Kagame alinda vijana wa Rwanda kwa wivu mkubwa

Kagame alinda vijana wa Rwanda kwa wivu mkubwa

Soul21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
210
Reaction score
351
1000426247.jpg

Hayawi hayawi yametimia. Baada ya hotuba ya rais wa Rwanda Paul Kagame kwa vijana wake akiwataadharisha juu ya athari ya pombe na hatima ya maisha yao leo naona habari yenye mvuto juu ya kupipgwa maarufu pombe kali kutoka Tanzania.

Hapa Tanzania tunataka tupate maendeleo ya haraka mno, I mean shortcut huku tukiangamiza kizazi kipya.

Pombe zimekuwa nyingi mno na bei rahisi hapa nchi kisa tu wanalipa kodi huku wengine wakiwa hata koda hawalipi na pombe wanauza.

TBS wamejaa ofisini wakizunguka na viti tu huku vijana wajinga( fikra zilizolala wakibuia pombel) na nguvu pekee waliobakiwa nayo ni kuitukana serikali .

Waandishi nendeni Mikoa ya Kaskazini mkaone watoto wadogo wanavyoangamia.

Asante Kagame kwa kuwema maslahi pembeni na kulinda afya za raia wako.
 
Tokea lini serikali ya CCM ikawaonea huruma vijana? Wana uziwa kik, visungura waharibu afya zao wafe mapema
Boda boda nazo zinapunguza idadi ya vijana

Hali inatisha siku hizi vijana wengi wanakufa mapema kuliko wazee
 
Twende mbele turudi nyuma,hii sekta ya pombe imekaa kikatili sana sio kwa wanywaji (wateja)Wala wahudumu,Huwa naona muhudumu yeyote wa bar ni mtumwa aliyechangamka.hebu fikiria mtu analipwa elfu 50 kwa mwezi Kwa hiyo ili aendane na hali ya maisha ni lazima auze uchi kwa wanaume tena kwa bei ndogo.NCHI YETU IMEKAA KIKATILI SANA
 
Tokea lini serikali ya CCM ikawaonea huruma vijana? Wana uziwa kik, visungura waharibu afya zao wafe mapema
Boda boda nazo zinapunguza idadi ya vijana

Hali inatisha siku hizi vijana wengi wanakufa mapema kuliko wazee

Only thing serikal inajali ni mapato, kodi itokanato nia vinywaji. Effects na vitu vingine mtajua wenyewe
 
Back
Top Bottom