Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kang, na mnaomtetea RA. Nadhani kumbukumbu zenu ni fupi kuhusu sakata la Richmond na kuhusishwa kwa RA. Tafadhali jikumbusheni. Nadhani ilikuwa nafasi nzuri sana kwa RA kutumia mkutano wake na waandishi wa habari kujibu tena na kwa ufasaha zaidi hoja nzito za Kamati ya Mwakyembe. Kwa vielelezo. Hakufanya hivyo unadahni hajui nini alitakiwa kufanya... Anajua, ila amechagua kutokuwa muwazi. Kamati ya bunge haikuwa na madaraka yeyote ya kumuwajiisha na serikali haikotayari... Maranyingi sana pamekuwa na maombi ya kujitokeza wenye ushahidi. ..maana yake upo mahali...
Bado mnatupotezea wakati. Rostam aliitisha mkutano kujibu shutuma za Mengi na si za Mwakyembe. Zaidi ya hapo alitoa nafasi kwa waliokuwepo kumuuliza maswali. Kwa nini hao wasiulizie shutuma za Mwakyembe? Aliulizwa ya Kagoda, akajibu kuwa hahusiki. Sasa kama muulizaji alikuwa na ushahidi wa kuhusika kwake si angeuweka wazi. Ameulizwa ya Dowan, akakana kuwa anahusika kibiashara. Mwenye ushahidi wa uongo wake kwa nini asimburure mahakamani. Amesema wazi kuwa anawafahamiana na wenye Dowans lakini si kibiashara. Sasa mnataka awaeleze undani wa mahusiano yake nao! Wangapi humu tunafahamiana na watu waliokuja kugundulikana kuwa ni wahalifu. Wengine wetu, ndugu zetu wako ndani kwa ajili ya vitendo vyao viovu. Kwa hiyo na sisi basi tumekuwa waovu kwa sababu tunafahamianan nao?
Ninarudia tena. Kama kuna mtu ana ushahidi, a call Rostam's bluff na ampeleke mahakamani. Atatusaidia wengi. Nje ya hapo tunapotezeana wakati.
Hatuwezi kumlaumu Rostam kama mwenye ushahidi hataki kujitokeza.
Amandla.........