David Kafulila, akizungumza na wananchi kupitia kituo cha runinga cha ITV, amewataarifu Watanzania kuwa barabara ya Kibaha–Chalinze, iliyotarajiwa kujengwa kwa mfumo wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi kwa makisio ya zaidi ya Shilingi trilioni moja (1,000,000,000,000), imekataliwa na serikali kwa maslahi mapana ya Taifa.
Kafulila, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC, amesema serikali ilifanya tathmini ya gharama za mradi mzima kabla ya kutangaza kwa sekta binafsi. Kampuni 9 zilionesha nia ya kushiriki, ambapo moja ilitoka Uturuki na zilizosalia kutoka China. Kati ya hizo, 5 zilionesha sifa stahiki, na 3 zikachaguliwa kuwasilisha nyaraka. Hata hivyo, ni kampuni moja tu kutoka China ndiyo iliwasilisha nyaraka hizo.
Mkurugenzi Kafulila ameeleza kuwa mwekezaji huyo alikuja na gharama kubwa zaidi ya ile iliyotathminiwa na serikali. Kwa msingi huo, serikali ilikataa kuendelea na mkandarasi huyo, akisisitiza kuwa kufanya hivyo kungeumiza Taifa na wananchi watakaotumia barabara hiyo kwa muda mrefu.
Aidha, Kafulila amesema serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji wengine kupitia Special Arrangement kwa usimamizi wa TANROADS.