Kagame anataka DRC iwatambue waasi wa M23 lakini yeye hataki kuwatambua waasi wa kihutu!

Kagame anataka DRC iwatambue waasi wa M23 lakini yeye hataki kuwatambua waasi wa kihutu!

..fdlr wako wangapi?

..Rwanda walishauwa Wahutu wengi sana katika makambi ya wakimbizi kipindi walipowavamia Mobutu na Kabila Snr.
Hoja yako ni kuwa FDRL wako "extinct"?!!
Hakuna FDRL wanaomiliki silaha na kuendesha operations za kijeshi ndani ya DRC na kufanya ugaidi nchini Rwanda?
 
..bado kuna tatizo la Tutsi vs Hutu katika nchi za Rwanda na Burundi.

..Rwanda ina-support Watutsi wanaopinga serikali ya Burundi.

..Burundi nayo ina-support Wahutu wanaopinga serikali ya Rwanda.

..kuhusu Fdlr tunapaswa kujiuliza kama bado ni walewale waliohusika na genocide au ni kundi tofauti?

..kuhusu M23, kwanza tunapaswa kuondoa malalamiko kuhusu uraia wao, halafu wawe chama cha siasa na washiriki uchaguzi.

..kama ni kundi tofauti na waliohusika na genocide madai yao ni yapi?
Point nzuri....

Sasa kama kuna watutsi wanaokuwa backed na Rwanda kuipinga serikali ya Burundi "and vice versa is true" ,mbona hatuoni nchi hizo zikiingiliana kutafuta "opponents" wao?!!
 
Sawasawa....

Kweli kabisa.....

Kagame anayajua hayo vyema tu...nilifuatilia zile GACHAGA na kujifunza hayo.....

Ni sawa na si kila BANYAMULENGE anawaunga mkono M 23....haitofautiani na ukweli kuwa kulikuwa na watutsi waliohusika kuwaua wahutu kipindi kile cha "genocide"....sawa na kuhilikishwa kwa wahutu waliopinga mauaji yale...hakika ni mvurugano unaotaka suluhu kupitia UTULIVU NA BUSARA KUBWA.....

..fuatilia hapa chini nini kiliwatokea wakimbizi wa Kihutu waliokimbilia DRC.

 
Hoja yako ni kuwa FDRL wako "extinct"?!!
Hakuna FDRL wanaomiliki silaha na kuendesha operations za kijeshi ndani ya DRC na kufanya ugaidi nchini Rwanda?

..Naona kama kwa Rwanda, Mhutu, au yeyote yule, akidai haki anapachikwa Uinterahamwe.
 
..Naona kama kwa Rwanda, Mhutu, au yeyote yule, akidai haki anapachikwa Uinterahamwe.
Ziko tuhuma hizo....

Binafsi najua watawala na wanasiasa "sometimes" wanajificha kuwajibika kwa kutumia "ngao za dhulma walizofanyiwa huko nyuma"....POLITICS

Ninaamini vizazi vijavyo vitaweza kuwa na "approaches" bora na mizania ya HAKI zaidi ya ilivyo sasa.....

Yaliyotokea Rwanda na Burundi ni "case study" kwa nchi zetu kutothubutu UBAGUZI na BIGOTRY kwani kuna msemo wa KIDINI usemao "FITINA HUWA IMELALA KAMWE USIIAMSHE"....

#Long live Tanzania yetu na watanzania wenye kuiabudu AMANI !!
 
..chunga kauli zako baada ya kusoma usije ukaitwa Interahamwe!!
Ha ha ha mimi sina upande wowote mkuu....

Siamini katika ubaguzi wa aina yoyote.....

Imani yangu ni AMANI ,HESHIMA NA USAWA kwa wote.....

Ninachotaka ni kuona tu watu wakiwajibika vyema kwa kufichuliwa unyama na uovu wao waliowafanyia/wanaowafanyia wengine.....

#Long Live AMANI ya Tanzania yangu pendwa!!
 
Hivi kwanini huyu jamaa PK anaogopwa kuambiwa ukweli? Ana nini hasa cha kutisha kiasi ma rais wa nchi karibu 5 kuogopa kumwambia ukweli??
 
Hivi kwanini huyu jamaa PK anaogopwa kuambiwa ukweli? Ana nini hasa cha kutisha kiasi ma rais wa nchi karibu 5 kuogopa kumwambia ukweli??
Watu wazima hawaogopani....

Viongozi hawaogopani....

Diplomasia ndio imani kuu ya kiuongozi......

Kubwa zaidi ni rais wa nchi , unataka ABWATUKIWE ?!! Ha ha ha
 
Back
Top Bottom