Kafulila: Rais Samia kuongoza mwelekeo wa Tanzania ya miaka 25 ijayo baada ya ile 25 ya Mkapa kukamilika

===
Huu ni mwaka ambao Dira ya Maendeleo ya Taifa ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa (2000-2025) imekamilika kwa mafanikio wakati Dira ya Sasa ya 2025-2050 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeandaliwa na inasubiri kuzinduliwa tu kwa mafanikio pamoja na kwamba huu ni mwaka wa Uchaguzi alisema David Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania PPPC Bw David Kafulila.

Kwenye Dunia hii ambayo ni ya Utandawazi ( information age ) Mahitaji ya binadamu duniani kote yamezidi kuwa makubwa zaidi ukilinganisha na uwezo w Serikali zetu zote duniani kuyakidhi Mahitaji hayo kwa kutumia Mikopo na Kodi ndio sababu Dunia inatutaka sisi kama Serikali kutafuta njia Mbadala ya kuendesha bajeti zetu nje ya Kodi au Mikopo alisisitiza.

Anasema, Kwa mujibu wa Ripoti ya IMF ya Oct 2024 uchumi wa dunia wa Serikali zote duniani umefikia US$ 102trilion wakati deni la dunia ni asilimia 95 ya Uchumi huo, Vile vile Deni lote la sekta binafsi nalo limefikia $164Trilioni huku Uchumi wote wa Dunia ukifikia $110trilioni ( Serikali & private ) lakini deni lote la Serikali, Sekta binafsi na Kaya jumla yake ni US$ 320 trilioni, Kwa maana nyingine deni la Dunia ni karibu mara tatu ya Uchumi wote wa Dunia kwa lugha nyepesi Dunia hii inaendeshwa kwa Mikopo.

Kafulila anasema wakati Uwiano wa deni la Africa kwa Uchumi wa Africa ni 67% Tanzania iko katika Hali nzuri kwani Uchumi kwa deni ni 47% wakati Kenya ni 70%, Rwanda% 71, Malawi 84% Msumbiji 96% Ghana 90% hivyo mwenendo wa deni la Tanzània kwa Uchumi wake ni mzuri ukilingamishwa na Chumi za nchi nyingi za Africa Mashariki na kati na Kusini.

View attachment 3231060
Kwahiyo huyu kijana Kufulila anatwambi kwamba dunia inadaiwa.
 
Kafulila ni mtu bora sana Kwa Sasa hapa Tanzania, hataki rushwa, hataki Ufisadi lakini ni mjuvi wa mambo mengi lazima uongozi umwangalie najua mtanisema Mimi ni chawa wake sawa ila hata nyie msikilizeni kwa makini
Unaweza kuthibitisha haya unayo yasema,nani asiependa hela dunia hii
 
===
Huu ni mwaka ambao Dira ya Maendeleo ya Taifa ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa (2000-2025) imekamilika kwa mafanikio wakati Dira ya Sasa ya 2025-2050 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeandaliwa na inasubiri kuzinduliwa tu kwa mafanikio pamoja na kwamba huu ni mwaka wa Uchaguzi alisema David Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini Tanzania PPPC Bw David Kafulila.

Kwenye Dunia hii ambayo ni ya Utandawazi ( information age ) Mahitaji ya binadamu duniani kote yamezidi kuwa makubwa zaidi ukilinganisha na uwezo w Serikali zetu zote duniani kuyakidhi Mahitaji hayo kwa kutumia Mikopo na Kodi ndio sababu Dunia inatutaka sisi kama Serikali kutafuta njia Mbadala ya kuendesha bajeti zetu nje ya Kodi au Mikopo alisisitiza.

Anasema, Kwa mujibu wa Ripoti ya IMF ya Oct 2024 uchumi wa dunia wa Serikali zote duniani umefikia US$ 102trilion wakati deni la dunia ni asilimia 95 ya Uchumi huo, Vile vile Deni lote la sekta binafsi nalo limefikia $164Trilioni huku Uchumi wote wa Dunia ukifikia $110trilioni ( Serikali & private ) lakini deni lote la Serikali, Sekta binafsi na Kaya jumla yake ni US$ 320 trilioni, Kwa maana nyingine deni la Dunia ni karibu mara tatu ya Uchumi wote wa Dunia kwa lugha nyepesi Dunia hii inaendeshwa kwa Mikopo.

Kafulila anasema wakati Uwiano wa deni la Africa kwa Uchumi wa Africa ni 67% Tanzania iko katika Hali nzuri kwani Uchumi kwa deni ni 47% wakati Kenya ni 70%, Rwanda% 71, Malawi 84% Msumbiji 96% Ghana 90% hivyo mwenendo wa deni la Tanzània kwa Uchumi wake ni mzuri ukilingamishwa na Chumi za nchi nyingi za Africa Mashariki na kati na Kusini.

View attachment 3231060
1.Ameasisi Dira Mpya ya 2025

2.Ameasisi Mageuzi ya Mitaala ya Elimu ya Msingi Hadi Vyuo Vikuu

3.Anakusanya maoni Ili kufumua mfumo wa Kodi ambao imekuwa sio Rafiki Kwa biashara na uwekezaji
 
Back
Top Bottom