Kagera: Mwalimu ampiga mpaka kuua mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyevunja mlango wa nyumba yake ili kuiba simu

Kagera: Mwalimu ampiga mpaka kuua mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyevunja mlango wa nyumba yake ili kuiba simu

Sasa hapo ame ua mwanafunzi au ameua Mwizi?Huyo ni mwanafuzi mwizi alikuwa akimuibia Raia ambaye ni mwalimu.
 
Msichanganye madensa, Mwalimu hajaua mwanafunzi wake. Ticha anafundisha msingi wakati marehemu alikuwa sekondry kidato cha tatu. Isipokuwa majina ya shule yanafanana ni kama vile ilivyo Orsterbay primary na Orsterbay sec Dsm.
 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Igurwa, Adrian Tinchwa (36) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua Phares Buberwa mwananfunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari Igurwa

Inadaiwa Mwalimu Adrian alifika nyumbani kwake na kukuta kufuli la mlango wa nyumba yake limevunjwa

Alipoingia ndani alikutana na Mwanafunzi Phares akijaribu kukimbia kisha kumkamata na kumshambulia kwa kumpiga ngumi pamoja na nondo

Phares alipelekwa nyumbani kwao na baadae kupelekwa Kituo cha Afya cha Rwambaizi kwa ajili ya matibabu ambapo alipofariki dunia

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Blasius Chatanda tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024 katika kijiji cha Kanoni Wilaya ya Karagwe saa 8:00 mchana

Kamanda Blasius amedai chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa kujichukulia sheria mkononi na kutoa adhabu iliyopitiliza kwa marehemu hadi kufikia hatua ya kukimbizwa kituo cha afya kwa ajili ya matibabu
 
Usije ukajiroga kumpiga mwizi peke yako ukamuua. Uwezekano wa kwenda jela ni asilimia 90.

Kuna Wananchi wenye hasira kali, hakuna Mwananchi mwenye hasira kali.
Mzee mimi naua kikubwa mahakani nitashitakiwa na jamuhuri kwenye utetezi wangu nitasema nilikuwa najihami maana alikuwa na silaha
 
Back
Top Bottom