Kagera: Mwalimu ampiga mpaka kuua mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyevunja mlango wa nyumba yake ili kuiba simu

Hio kesi ni kujichukulia sheria mikononi, hata hivyo bado ni maelezo mwalimu, na huyo marehemu ni mtuhumiwa kwa maana hii habari haijathibitishwa..

Ma doctor wakifanya uchunguzi wataeleza kama alipigwa nondo kichwani au kifuani n.k
Hujaelewa swali au hujui tofauti kati ya kuua na kuua bila kukusudia?
 
Sure kwanza huyo dogo kwanini avunje kufuri.
Hapo mwalimu hana kesi.
Sio rahisi hivyo unavyodhani. Hapo mwalimu ana kama miaka mitano ya kukaa mahabusu kesi ikisikilizwa... uchunguzi wa kesi za mauaji huchukua muda. Baada ya hapo anaweza kuhukumiwa kunyongwa mpaka kufa ambapo hatanyongwa na kuishia kukaa magereza kwa miaka mingi. Ikitokea katoka kwa msamaha wa Rais ni baada ya miaka mingi. Lakini labda pia tumsikilize Mpwayungu Village anaweza kuwa na maoni tofauti
 
Hayo maelezo ameyetoa Mwalimu? Maana hapo ndani si walikuw Mwalimu na huyo "Mwizi"? Sasa hizo "chumvi na Binzari" nyingine zinatokea wapi?
Kwani mada imekujaje!?
Mie nimeeleza kulingana na mada ilivyoletwa na maelezo yalivyokuja.
 


Yes Kama Hana pesa ya kutoa hii kesi itamsumbua

Upelelezi wa kesi ya mauaji huchukua 2-5yrs yaani ni hatari Sana


Murder case sio mchezo
 
Hata vibaka wa Tandale wanapigwa na kuuawa
 
Yes Kama Hana pesa ya kutoa hii kesi itamsumbua

Upelelezi wa kesi ya mauaji huchukua 2-5yrs yaani ni hatari Sana


Murder case sio mchezo
Mwalimu kashaharibu mwelekeo mzima wa maisha yake.... nashindwa kuelewa ni hasira za kiasi gani hadi kuchukua nondo kumpiga mtu ambaye tayari umeshamdhibiti tena mwanafunzi? Waalimu wengi wana shida kisaikolojia.
 
Mwalimu kashaharibu mwelekeo mzima wa maisha yake.... nashindwa kuelewa ni hasira za kiasi gani hadi kuchukua nondo kumpiga mtu ambaye tayari umeshamdhibiti tena mwanafunzi? Waalimu wengi wana shida kisaikolojia.


Yes hawapo vzr mentally nafikiri pia maisha yanachangia
 
Tuna uhakika gani kuwa mwanafunzi alienda kuiba simu au mwalimu alimdhulumu na kumfanyia kitu mbaya alafu akampatia kipigo cha mbwa mwizi? Marehemu hawezi kujitetea!
 
Hiyo ni kuua bila kukusudia akipata wakili mzuri kesi nyepesi hiyo
kati ya daktari na mwalimu nani aliyeua? mtu kafia mikononi mwa daktari, mwalimu alimfikisha kwa wazazi wake mzima, wazazi ndio waliompeleka kwa daktari. mie naona chanzo za kifo ni kukosa huduma stahiki za afya na si kipigo cha mwalimu
 
Ukubali kuibiwa simu ya laki tatu au unende jela maisha?
Mwalimu: laki tatu ni mahahara wangu wote, ntaenda jela.


Sasa kakosa simu, na maisha
Inasikitisha sana
 
Una nunua simu kwa Mkopo, kwa kujibana.
Halafu kuna mtu mmoja, anakuja kuichukua kama yake.
 
Wasiseme mwanafunzi Huyo alikuwa mwizi kama wezi wengine,Hata ningekuwa Mimi nakumfuma MTU ndani kwangu siwezi kucheka naye,nitafanya lolote Kwa kadri nitakavyojaliwa.Kaua mwizi bila kukusudia .
 
Unazifafahamu tofauti kati ya *kuua na *kuua bila kukusudia?
Ndio.

Huwezi kumpiga mwanafunzi, ukaona kana kwamba haitoshi, ukachukua nondo na kumgonga hadi kumuua, halafu useme eti umeua bila kukusudia.

Hiyo mahakama labda itakuwa ni ya baba yako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…