Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nilitegemea sana Yanga leo kucheza chini ya kiwango na hilo limeonekana dhahiri shahiri wachezaji wamechoka sana ratiba ya ovyo ovyo hii sijawai kuona, Pamoja na yote wachezaji wamecheza kikubwa na kushinda kikubwa cha muhimu leo ilikuwa ni point 3 na zimepatikana ashukuriwe Mungu.
Pongezi sana kwa kipa makini Djigui Diara ameonyesha thamani yake iliyomfanya alipiwe tiket ya ndege kutoka Mali kutua Tanzania ni bonge la kipa, Timu inayocheza kibingwa ata ikicheza vibaya lazima iweke mpira kambani na kuondoka na point 3 muhimu