Kagoda: Ni Rostam


Bado mnatupotezea wakati. Rostam aliitisha mkutano kujibu shutuma za Mengi na si za Mwakyembe. Zaidi ya hapo alitoa nafasi kwa waliokuwepo kumuuliza maswali. Kwa nini hao wasiulizie shutuma za Mwakyembe? Aliulizwa ya Kagoda, akajibu kuwa hahusiki. Sasa kama muulizaji alikuwa na ushahidi wa kuhusika kwake si angeuweka wazi. Ameulizwa ya Dowan, akakana kuwa anahusika kibiashara. Mwenye ushahidi wa uongo wake kwa nini asimburure mahakamani. Amesema wazi kuwa anawafahamiana na wenye Dowans lakini si kibiashara. Sasa mnataka awaeleze undani wa mahusiano yake nao! Wangapi humu tunafahamiana na watu waliokuja kugundulikana kuwa ni wahalifu. Wengine wetu, ndugu zetu wako ndani kwa ajili ya vitendo vyao viovu. Kwa hiyo na sisi basi tumekuwa waovu kwa sababu tunafahamianan nao?

Ninarudia tena. Kama kuna mtu ana ushahidi, a call Rostam's bluff na ampeleke mahakamani. Atatusaidia wengi. Nje ya hapo tunapotezeana wakati.

Hatuwezi kumlaumu Rostam kama mwenye ushahidi hataki kujitokeza.

Amandla.........
 

RA anatuhumiwa kumweka Rais na viongozi kibao serikalini kwenye nafasi zao. Katika mazingira haya, DPP si rahisi kufanya kazi yake kumfikisha RA mahakamani na kumfungulia mashitaka.

Anachofanya RM na wapiganaji wengine ni kumshtaki RA kwenye "court of public opinion". Kama kadamnasi itaridhika kwamba RA ni adui wa taifa, basi hukumu watakayotoa ni kubwa kuliko ya mahakama yoyote hapa nchini. RA hatoweza kuonesha uso wake hadharani.

Hapa ndo vita dhidi ya ufisadi ilipofikia. Bado haijafanikiwa, lakini tutafika tu.
 

Humu humu, Mkuu Mwanakijiji ametuelimisha kuwa HAKUNA mwenye nguvu juu ya DPP! sasa mwenzetu unataka kusema Rostam amemweka ribit! Iko kazi.

Amandla......
 
Humu humu, Mkuu Mwanakijiji ametuelimisha kuwa HAKUNA mwenye nguvu juu ya DPP! sasa mwenzetu unataka kusema Rostam amemweka ribit! Iko kazi.

Amandla......

Theoretically yes. Practicaly....................

Husikii hata Jaji Mkuu analalamika bunge na dola vinaingilia kazi yake?
 
Kinachotakiwa ni mtu mwenye ushahidi, mwenye uchungu na nchi hii, kusimama na kuziweka wazi allegations hizo na ushahidi wake. Bahati mbaya, Mengi si mtu huyo!

Amandla.......

Kwa bahati mbaya mpaka hivi sasa hakuna mwenye ushahidi wa Rostam kuhusiana na hizo tuhuma nyingi anazorushiwa. Yote yanayoongelewa kuhusu yeye ni Folklore!

Sasa inawezekana kweli Rostam ni fisadi au inawezekana wala siyo fisadi ila hatuwezi kutumia maneno matupu ya watu kuwa ndio ushahidi dhidi yake.
 
ona sasa huyu nae anaandika makala ndefuuuuuuu, zinalalia upande mmoja,
pale alikuwa (rostam)anajibu tuhuma ulitaka ajizungumzie yeye tena?
mi nishasema nchii hii wajinga wengi wanajifanya wajuaji bure!
umeniudhi sana ila asante kwa kupoteza mda wako
 
THANK YOU BUBU ATAKA KUSEMA.

REGINALD MENGI FEDHA ZAKE NA VIWANDA VYAKE VINAINUA UCHUMI WA TANZANIA. AMEAJIRI WATANZANIA WENGI SANA. NA HAO WALIOAJIRIWA WANAE XTENDED FAMILIES.
SASA CASPIAN AKA RICHMOND AKA DOWANS WAO WANAKWAPUA FEDHA ZA KODI YA WATANZANIA WANAWEKEZA NJE YA NCHI.

