Anonymous
Senior Member
- Apr 6, 2006
- 118
- 339
Paul Kagame
Siku za nyuma, Katibu Mkuu wa chama tawala, RPF inkotanyi, bwana Wellars Gasamagera, alitamka wazi kuwa, RPF haiwezi kuachia madaraka kwa mtu mwingine au chama chochote.
Ikumbukwe, chaguzi zote zilizopita, matokeo ya uchaguzi yalionyesha kiongozi wa chama hicho, ambaye mara zote ni Paul Kagame, zimeleta matokeo ya kujiuliza mara mbili mbili. Hajawahi kupata chini ya 95%.
Japo yawezekana ni kweli kuwa Kagame anapendwa na raia wake kwa kiasi kikubwa, lakini haijawahi kutokea nchi nyingine hasa za Afrika, kuwa na uchaguzi wa namna hiyo.
Kujiunga chama tawala si hiari
Japo kwa usiri mkubwa, lakini watu wote hasa wanaopatikana kiurahisi (wanafunzi vyuoni, wafanyakazi sehemu mbalimbali, wafanyabiashara, nk)nchi nzima, wote hulazimishwa kujiunga na chama hicho, hata kama hujapenda.
Wafuasi wa chama husakwa kwa njia mbalimbali na bila ridhaa, huorodeshwa na kulishwa kiapo. Ukishakula kiapo, ni sawa na umejitia kitanzi.
Kuchangia chama tawala ni lazima
Kwanza kabisa, bila kujali hali yako kiuchumi, lazima utoe kile utakachoombwa.
Hivi majuzi wakati wa mchakato wa vuguvugu la Uchaguzi linaloendelea, kumekuwepo malalamiko ya wafanyakazi waliokatwa kiasi furani cha mishahara yao - kama michango ya uchaguzi. Hapo hapo, kama wanachama, pia michango ya chama inaendelea. Na matokeo yake, taarifa hutolewa kwamba wametoa kwa hiari yao.
Wananchi wanaolipwa hadi laki na nusu kwa mwezi walilazimishwa kutoa elfu 20 ya Rwanda (yaani, 20,000 ya Rwanda ni takribani TZS 40,000). Na wakuu wa shule za sekondari, wao wanatakiwa kutoa laki 2 za Rwanda. Familia za walalahoi, kila familia ni elfu 3 (sawa na TZS 6,000).
Hizi pesa hukatwa kwenye mishahara(kwa wafanyakazi) na huletewa fomu na kusaini kuwa wametoa kwa hiari.
Na, ndo mnaposikia kwamba Bajeti ya Taifa la Rwanda inajitegemea kwa 85%, mbinu zinazotumika ni hizi hizi. Pia kwenye Mamlaka ya Mapato, faini na hesabu zisizo na maelezo, huwaha na mbinu hizo hizo. Trafiki wanatumia mbinu zilezile, za kukubambikia makosa na huwezi kukataa kulipa. Huku ukijenga nyumba nzuri bila maelezo ya kutosha juu ya pesa umepata wapi, elewa hiyo si nyumba yako yako tena. Iwe umenunua gari au ardhi, na maelezo yako hayatoshi kueleza ulipatapata vipi pesa, elewa ndo kwaheri!
Bahati mbaya, kwa kuwa ni agizo la serikali, wengi wao hubaki na mateso mioyoni mwao na hawana wa kuwasaidia.
Ukivunja kiapo, utakiona cha moto
Kwenye kiapo, unakiri mwenyewe kwamba ukienda kinyume na kiapo hicho, basi wewe uchukuliwe hatua kama adui yeyote.
Hii ndo imepelekea baadhi ya watu kukosa uhuru na kujawa na hofu.
Ubaguzi wa waziwazi
Juzi, Juni 20, 2024 Waziri wa Mambo ya Maafa, Mej. Jenerali (mstaafu) Albert Murasira alinukuliwa akiongea kuhusu raia wa Rwanda waliomaliza kifungo katika gereza la Umoja wa Mataifa, kwamba kuna wadhifa wamevuliwa hivyo hawana nafasi kwao.
Kauli hii hii, hutumika pia kwa familia za watu zinazohusishwa na mauaji ya 1994 dhidi ya kabila la watutsi. Hawa, hutengwa kimtindo katika shughuli mbalimbali hasa za kisiasa.
Ikumbukwe pia kuwa serikali hii ndo iliyohimiza watu kuwa kosa la mtu ni lake tu, ila imefikia hatua hata wengine wanaonja machungu ya dhambi ambazo hawajazitenda au zilitendwa na wazee wao.
Sasa, demokarasia inayohubiriwa Rwanda iko wapi? Je, uhuru wa kujieleza, uko wapi?!
Inakuwaje vyombo vya dola haviruhusu wananchi kuongea kwa uhuru ili mamlaka husika ziweze kujua kero za wananchi na kuzitatua (maoni yasiyohitajika huminywa na kupitisha tu yenye kusifia)?
Kuna wanyarwanda wengi, wamefilisiwa na kuharibiwa maisha na mfumo wa utawala. Wao wenyewe wakiwa wahanga wa siasa hiyo, familia zao ndio huathirika zaidi.
Uenguaji wagombea kibabe
Kama kweli uchaguzi ni wa haki, kwanini kuna mbinu za kuwamaliza wengine wasishiriki kwenye mchakato huu? Haiwezekani watu zaidi ya sita wadaiwe kuwa na kosa la aina moja, na hivyo kupelekea kukosa sifa za kushiriki.
Yupo mgombea aliyesingiziwa kuwa na ukichaa. Tuseme wako sahihi, lakini ilikuwaje akaundiwa akatakiwa kuchunguzwa afya ya akili, wakati jamii ilikuwa inamwona yupo tu sawa?