Yanga wamepambana sana ila Madaktari na watu wa physical wa Yanga wafanye kitu, Miili ya wachezaji baada ya hii mechi itakua na Hali mbaya sana.
Maji, matope uwanjani na uchovu unaweza leta injury nyingi au Homa Kali Kwa wachezaji.
Wasichukulie poa, tumepata point 3 lakini Miili ya wachezaji kesho itakua imevunda vibaya Kwa baadhi ya wachezaji hasa waliocheza kule Tunis.
Leo baada ya mechi wasiwatie kwenye barafu, wapige massage tu.
Enzi sisi tunacheza ikitokea mmecheza mechi mfululizo Kwa kipindi kifupi tulikua tukimeza dawa za kutuliza maumivu wakati wa warm-up katika mechi husika ya muda uo ilisaidia kuondoa uchovu, kwasasa nafikiri Wana njia Bora zaidi ki Afya.