Socio cultural difference. Labda na wewe ungesema ni mtu wa wapi na mambo yako ni yapi hasa ili tuone nini ilisababisha hayo yaliyokukuta.
Kikubwa ni ku embrace difference zetu na kuendana na mambo. Hizo tabia Tanzania sehemu nyingi zipo zinatofautiana ujazo tu. Kwa maeneo ya mikoa ambayo ni ya mjini inapungua, kwa maeneo ambayo ni ya mipakani na kuna kabila moja la asili lime dominate hayo mambo yanakuwa mengi zaidi.
Mara ya kwanza natembelea Bukoba, japo sikukaa sana lakini nilienda hadi maeneo ya ndani ndani kama vile kata ya Rubafu nikaishi nao fresh tu.
Mambo mengine ni uoga wa asili wa wazawa. Hata Pwani ukiend deepkuna namna watu wanagwaya mgeni ukiingia na kuanza mambo kama ya kutafuta mashamba, biashara n.k
Ni kama hata kwa level ya taifa tunavyoogopa kutoa uraia pacha na kuwapa wageni haki au uhuru wa kununua ardhi n.k Lakini kuna watu kibao tu wamejenga na kununua ardhi kienyeji.
Kagera haiendelei iko vile vile miaka rudi miaka nenda. Mji umepangiliwa vibaya majumba yale yale yani hovyo hovyo tu.
Kuhusu watu kushindwa biashara sio kweli maana wachaga wamejaa tele ndiyo wenye mabaa na mapub na wenye biashara kubwa za kuuza pombe kama deport za bia.
Kuhusu nyumba, yes Bukoba mjini kuna nyumba za kupanga mbaya mbaya na nyumba nzuri chache kwa sababu wenye kujenga nyumba nzuri hawazipangishi wanajenga tu kwa sifa hata kama hawakai.
Kuhusu ardhi, sidhani kama ardhi ni gharama kama unavyosema. Hapo 5-10 km kutoka bukoba mjini lazima ardhi iwe ghali maana wenye nayo bado wanajiona wako mjini wakiwa wanahisi mji utapanuka pila ukienda vijijini huko mfano sehemu kama izimbwa, ibwera ardhi bei rahisi. Huko wasukuma wamewanunua wazawa karibu kunageuka kuwa usukumani na wazawa wamegeuzwa wafanya kazi kwenye mashamba waliowauzia wasukuma.
Huko utapata mashamba ya laki mbili ardhi ni plenty. Wasukuma wanalima mpunga huko.
Kuhusu customer care, hujakosea wahaya hawana customer care ni kama vile anayeuza ndiye boss unayenunua kijakazi.
Lugha, yes wahaya wanazungumza sana kihaya hadi ofisini, lakini sishangai hata wasukuma wako hivyo hivyo. Kuna kipindi nilishi kahama, ni kisukuma kwa kwenda mbele hata mtu hajafahamu kama wewe ni msukuma anaanza kukuongelesha kisukuma akigundua kuwa wewe si msukuma na switch na kuongea kiswahili. Kwangu haikuwa big deal.
Pia Kagera kuna mzunguko mdogo wa pesa. Halafu wahaya ukiondoa kilimo cha kuchanganya mazao shambani sijui kutokana na kulima migomba hawajaweza kufanya kilimo cha maana kama watu wa mbeya na Iringa. Nadhani hao wasukuma wa huko nilikokutajia watawafundisha kazi.
Hiyo customer care mbovu si kwamba wanafanyiwa wageni ndivyo walivyo anafanyiwa kila mtu ila wazawa wao wanaona kawaida tu maana wahaya na maringo hata kama hana kitu ni sawa na mzaramo na dera