Kagame anataka DRC iwatambue waasi wa M23 lakini yeye hataki kuwatambua waasi wa kihutu!

Kagame anataka DRC iwatambue waasi wa M23 lakini yeye hataki kuwatambua waasi wa kihutu!

FDLR hawataki kurudi Rwanda

..usiseme Fdlr hawataki kurudi Rwanda.

..sema Fdlr hawataki kurudi Rwanda kwa njia za amani.

..kinachotakiwa kufanyika ni kukaa nao mezani na kusikiliza madai yao.

..Genocide dhidi ya Watutsi tulipoteza watu karibia millioni 1, lakini tangu Rwanda na Uganda wavamie DRC mwaka 1998 tumepoteza watu millioni 6 au zaidi.

..Hatuwezi kuwaendekeza viongozi wakatili wasiokuwa na ubinadamu.
 
Wakimbizi wa kihutu hawaishi katika makambi ya wakimbizi....wakimbizi gani wana silaha na armoured machineries?!!!

Watanzania tungekubali wakimbizi wa kirundi wawe na silaha za kivita na kurandaranda katika ardhi yetu?!!

..Rwanda walishapewa ruhusa na serikali kufanya operation za kuwasaka Fdlr ktk ardhi ya DRC.

..sasa badala ya Rwanda kuendeleza urafiki huo amekwenda ku-support kikundi cha waasi wanaotaka kupindua serikali ya DRC.

..Rwanda ndio wanaochochea mgogoro na mauaji ya wananchi wasio na hatia.
 
Ujinga ndio huo....

Unawezaje kutoa ruhusa kwa majeshi ya kigeni kusaka watu wao ndani ya nchi yako tena militarily?!!

Serikali ya DRC ndio mwanzo wa matatizo yote.....
 
Soma vizuri, Hao banyamulenge ni Warwanda waliokimbia vita vya kimbari. Na kufika Congo wakaungana na watusi wenye asili ya Congo. Kumbuka watusi wa Congo, Rwanda na Burundi walikua ni jamii moja ambayo ilikuja kutenganishwa na mipaka tu.So wale watusi waliopo Congo kuna wacongo na warwanda. Sawa na wamasai wa Tz wakimbilie Kenya then Kenya iwachanganye wote wamasai wa Kenya na Tz kama wahamiaji haramu.
Uongo mtupu....

Revise your notes....

Banyamulenge wako miaka mingi kabla ya kuitwa hata Zaire ya Mobutu....walikwenda huko baada tu ya vita vya pili vya dunia 1945.....

Fanya "research" kabla ya kuonyesha ujinga mbele za watu.....
 
mkuu, Yuko sahihi wale ni wahutu na watutsi wa kongo....zingatia mipaka ya kimataifa ...kama DRc haiwapi Huduma unataka warudi Rwanda
 
Toka mwaka 2000 ilipoundwa FDLR Kagame hajawahi kuwa na nia ya kuzungumza nao.

Wasubiri mpaka lini ?
Sawa....

Ili mazungumzo yawe na tija ni lazima kwanza wakiri kuhusika na mauaji ya kimbari.....

Mbona wengine walikubali katika zile mahakama za GACHAGA?!!

Walikiri kuhusika kwao....wako waliosamehewa kupitia "njia za kimahakama".
 
Sio wapiganaji wote wa FDLR wamehusika na genocide.

Wengi wao ni watoto wa wakimbizi wa kihutu waliozaliwa huko Drc ukimbizini baada ya genocide ila wameshika silaha Sasa Ili kujihamia dhidi ya kushambuliwa na jeshi la Rwanda na washirika wao.

Hawa watoto wakiri nini wakati hata hawakuhusika?
 
Moja ya utetezi aliokuja nao Rais Kagame kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na EAC kuhusu kutatua mgogoro wa DRC ni kutaka serikali ya DRC iwatambue kwanza waasi wa M23 ambao wanajumuisha jamii ya walowezi wa kitutsi iliyopo DRC (Banyamlenge), lakini hapo hapo Kagame hataki kabisa kutaka kusikia suala la waasi wa kihutu waliokimbilia DRC nao kutambuliwa kama sehemu ya jamii ya Rwanda yenye haki ya kuongoza na kutawala Rwanda.

Kweli mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
Wahutu, FDLR,ni wana jeshi wazamani, wa serikali ya Rwanda chini ya, Juvenal habyarimana, walioendesha mauaji ya kimbari dhidi ya watusi, hawa ni wanyarwanda, hawajanyanganywa uraia, ila wana kesi ya mujibu, inabidi wawe jera!
M23, ni wa Congo wenye asili ya Rwanda, kwa kimombo, ni rwandese speaking Congolese. Hawa wapo kwao, kwa muda mrefu serikali ya Kinshasa imekuwa ikiwabagua kisa tu wanafanana na watusi wa Rwanda! Fikiria u wafukuze wamasai wa Arusha, waende Kenya, kisa tu kuna wamasai Kenya, m23, wanyamurenge, wanataka haki Yao kutambuliwa kama wa Congo, kama Congo kinshasa, haiwataki, iwarudishe Rwanda na Ardhi Yao!Ukifukuza wamasai waende Kenya, mega na Arusha iende, ukifukuza wamakonde wa mtwara waende msumbiji kwa ndugu zao, mega na mtwara iende! It's no brainer ni swala Dogo tu!
Vita inayoendelea sasa, visababishi vingine vikaingia, kuna madini pale, Kagame available, jwtz ya kikwete iliiba, Ramaphosa anaiba,ufaransa anaiba,! Majizi ni mengi na yana siraha!
 
