Mkunazi Njiwa
JF-Expert Member
- Apr 22, 2023
- 8,538
- 7,559
Hoja yako ni kuwa FDRL wako "extinct"?!!..fdlr wako wangapi?
..Rwanda walishauwa Wahutu wengi sana katika makambi ya wakimbizi kipindi walipowavamia Mobutu na Kabila Snr.
Point nzuri......bado kuna tatizo la Tutsi vs Hutu katika nchi za Rwanda na Burundi.
..Rwanda ina-support Watutsi wanaopinga serikali ya Burundi.
..Burundi nayo ina-support Wahutu wanaopinga serikali ya Rwanda.
..kuhusu Fdlr tunapaswa kujiuliza kama bado ni walewale waliohusika na genocide au ni kundi tofauti?
..kuhusu M23, kwanza tunapaswa kuondoa malalamiko kuhusu uraia wao, halafu wawe chama cha siasa na washiriki uchaguzi.
..kama ni kundi tofauti na waliohusika na genocide madai yao ni yapi?
Sawasawa....
Kweli kabisa.....
Kagame anayajua hayo vyema tu...nilifuatilia zile GACHAGA na kujifunza hayo.....
Ni sawa na si kila BANYAMULENGE anawaunga mkono M 23....haitofautiani na ukweli kuwa kulikuwa na watutsi waliohusika kuwaua wahutu kipindi kile cha "genocide"....sawa na kuhilikishwa kwa wahutu waliopinga mauaji yale...hakika ni mvurugano unaotaka suluhu kupitia UTULIVU NA BUSARA KUBWA.....
Sawa ngoja niisome kwa utulivu......fuatilia hapa chini nini kiliwatokea wakimbizi wa Kihutu waliokimbilia DRC.
Hoja yako ni kuwa FDRL wako "extinct"?!!
Hakuna FDRL wanaomiliki silaha na kuendesha operations za kijeshi ndani ya DRC na kufanya ugaidi nchini Rwanda?
Sawa ngoja niisome kwa utulivu....
Ziko tuhuma hizo......Naona kama kwa Rwanda, Mhutu, au yeyote yule, akidai haki anapachikwa Uinterahamwe.
Ha ha ha mimi sina upande wowote mkuu......chunga kauli zako baada ya kusoma usije ukaitwa Interahamwe!!
Watu wazima hawaogopani....Hivi kwanini huyu jamaa PK anaogopwa kuambiwa ukweli? Ana nini hasa cha kutisha kiasi ma rais wa nchi karibu 5 kuogopa kumwambia ukweli??