Kagera: Amuua Mama yake mzazi baada ya Mganga kumwambia apeleke damu ili kuongeza utajiri

Kagera: Amuua Mama yake mzazi baada ya Mganga kumwambia apeleke damu ili kuongeza utajiri

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Fredius Philibart Kibengo mkazi wa Omurushaka wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua mama yeke mzazi kwa kumkata shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali baada ya mganga wa kienyeji kumtaka kupeleka damu ya mama yake au ndugu yake wa karibu ili kutengenezewa dawa za kuongeza utajiri kwenye biashara.

Katika uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera umebaini kuwa katika kipindi cha siku chache kabla ya tukio hilo kutokea mtuhumiwa alisafiri kuelekea nchini Burundi kutafuta dawa za kuongeza utajiri na aliporejea nyumbani kwake alimshirikisha mkewe kuhusu mashariti aliyopewa na waganga wa kienyeji lakini mke wake hakukubaliana na masharti hayo.

Hata hivyo Februari 17 mwaka huu mtuhumiwa alionekana maeneo ya nyumbani kwa mama yake mzazi na ilipofika usiku wa kuamkia Februari 18 alimvamia mama yake na kumkata na kitu chenye ncha kali kisha kupoteza maisha.

Hata hivyo kamanda Malimi amewataka wakazi wa mkoa wa Kagera kujiepusha na imani za kishirikina ambazo zimekuwa zikichangia mauaji ya wananchi wasio na hatia.

ITV
 
Hizi pesa hiziii,
Haya hata kama umefikia hukooo, ndio umkate kiasi cha kuua, nakati shida ni damu...

Ngoja sasa akale na kuamka kwa firimbi.
Na huo utajiri aliokua nao anaukosa piaa
 
Kumbe kile kisa cha yule mkuu aliye kwenda Kongo kusaka utajiri, kinaweza kuwa cha kweli. Huyu mwenzie alienda hapo Burundi kusaka dawa ya utajiri!
 
Pwani hadi zanzibar huko si ndo mto katoka falme za kiarabu kuja kununua jini na kitita cha sh milioni 150? Unadhani huyo jini anakunywa mbege?
Hiyo ya majini hayahusiani na hayo mnayoyafanya huko watu wa bara
Unauaje mzazi wako kisa mali?
Hayo huwezi kusikia pwani
 
Back
Top Bottom