Hawajakatazwa kurudi, wanaogopa wenyewe kawani wengi waowanajua walivyoshiriki kwenye genocide. Waende tu watapokelewa.
Kuna KITU sikielewi....
Tangu genocide mpaka Leo ni miaka 30! Hapo FDLR si watakuwa ni wazee sasa? Kagame anawaogopaje wazee🤭🤭

Kuna HIKI pia...
Kabla Kagame hajawa rais, yeye na RPF yake walikuwa ni waasi dhidi ya Serikali ya Habyarimana wakiwa KATIKA maeneo na sababu Sawa na hizo walizonazo FDLR. Anafeli wapi kushughulikia huo mgogoro kwa amani??
 
Jinai haifi....

Uzee si "immunity" ya jinai....

Tukiachana na hayo....

Imagine mfanya jinai alikuwa na 20s...miaka 30 baadaye hata hajafikia umri wa kustaafu hapa Tanzania.....
 
Wahutu, FDLR,ni wana jeshi wazamani, wa serikali ya Rwanda chini ya, Juvenal habyarimana, walioendesha mauaji ya kimbari dhidi ya watusi, hawa ni wanyarwanda, hawajanyanganywa uraia, ila wana kesi ya mujibu, inabidi wawe jera!
M23, ni wa Congo wenye asili ya Rwanda, kwa kimombo, ni rwandese speaking Congolese. Hawa wapo kwao, kwa muda mrefu serikali ya Kinshasa imekuwa ikiwabagua kisa tu wanafanana na watusi wa Rwanda! Fikiria u wafukuze wamasai wa Arusha, waende Kenya, kisa tu kuna wamasai Kenya, m23, wanyamurenge, wanataka haki Yao kutambuliwa kama wa Congo, kama Congo kinshasa, haiwataki, iwarudishe Rwanda na Ardhi Yao!Ukifukuza wamasai waende Kenya, mega na Arusha iende, ukifukuza wamakonde wa mtwara waende msumbiji kwa ndugu zao, mega na mtwara iende! It's no brainer ni swala Dogo tu!
Vita inayoendelea sasa, visababishi vingine vikaingia, kuna madini pale, Kagame available, jwtz ya kikwete iliiba, Ramaphosa anaiba,ufaransa anaiba,! Majizi ni mengi na yana siraha!

..bado kuna tatizo la Tutsi vs Hutu katika nchi za Rwanda na Burundi.

..Rwanda ina-support Watutsi wanaopinga serikali ya Burundi.

..Burundi nayo ina-support Wahutu wanaopinga serikali ya Rwanda.

..kuhusu Fdlr tunapaswa kujiuliza kama bado ni walewale waliohusika na genocide au ni kundi tofauti?

..kuhusu M23, kwanza tunapaswa kuondoa malalamiko kuhusu uraia wao, halafu wawe chama cha siasa na washiriki uchaguzi.

..kama ni kundi tofauti na waliohusika na genocide madai yao ni yapi?
 
Sio wapiganaji wote wa FDLR wamehusika na genocide.

Wengi wao ni watoto wa wakimbizi wa kihutu waliozaliwa huko Drc ukimbizini baada ya genocide ila wameshika silaha Sasa Ili kujihamia dhidi ya kushambuliwa na jeshi la Rwanda na washirika wao.

Hawa watoto wakiri nini wakati hata hawakuhusika?
Sawasawa....

Kweli kabisa.....

Kagame anayajua hayo vyema tu...nilifuatilia zile GACHAGA na kujifunza hayo.....

Ni sawa na si kila BANYAMULENGE anawaunga mkono M 23....haitofautiani na ukweli kuwa kulikuwa na watutsi waliohusika kuwaua wahutu kipindi kile cha "genocide"....sawa na kuhilikishwa kwa wahutu waliopinga mauaji yale...hakika ni mvurugano unaotaka suluhu kupitia UTULIVU NA BUSARA KUBWA.....
 
Jinai haifi....

Uzee si "immunity" ya jinai....

Tukiachana na hayo....

Imagine mfanya jinai alikuwa na 20s...miaka 30 baadaye hata hajafikia umri wa kustaafu hapa Tanzania.....

..fdlr wako wangapi?

..Rwanda walishauwa Wahutu wengi sana katika makambi ya wakimbizi kipindi walipowavamia Mobutu na Kabila Snr.
 
Back
Top Bottom