Baltazar Engongo
JF-Expert Member
- May 6, 2024
- 604
- 932
Unapoandika kwa kirefu hivi jitahidi uweke paragraphNimekupa mfano tu....,kama Congo wananunua vitu minor kama mkaa..,utawauzia vitu vingapi vikubwa unavyozalisha? Kusipokuwa na wananunuaje?
Umesema kwa nini hatuingili mgogoro wa Somalia....ni jambo lisilo na uwiano na maelezo yangu kuhusu DRC....kwa sababu nilisema upande wa mashariki ya Congo ,kutokana na kijiografia watatarajiwa kuitumia zaidi Dar port kwa export jambo ambalo linainufaisha Tanzania. Somalia siyo land locked,wana bandari..na position yao kijiografia haiitegemei Tanzania..kwa hiyo hatuwezi kunufaika directly na Somalia...,kwa hiyo kwa nini tuhusike Somalia. Lakini Mashariki ya Congo ikiwa na misukosuko, Tanzania inaathirika moja kwa moja kiuchumi na kibiashara.
Umesema nikasome historia ya huo mgogoro....na kwamba rais Kabila na aliingia mikataba na Rwanda. Sijui unamaanisha nini kuhusu hilo....au una maanisha misemo ya vichochoroni inayodai kwamba Kabila alikubaliana na Rwanda kwamba endapo Rwanda itamsaidia kumuondoa Mobutu madarakani,malipo kwa Rwanda iwe ni kumegewa Kivu kaskazini?
Hayo ni maneno ya vichochoroni kwa sababu hata huyo Kagame hajawahi kudai hilo popote na kamwe hawezi kudai.
Madai ya Rwanda na Uganda yalikuwa kuna waasi wamefanya makazi ndani ya Congo lakini wana malengo ya kuzipiga nchi zao. Wote Uganda na Rwanda wakaingia na kuweka kambi ndani ya Congo na kujihusisha na uchimbaji wa madini. Uganda kaondoa majeshi miaka michache tu nyuma baada ya kitisho cha kushtakiwa kimataifa. Lakini wote Uganda na Rwanda wakatumia ujanja wa kutengeneza waasi wa kuchonga M23 ili wafanye yale yale kwa niaba yao.
Ulichonacho ni uoga dhidi ya Rwanda, wala hakuna kingine. Hii hofu kakutegenezea nani?