View: https://www.youtube.com/watch?v=oRSdtN4PaWI
“Mnajua jinsi rais wa sasa alivyoingia madarakani? Aliitwa tu ofisini, na huyu mtu akadhani anafanya makubaliano mazuri, akaikabidhi mamlaka. Pia mnajua kwamba kulikuwa na mashahidi, marais wa nchi mbalimbali? Mnajua hilo? Mmoja wao akiwa rais wa zamani wa Kenya, Kenyatta. Mwingine akiwa rais wa Misri, Na mwingine akiwa rais wa Afrika Kusini, Ramaphosa. Mnaweza kwenda kuwauliza swali hili.
Hii yote mnayoiona sasa… natamani wangejitokeza waziwazi na kusema, ‘Subiri kidogo, sisi tunaijua hii historia.’
Na jambo lingine ni kwamba mnajua Rwanda imekuwa ikilaumiwa kuhusu M23 huko mashariki mwa Congo, na mambo mengine mengi. Sawa, mnaweza kutulaumu kwa kufanya chochote tulichoweza kuhakikisha kwamba FDLR haisababishi Rwanda matatizo, pamoja na wale waliokuwa wanaiunga mkono. Lakini hamwezi kutulaumu kwa kuanzisha huu mgogoro, kwa sababu kila mtu anajua ulianzia wapi na ulianzishwa na nani. Haina uhusiano wowote na Rwanda.
Hii M23, nilishasema kabla, ilitoka Uganda. Hawakutoka hapa Rwanda. Kwa nini basi Uganda haikulaumiwa?”