Kagera: Amuua Mama yake mzazi baada ya Mganga kumwambia apeleke damu ili kuongeza utajiri

Kagera: Amuua Mama yake mzazi baada ya Mganga kumwambia apeleke damu ili kuongeza utajiri

Tukisema ndumba na ramli potofu zitumike kuj3nga madaraja, barabara, kuleta mvua, computer, chakula n.k. hamtaki!
Wasukuma twaua wazee wenye macho mekundu, albino, sijuwi wahaya mama zao wanywe damu, nani sijuwi anabaka watoto miaka 2 na mitatu, huyu sijuwi anavaa hirizi, yule sijuwi kavunja nazi na kuuwa paka, basi ni ujinga, upumbafu na ukatili kisa utajiri???!!!!
Tunasikitisha kwa kweli...
 
Huyo mkewe nae ana kesi ya kujibu,baada ya kutaka kushirikishwa katika hayo mauaji alitakiwa kutoa ripoti Polisi ili kunusuru hayo mauaji kabla hayajatokea,

Unamuua Mama yako kisa utajiri? Na huo utajiri angeupata angeutumia na nani wakati tunatambua kua Nani kama Mama,

Mama kakibeba kiumbe miezi 9 tumboni,kisha kikazaliwa,akakilea kwa mateso mpaka kikakua,masikini kumbe hakua anajua analea kiumbe kitakachokuja kuyaondoa maisha yake hapa Duniani!

Tuwe tunawaelimisha watoto wetu toka wakiwa wadogo ili waachane na hizi imani za kipumbavu.
It's real pain[emoji26][emoji26][emoji22][emoji22][emoji24][emoji24]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Huo utajiri inaonrkana ulikuwa unahitajika haraka sana ndio maana jamaa limeshindwa hata kufuata ushauri wa mke wake
 
Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Fredius Philibart Kibengo mkazi wa Omurushaka wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua mama yeke mzazi kwa kumkata shingoni kwa kutumia kitu chenye ncha kali baada ya mganga wa kienyeji kumtaka kupeleka damu ya mama yake au ndugu yake wa karibu ili kutengenezewa dawa za kuongeza utajiri kwenye biashara.

Katika uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera umebaini kuwa katika kipindi cha siku chache kabla ya tukio hilo kutokea mtuhumiwa alisafiri kuelekea nchini Burundi kutafuta dawa za kuongeza utajiri na aliporejea nyumbani kwake alimshirikisha mkewe kuhusu mashariti aliyopewa na waganga wa kienyeji lakini mke wake hakukubaliana na masharti hayo.

Hata hivyo Februari 17 mwaka huu mtuhumiwa alionekana maeneo ya nyumbani kwa mama yake mzazi na ilipofika usiku wa kuamkia Februari 18 alimvamia mama yake na kumkata na kitu chenye ncha kali kisha kupoteza maisha.

Hata hivyo kamanda Malimi amewataka wakazi wa mkoa wa Kagera kujiepusha na imani za kishirikina ambazo zimekuwa zikichangia mauaji ya wananchi wasio na hatia.

ITV

1 Timotheo 6:10 BHN​

"Kwa maana kupenda sana fedha ni chanzo cha uovu wote. Watu wengine wametamani sana kupata fedha hata wakatangatanga mbali na imani, na wameivunja mioyo yao kwa huzuni nyingi"
 
...
mtuhumiwa alisafiri kuelekea nchini Burundi kutafuta dawa za kuongeza utajiri na aliporejea nyumbani kwake alimshirikisha mkewe kuhusu mashariti aliyopewa na waganga wa kienyeji lakini mke wake hakukubaliana na masharti hayo.

Hata hivyo Februari 17 mwaka huu mtuhumiwa alionekana maeneo ya nyumbani kwa mama yake mzazi na ilipofika usiku wa kuamkia Februari 18 alimvamia mama yake na kumkata na kitu chenye ncha kali kisha kupoteza maisha.
Tulishauri itengenezwe database kwaajili ya kupima akili za watanzania wote (kuanzia viongozi mpaka raia wa mwisho) ili iwe rahisi kuepusha matukio ya namna hii lakini wazo halikutiliwa maanani
 
Pwani hadi Zanzibar huko si ndo mto katoka falme za kiarabu kuja kununua jini na kitita cha sh milioni 150? Unadhani huyo jini anakunywa mbege?
huki hawaui sheikh.... utakuta tu mtu anaishi na jini lake ndani ila huwez kusikia kamuua ndugu/mama kisa utajiri hayo mambo mnayo nyie huko nyikani
 
Back
Top Bottom