Kagera: Amuua Mama yake mzazi baada ya Mganga kumwambia apeleke damu ili kuongeza utajiri

Kagera: Amuua Mama yake mzazi baada ya Mganga kumwambia apeleke damu ili kuongeza utajiri

Huyo mganga haishi kidigitali, ni kitu kinatumwa tu dakika 0 mtu ameshaondoka.
 
Sema pande zile wanyambo nao wachawi sana ,, mitaani kuna vichaa wa kutosha na matajiri wao wengi ukija kusikia habari zao wengi wana utajiri wa ndumba
 
Kwahiyo angefanya hayo kimya kimya ingekuwa saw! Yaani umeamua kwa dhati ku deflect blame kwa mwanamke. Muwapumzishe wanawake siku mara zote wanahusika kwenye ujinga wenu.
Mwanaume bila mwanamke utajiri wa nini? Kwa hiyo unataka kusema mwanaume alijishawishi mwenyewe kutafuta utajiri kwa njia hizo bila kushawishiwa na mkewe? Kikulacho kinguoni mwako.
 
Kwako ni sahihi jamaa kumuuwa mama yake
Hujamwelewa jamaa., yeye hajasema ni sawa kuua mama yake. Ila katoa angalizo kiujumla katika yote mwanamke si msiri hata siku moja.
Hivyo tujihadhari na wanawake/wake zetu katika mipango yoyote ile wao. Hawawezi kuvumilia kukaa na kitu moyoni.
 
watu wa kagera ,punguzeni matukio,mna trand Sana kwa matukio ya ajabu ajabu.nn shda !!?
 
Huyo mkewe nae ana kesi ya kujibu,baada ya kutaka kushirikishwa katika hayo mauaji alitakiwa kutoa ripoti Polisi ili kunusuru hayo mauaji kabla hayajatokea,

Unamuua Mama yako kisa utajiri? Na huo utajiri angeupata angeutumia na nani wakati tunatambua kua Nani kama Mama,

Mama kakibeba kiumbe miezi 9 tumboni,kisha kikazaliwa,akakilea kwa mateso mpaka kikakua,masikini kumbe hakua anajua analea kiumbe kitakachokuja kuyaondoa maisha yake hapa Duniani!

Tuwe tunawaelimisha watoto wetu toka wakiwa wadogo ili waachane na hizi imani za kipumbavu.
 
Back
Top Bottom