Kitu umefanikiwa katika huu uzi ni kuonesha kuwafahamu vema watanzania ambao ndio walengwa wako. Kwamba ukipangilia maneno yako vizuri wanakubaliana na wewe hata pasipo ushahidi wa kutosha wa kutetea hoja zako.
Sasa ndugu nikuulize, huko Bukoba hakuna jema?
Ni mkoa gani hakuna ubaya?
Yaani mkoa upi una wema tu na hauna ubaya wowote, bali ubaya ulijikusanya ukashamiri mkoa wa Kagera tu!!?
Suala la kujengeka mji wa Bukoba, uliambiwa ni wahaya tu ndio maafisa katika ofisi zote za manispaa ya Bukoba?! Kwamba maamuzi ya kiutendaji ambayo yanapaswa kuubadili mji ni ya wahaya tu? Hakuna makabila mengine kwenye ofisi hizo za manispaa au mkoani?
Je ni mji gani haswaa umejengeka katika nchi hii? Kwa akili yako Dar imejengeka? Yaani akija mgeni kutoka nje kisha akarudi kwao ataseme Dar ni jiji la kisasa? Huoni kwamba ndiyo sasa miundo mbinu yake haswa barabara ndio zinaboreshwa? Kama Dar mji wenye hadhi ya kitaifa uko hivyo sembuse Bukoba!?
Hujui kuwa mji mpya ni rahisi kujengeka kirahisi na kwa mpangilio mzuri kuliko miji mikongwe?! Kulinganisha Bukoba na miji inayochipukia ni kutokuelewa mambo.
Hivi ni kwa nini watu wanawapinga wahaya kuzungumza kihaya, si ni lugha yao!! Na kwa nini wewe huzingumzi lugha yako!? Unaionea aibu kisha unawaponda wanaojivunia lugha yao ya asili? Kweli!?
Kwa nini wageni wakija Tanzania wanakuta tunajivunia kiswahili? Je mzungu au mchina akikuta tunazungumza kiswahili mahali fulani huwa tunaendelea kutumia lugha yetu hii au inatubidi kubadili na kuzungumza kiingereza ili tuendane nao hata kama tunayoyazungumza hayawahusu...!! Why kihaya tu ndio kinawakera!?
Maswali ni mengi kuliko majibu! Why always wahaya...?
Mlaturugao norunwanwa...!