Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 3,629
- 3,015
Umechanganya umiliki wa mali na chanzo cha mapato. Hakuna anayesema Halmashauri zisiingize mapato kwenye stendi, masoko, maegesho au vyoo. Hoja ni: je, lazima Serikali itumie fedha zake kujenga na kuendesha kila biashara inayoweza kujengwa na kuendeshwa na sekta binafsi?Huyu cuma sasa kanishinda kumtetea
Maegesho, Stendi za mabasi, masoko, na vyoo vya kulipia huwa ni mali za serikali ya mkoa, wilaya au mji kama njia ya kukusanya mapato
Hata mwekezaji binafsi akijenga au kuendesha stendi, soko, parking au choo kupitia PPP, Halmashauri inaweza kuendelea kupata mapato kwa tozo, ada, kodi, concession fee au mgawanyo wa mapato kulingana na mkataba. Serikali inabaki msimamizi na inaweza kubaki mmiliki wa ardhi au mali kulingana na muundo wa PPP.
Kwa hiyo kusema “ni chanzo cha mapato ya Halmashauri, basi lazima Halmashauri yenyewe ijenge na kuendesha” ni hoja dhaifu. Chanzo cha mapato si lazima kiwe chanzo cha matumizi ya Serikali. Serikali inaweza kupata mapato bila kubeba gharama zote za uwekezaji na uendeshaji kupitia PPPs.