Kafulila: Si sahihi serikali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga maegesho, stendi, majosho, masoko na vyoo vya kulipia

Kafulila: Si sahihi serikali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga maegesho, stendi, majosho, masoko na vyoo vya kulipia

Hoja ya kusema “tatizo si kuzaliana, bali kuwafanya watoto wawe na tija” sio hoja ,

Utawajengeaje wote ubora kama watoto wanaongezeka kwa kasi kuliko uwezo wa uchumi kuongeza walimu, madaktari, madarasa na ajira?

Tanzania ina ukuaji wa watu wa karibu 3% na wastani wa watoto 4.8 kwa mwanamke. IMF inaonya kuwa kasi hiyo inaweza kuzidi uwezo wa uchumi kutoa elimu, afya na ajira za kutosha.

Mfano hai ni Rwanda: uzazi umeshuka kutoka watoto 6.1 kwa mwanamke mwaka 2005 hadi 3.7 mwaka 2025, sambamba na kupanuka kwa uzazi wa mpango; lengo ni kupunguza mzigo wa wategemezi na kuongeza nafasi ya kuwekeza zaidi kwa kila mtoto. Bangladesh nayo ilipunguza uzazi na uwiano wa wategemezi ukashuka kutoka karibu 90 hadi 53, jambo lililofungua nafasi kubwa zaidi ya kuwekeza kwenye rasilimali watu. Vietnam pia ilipitia kushuka kwa uzazi sambamba na kupanda kwa elimu, na leo ina viwango vya juu vya elimu na rasilimali watu ukilinganisha na nchi nyingi za kipato cha kati-chini.

Na Tanzania yenyewe, World Bank imekadiria kuwa ifikapo 2061, hali ya kuwa na watoto wengi inaweza kufanya gharama za elimu ya umma kufikia 4.1% ya GDP, wakati kwa uzazi mdogo zinaweza kuwa karibu 2.9% ya GDP—fedha zinazoweza kuelekezwa kuboresha ubora wa elimu, afya na miundombinu.

Kwa nchi maskini, ushindi si kuwa na watoto wengi halafu kutafuta namna ya kuwahudumia; ni familia kuwa na watoto wanaoweza kuwahudumia vizuri na taifa kujenga kizazi kidogo kwa uwiano, chenye afya, elimu, ujuzi na tija kubwa. Hapo ndipo demographic dividend inapoanzia.
Huo uzazi wa mpango unatokana na uwekezaji kwa kuwaelimiaha wahusika.
Hauji/haitokei tu.
Hivi kweli tumefika kuwaza kuwa Choo ni mradi? Choo nimekuwa chanzo cha mapato?
Choo cha stendi [tuliko mafukara] ni cha kulipa wakati Choo cha uwanja wa ndege [waliko matajiri] ni huduma ya bure.
Kiwango cha matumizi ya choo kitaifa kipo chini mno. Tuna familia nyingi hazina vyoo. Hatuoni hili? Baadhi ya sehemu malipo ya Choo ni sawa na malipo ya chupa ya soda.
Wasomi/wachumi mmekosa vyanzo vya mapato Hadi kuvamia Choo?
Tafakarini.
 
Huo uzazi wa mpango unatokana na uwekezaji kwa kuwaelimiaha wahusika.
Hauji/haitokei tu.
Hivi kweli tumefika kuwaza kuwa Choo ni mradi? Choo nimekuwa chanzo cha mapato?
Choo cha stendi [tuliko mafukara] ni cha kulipa wakati Choo cha uwanja wa ndege [waliko matajiri] ni huduma ya bure.
Kiwango cha matumizi ya choo kitaifa kipo chini mno. Tuna familia nyingi hazina vyoo. Hatuoni hili? Baadhi ya sehemu malipo ya Choo ni sawa na malipo ya chupa ya soda.
Wasomi/wachumi mmekosa vyanzo vya mapato Hadi kuvamia Choo?
Tafakarini.
Hoja yako kuhusu umuhimu wa vyoo na uwezo wa wananchi kulipia ni ya msingi, lakini unaposema “tumefika kuwaza choo ni mradi?” ndipo hoja inapopoteza mwelekeo.

Ndiyo, choo cha umma ni mradi wa miundombinu na huduma. Kinahitaji ardhi, ujenzi, maji, umeme, usafi, wafanyakazi, matengenezo, ukusanyaji na usafirishaji wa taka pamoja na usimamizi endelevu. Hayo yote yana gharama. Swali la msingi si kama choo ni mradi; ni nani alipie gharama hizo, kwa mfumo gani, na maskini atalindwaje?

Kulinganisha choo cha stendi na cha uwanja wa ndege pia hakumaanishi choo cha uwanja wa ndege hakilipwi. Mara nyingi gharama ya huduma hizo imejumuishwa katika mfumo mpana wa mapato na uendeshaji wa uwanja. Kwa hiyo kutokutoa fedha mlangoni si sawa na kusema huduma haina gharama.

