Kagera: Watuhumiwa tisa wa mauaji ya Asimwe Novart wafikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la kuua kwa kukusudia

Halafu kuna Wanaharakati uchwara utawasikia wanasema "Hukumu ya kifo iondolewe, maana ni uvunjaji wa haki za binadamu." Pumbavu zao, kwani Muuaji yeye alipokuwa anajua alikuwa hajui anamvunjia mwingine haki yake ya kuishi.

Mimi ningekuwa Rais ningesinya mapema sana saini yangu kwenye hukumu ya mauaji ya huyo mtoto. Mbona Rais wa China anasaini fresh tu.
wanaharakati kazi yao kubwwa kuangalia makonda kmbananisha nani kala hela ya umma ndiyo utawasikia kwenye mambo nyeti kimyaaaaa pumbavu zao
 
Natamani sana kujua ukweli, uhakika na uhalisia juu ya tukio Hilo lote kabisa, sema tatizo ni kwamba Sheria za nchi hii ya Tanzania haziruhusu Independent Police Investigation, na kwa bahati mbaya sana kupita kiasi ni kwamba hata ripoti au taarifa za upelelezi za Jeshi la Polisi nazo haziaminiki kabisa. Hivyo, huenda tunaweza tusiujue ukweli halisi kuhusiana na tukio hili.
Kabisa kabisa. Nakubali. Cases kama hizi unaweza kukuta mambo yako tofauti kabisa.
 
Kwanini hili suala la watuhumiwa kupelekwa mahakamani nakurudishwa bila ya kesi kusikilizwa,linajirudia?
Inamaana bado suala la kujua mahakama ipi ni sahihi au si sahihi,kwa kuwapeleka watuhumiwa wa kesi flani,halijawahi kutatuliwa?
Mambo ya kijingajinga sana haya.
Kama hujui sheria unaweza kudhani ni uzembe. Huu siyo uzembe bali ni matakwa ya kisheria.
 
Elpidius Alfred Rwegoshora miaka 49 ambaye ni padri..!! Yule padri nae yumo, Kanisa Katoliki lingefaa litoe tamko kali sana kulaani padri kuhusika katika huu uuaji, unyama na ukatili mbaya sana..!!
Kwa sasa bado ni tuhuma tu hazijathibitishwa. Kuna 1) kutuhumiwa na kuna 2) kukutwa (kuwa) na hatia - ni vitu viwili tofauti. Hata hivyo, askofu wake amemsimamisha kutoa huduma zozote za kiuchungaji hadi hapo itakapothibitika kwamba hakufanya hivyo anavyotuhumiwa na vyombo vinavyohusika.
 
Aisee nyuso zao zinaonyesha kusikitika na kujutia kosa lao...
 
Kanisa limetoa taarifa kumsimamisha kwa sasa hawawezi kusema lolote maana bado mtuhumiwa ....akija kuachiwa kuwa hana hatia ....? Tusikurupuke kumaliza maneno.....acha haki itendeke...mudavni mwalim mkuu

Kwanini ufikirie upande mmoja tu kuwa huenda hatakutwa na hatia? Hadi hapo kitendo cha padri kuwa mtuhumiwa tayari ni fedheha, aibu na kanisa limechafuka sana sanaaaa, kukutwa na hatia ni kitu cha mbeleni, hapo ilipofikia, tayari ni doa baya sana kwa kanisa Katoliki..!!
 
Aisee nyuso zao zinaonyesha kusikitika na kujutia kosa lao...
Sasa zitaonyeshaje kusikitika na kujutia kosa lao wakati hujui kama ni wao waliotenda kosa au ulishuhudia wakitenda kosa? Mimi kwa mambo haya huwa ninakuwa na subira maana inaweza kutokea wakosoaji wakawa watu wengine kabisa. Sasa kama unakuwa umeshamhukumu mtu, halafu baadaye ukakuta siyo huyo uliyemhukumu, mimi huwa inanipa tabu sana moyoni mwangu maana na mimi sitaki nihukumiwe vibaya. Hivyo, huwa najitahidi kuwa mwangalifu.
 
Elpidius Alfred Rwegoshora miaka 49 ambaye ni padri..!! Yule padri nae yumo, Kanisa Katoliki lingefaa litoe tamko kali sana kulaani padri kuhusika katika huu uuaji, unyama na ukatili mbaya sana..!!
Limeshatoa!
Mshahara wa dhambi ni mauti - mauti yao yametimia.
Nahisi washirika wao wengine, naamini watakuwepo, watakuwa wameshakimbia nchi
 
Sasa zitaonyeshaje kusikitika na kujutia kosa lao wakati hujui kama ni wao waliotenda kosa au ulishuhudia wakitenda kosa? Mimi kwa mambo haya huwa ninakuwa na subira maana inaweza kutokea wakosoaji wakawa watu wengine kabisa. Sasa kama unakuwa umeshamhukumu mtu, halafu baadaye ukakuta siyo huyo uliyemhukumu, mimi huwa inanipa tabu sana moyoni mwangu maana na mimi sitaki nihukumiwe vibaya. Hivyo, huwa najitahidi kuwa mwangalifu.
Kwa hiyo ulitaka wasikamatwe mkuu mbona haueleweki hizi kesi za mauaji ya watoto wenye ulemavu mara nyingi zinahusisha familia na mara chache sana toka nimeanza kuzisikia ikaja taarifa kuwa sio wao labda wewe unikumbushe na pia Tanzania kwenye mambo ya kutafuta taarifa za wauaji Polisi wanajitahidi mno mno kuliko sehemu nyingi ninazoishi hao jamaa nawapa Big up....
Watu wamekutwa na baadhi ya viungo na wametajana wewe unasema tusubiri nini ina maana hivyo viungo Polisi walienda navyo kuwakamata ni vile Tanzania tuna hizi mambo hiyo ishu China hata wiki haifiki yaani hawapewi hata nafasi ya kuvuta sigara wanaliwa Vichwa uone kama utasikia tena hizo mambo tena hadharani kwenye Kijiji walichofanya hayo mambo..
 
Mimi nasema sheria za nchi zinavyosema/elekeza. Wewe unasema unavyodhani ndivyo ilivyo. Ni vitu viwili tofauti. Hebu dondoa sehemu niliyosema "wasikamatwe". Kwani hizo sheria nimezitunga mimi? Soma vizuri nilivyochangia uelewe mantiki ya mchango wangu.
 
Back
Top Bottom