vitu ambavyo hatajibu
 
Sasa utabiri unawezaje kuwa hewa kabla ya muda wake kutumia?
Utabiri lazima uendane na Kile kinachofanyika wakati uliopo, ukiangalia jinsi mambo yanavyoenda nchini kwa wakati huu haikupi hayo matumaini anayoongelea huyo Tumbiri
 
na vitu vimepanda mara mia ngapi toka huo mwaka 2000 hadi leo
chukuamfano sukari ilikuwa shilingi 200 na leo ni kati ya 3000 na 4000
 
Lazima kuhakikisha uchumi unashikwa na watanzania asilia kwa asilimia kubwa, vinginevyo hizo namba hazina maana yoyote.
Mapato yakichukuliwa na wageni, serikali ikawa na takwimu na kumbukumbu zitamsaidia nini mtanzania ambaye atakuwa mtumwa katika nchi yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…