Kafulila: Tanzania kwa mara ya kwanza tunajenga barabara za kisiasa za kulipia 150km kutoka Kibaha Pwani-Morogoro bila Fedha ya Serikali

Hata hapo Kenya zipo

sasa kenya ina tofauti gani na tanzagiza? kwanza kenya imeanza kuuzwa zamani, weka mfano wa highway system USA, EU au any western christian country ambapo barabara imepewa watu binafsi namaanisha important highway system ambayo ina compromise national security nitajie nchi moja tu iliyofanya hivyo …
 
Kila siku TUTA , TUNATARAJIA, MIAKA IJAYO,. TUNATEGEMEA.
MPAKA SASA SGR HAIFANYI KAZI. MADEREVA WAPO, WAHUDUMU WAPO, MATRENI YAPO, ENGINE ZIPO, RELI IPO. WOTE WANAKULA MSHAHARA PASIPO KUFANYA KAZI.
WATU TUNATESEKA KWENYE FOLENI YA CHALINZE KIBAHA.
 
Ni nyingi sana fanya ku-google
 
Kila siku TUTA , TUNATARAJIA, MIAKA IJAYO,. TUNATEGEMEA.
MPAKA SASA SGR HAIFANYI KAZI. MADEREVA WAPO, WAHUDUMU WAPO, MATRENI YAPO, ENGINE ZIPO, RELI IPO. WOTE WANAKULA MSHAHARA PASIPO KUFANYA KAZI.
WATU TUNATESEKA KWENYE FOLENI YA CHALINZE KIBAHA.
Huyu ni Kafulila hebu na yeye apewe muda tuone
 
View attachment 2985383
Mkurugenzi Mtendaji wa PPP Tanzania Mhe David Kafulila amesema ule mradi wa barabara za kulipia(toll road) uliokwama tangu awamu zilizopita Sasa kwenye awamu hii ya sita umeiva.

Mhe Kafulila amesema, mradi huu utatumia zaidi ya US$ 800 milioni karibu sawa na TZS 2.08Trilioni.

Mhe Mkurugenzi Kafulila amesema barabara zinazokwenda kujengwa zitakuwa ndio barabara Bora zaidi hapa nchi zitakazoishi mpaka miaka 35 bila kufanyiwa Ukarabati mkubwa.

Aidha, Mhe Kafulila amesema nia ni kupunguza msongamano wa magari na watu kati ya Dar-Morogoro-Dodoma ambapo Sasa yule anayehitaji kwenda kwa kasi itamlazimu alipie kiasi Fulani Cha pesa ili apite barabara ya Express.

Mhe Kafulila anaeleza kuwa Tanzania itafunga mkataba na mwekezaji huyo na baada ya mkataba kuisha barabara zitasalia kuwa mali za watoto wa Tanzania.

Kafulila anasema nia kubwa ya Serikali ya Dkt Samia Suluhu ni Watanzania kupata huduma bora kwa gharama nafuu pasina kutumia Fedha ya Serikali.

===​
mheshimiwa Kafulila kamilisheni basi za huku mikoani kwanza,mfano Kigoma Katavi,Kigoma Tabora na Kigoma Kagera.
Kwann mnapenda fantasies sana,miradi ambayo mnaifikiria ni mizuri lakini kamilisheni ya misingi kwanza!
 
Kwahiyo hao bodaboda watakaogongwa na hizo lombardine nani atawalipa fidia? Hizi mwendo kasi za kimara zinaenda 40mph kilasiku wanagongwa, sembuse hizo xpress, mradi kuchelewa sio kwa sababu ya kukosa maarifa waliona ni mradi wa kipuuzi, anasema wajukuu zetu ndo watakabidhiwa ni baada ya miaka mingapi? Kule djibut kuna mwekezaji kagoma kukabidhi bandari, bukina faso ikulu ni ya kupanga kwa wafaransa ilijengwa kwa mikataba hii ya kishenzi
 
tulichelewa sana kufika hapo, tena ikiwezekana wawekwe wakandalasiwatano na wapewe miezi 12 tu ikutane na uchaguzi wa next year. bora hawa wajenge kuliko hao wanaokusanya na kuweka ng'ambo. Mama kazi iendelee.
 
Boda boda anapitaje huko kwa Express hata hivyo,
 
tulichelewa sana kufika hapo, tena ikiwezekana wawekwe wakandalasiwatano na wapewe miezi 12 tu ikutane na uchaguzi wa next year. bora hawa wajenge kuliko hao wanaokusanya na kuweka ng'ambo. Mama kazi iendelee.
Polepole tutafika tu Mungu yupo Upande wetu sana.
 
Back
Top Bottom