Na kama tunakubaliana kwamba familia nyingi bado hazina vyoo, hiyo ndiyo sababu zaidi ya kutafuta uwekezaji mkubwa katika sanitation, si sababu ya kukataa uwekezaji. Serikali haiwezi kutatua kila pengo kwa bajeti na mikopo pekee. Sekta binafsi inaweza kujenga, kuendesha na kutunza miundombinu kwa masharti ambayo Serikali inaweka ili huduma ibaki salama na inayomudu wananchi.
Hapa ndipo PPP inapokuwa na maana. Siyo kugeuza haja ya mwananchi kuwa biashara ya kumnyonya; ni kutumia mtaji na ufanisi wa sekta binafsi kutoa huduma ambayo vinginevyo Serikali ingelazimika kuitolea fedha za kodi au kukopa.

Kama Sh 500 ya choo ni mzigo kwa mwananchi maskini, mjadala uwe namna ya kupunguza gharama, kutoa ruzuku kwa wanaohitaji au kutengeneza mfumo mwingine wa mapato—si kusema choo hakiwezi kuwa mradi.
Na kuhusu uzazi wa mpango, ni kweli elimu na uwekezaji katika afya vina nafasi kubwa. Lakini hilo halipingani na hoja ya kuwekeza katika miundombinu. Taifa linahitaji vyote: watu wenye elimu na afya, pamoja na miundombinu bora inayowahudumia.

Kwa hiyo wachumi hawajaishiwa vyanzo vya mapato kwa “kuvamia choo”. Wanachouliza ni swali rahisi: Huduma hii ina gharama; tukiitaka iwe safi, salama na endelevu, nani atalipa na tutapangaje mfumo usimuumize mwananchi wa kipato cha chini? Huo ndio mjadala unaostahili kufanyika.
 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, amewataka wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa wa Pwani kutumia fursa za ubia na Serikali kuwekeza katika miradi mbalimbali ya miundombinu ya huduma za umma, badala ya kuiachia Serikali pekee jukumu la kugharamia miradi hiyo.

Akizungumza na wafanyabiashara hao, Kafulila alisema katika mazingira ya sasa ya maendeleo, si lazima Serikali ikope au kutafuta fedha za kujenga kila mradi wa huduma za kijamii na kiuchumi, ikiwemo maegesho ya magari, masoko, machinjio, majosho ya mifugo na hosteli za wanafunzi.

"Katika dunia ya leo, si lazima Serikali itafute au kukopa fedha za kujenga maegesho ya magari, masoko, machinjio, majosho au hosteli za wanafunzi. Hivi ni vitu ambavyo kwa kawaida kabisa vinaweza kujengwa na sekta binafsi, na wananchi wakalipia huduma wanazozitumia," alisema Kafulila.

Alifafanua kuwa hata pale ambapo Serikali ndiyo inayojenga miundombinu hiyo, wananchi hulazimika kulipia huduma hizo, hivyo hakuna sababu ya kutoshirikisha sekta binafsi katika uwekezaji wake.

Kwa mujibu wa Kafulila, mfumo wa ubia unaipa Serikali nafasi ya kuelekeza rasilimali zake katika maeneo mengine muhimu ya maendeleo ambayo hayana mvuto mkubwa wa kibiashara, huku wawekezaji wakichangia maendeleo ya miundombinu yenye uwezo wa kujigharamia.

Aidha, alisema sababu nyingine muhimu ya kuhamasisha ubia ni kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Sababu ya pili ya kufanya ubia ni kuleta ufanisi. Sekta binafsi mara nyingi ina uwezo mkubwa wa kusimamia miradi na huduma kwa ufanisi zaidi, jambo ambalo huongeza tija na ubora wa huduma kwa wananchi," alisisitiza.

Kafulila alitoa wito kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi ya ubia, akieleza kuwa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ni nguzo muhimu ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Sawa
 
Huo uzazi wa mpango unatokana na uwekezaji kwa kuwaelimiaha wahusika.
Hauji/haitokei tu.
Hivi kweli tumefika kuwaza kuwa Choo ni mradi? Choo nimekuwa chanzo cha mapato?
Choo cha stendi [tuliko mafukara] ni cha kulipa wakati Choo cha uwanja wa ndege [waliko matajiri] ni huduma ya bure.
Kiwango cha matumizi ya choo kitaifa kipo chini mno. Tuna familia nyingi hazina vyoo. Hatuoni hili? Baadhi ya sehemu malipo ya Choo ni sawa na malipo ya chupa ya soda.
Wasomi/wachumi mmekosa vyanzo vya mapato Hadi kuvamia Choo?
Tafakarini.
Sawa
 
Back
Top Bottom