Kagera: Mwalimu ampiga mpaka kuua mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyevunja mlango wa nyumba yake ili kuiba simu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Igurwa, Adrian Tinchwa (36) kwa tuhuma za kumuua, Phares Buberwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Igurwa.

Taarifa iliyotolewa jana Jumanne Septemba 24, 2024 na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Blasius Chatanda imesema mwalimu huyo ambaye ni mkazi wa Kata ya Kanoni wilayani Karagwe, inadaiwa alimshambulia marehemu kwa kumpiga ngumi kwenye paji la uso na kutumia nondo kumpiga nayo miguuni na mikononi baada ya kumtuhumu kuiba simu yake.

Soma pia: Mwalimu adaiwa kumpiga ngumi mwanafunzi na kumng'oa jino, eti Kisha kapata alama 29 za Hisabati

"Tukio hili lilitokea Septemba 18, 2024 saa 8:00 mchana katika kijiji cha Kanoni Wilaya ya Karagwe, ambapo mtuhumiwa awali mnamo tarehe hiyo saa 3 asubuhi, imedaiwa alifika nyumbani kwake na kukuta kufuli la mlango wa nyumba yake likiwa limevunjwa na alipotaka kuingia ndani alikutana na Phares Buberwa mlangoni akiwa anatoka ndani huku akijaribu kukimbia," amesema.

"Na ndipo mtuhumiwa alimkamata na kuanza kumshambulia hadi kusababisha kupata majeraha makubwa mwilini mwake na baadaye mtuhumiwa alimpeleka hadi nyumbani kwa wazazi wake na kumkabidhi kisha wazazi wake walimpeleka katika Kituo cha Afya cha Rwambaizi kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu," amesema Kamanda Chatanda.

Source: Mwananchi
 
Inabidi Polisi wasambazwe tena,
 
Kuua bila kukusudia.

Ukimchoma MTU kisu mara moja na akafa hiyo mahakamani wanasema umeua bila kukusudia.

Ila ukimchoma visu kuanzia viwili basi utahsabiwa umeua kwa makusudi.

Unapotaka kumuibia simu Mwalimu mwenye changamoto ya maisha ni ngumu kutoka salama.
 
Mstari wa mwisho ndio chanzo cha hasira ya huyo Mwalimu kujichukulia sheria mkononi,
Stress za maisha.
 
Back
Top Bottom