HATA KAMA MENGI ALIKOPA NBC, si amewekeza TANZANIA? Si analipa kodi? Si ameajiri watanzania? SI anatoa huduma kwa jamii?
 
ona sasa huyu nae anaandika makala ndefuuuuuuu, zinalalia upande mmoja,
pale alikuwa (rostam)anajibu tuhuma ulitaka ajizungumzie yeye tena?
mi nishasema nchii hii wajinga wengi wanajifanya wajuaji bure!
umeniudhi sana ila asante kwa kupoteza mda wako

Wewe unadhani ndo hujaudhi wengine?

Alijibu tuhuma ama alikuja kutuhumu kwa akili yake pungufu akidhani kwamba akituhumu itaosha tuhuma zake?

Tuhuma ziko pale pale.. hata huko Takukuru aliko kimbilia hakuwezi kumsafisha, he has to face it this time! 40 yake ndo inakaribia hiyooo.
 


Duh michango mingine jamani... On the same line of reasoning Benki M, Mchuchuma, Dowans et al si zinatoa ajira kwa extended family za wabongo je tuzisafishe kutokana na ufisadi?
 
Humu humu, Mkuu Mwanakijiji ametuelimisha kuwa HAKUNA mwenye nguvu juu ya DPP! sasa mwenzetu unataka kusema Rostam amemweka ribit! Iko kazi.

Amandla......

Na baada ya kutuelimisha juu ya nguvu za ajabu za huyu DPP anaendelea kusema kwamba watuhumiwa wakubwa wa ufisadi hawajachunguzwa wala kufikishwa mahakamani licha ya ushahidi kutolewa kwenye vyanzo mbalimbali

Anaconclude kwamba DPP ni muoga na mzembe sana.

We unaonaje ukweli wa analysis ya Mwanakijiji?
 

I really hope readers of this absolute juvenille and illiterate tirade published by the editor of 'This Day' today are not stupid and treat this with the distain it deserves. What on earth is all this doing to the reputation of Tanzania???

Rostam need not defend himself, the law presumes him innocent of the allegations. It is for Mengi to prove them and so far, he is not the one handing over any evidence to the PCCB !!!
 
Ragamuffin,kazi nzuri! I think Rostam must reciprocate by rewarding you handsomely.
 

Wewe kama unaacha acha.

Hakuna mtu anashabikia nani kasema nini, tunajadili hoja zilizo tolewa.

Hapa kuna watu wa kila aina wengine ni wakali wa Hesabu lakini socially ni wafu.
Wengine income zao zinatokana na uwezo wao wa kujipendekeza na kujikomba wengine huongeza bidii na juhudi katika kazi zao ili wafanikiwe.
Wengine wametumwa na kuja kutanda mawingu hapa JF na Unene wa pochi kwenye malipo yao ya mezani unategemea Post zao ziliwatibua wana JF kiasi gani, wkati wengine wapo hapa kujifunza na kunoa uelewa wao.

Kwa hiyo neno kushabikia lina ukweli kwa baadhi ya makundi ya watu hapa JF, si neno linalojumuisha watu wote katika hoja zao.
 

Why should he hand this evidence to PCCB?
 

As if PCCB have done anything worth to show off!!!! Unakumbuka Mengi walirushiana maneno na Hosea Edwards kuhusu utendaji wake finyu kama mkuu wa PCCB sasa huyo huyo ambaye kazi imemshinda apelekewe ushahidi. PCCB ni UPUUZI MTUPU! ni kimbilio la mapapa mafisadi.
 
Kama alivyouliza Rostam mwenyewe, " aende mahakamani kufanya nini?"

Amburuze Mengi mahakamani na amfungulie kesi ya kuchafuliwa jina kwa kuitwa fisadi papa wakati siyo kweli na ndivyo inavyotakiwa kufanyika. Kutokuwa tayari kufanya hivyo ni dalili ya kuogopa kuumbuliwa.

Mnataka aende mahakamani kujishtaki kuwa yeye si fisadi? Hamuoni tuu kuwa jambo hilo haliwezekani?

Ala kumbe, hakufanya hivyo kwa kwa kuogopa kujishtaki - kweli hilo haliwezekani kwani ukweli usio na shaka ni kwamba Rostam ni fisadi wa kutupwa.

Alichofanya yeye ni kusema kuwa yeyote mwenye ushahidi wa ufisadi wake aende mahakamani kumshtaki! Kigugumizi sasa cha nini?

Tafadhali fundi Mchundo usiwe mvivu wa kufukiri - kwa kushindwa kufungua mashitaka dhidi ya Mengi na badala yake kumtuhumu Mengi, sasa mambo yanaenda huko huko alikoogopa. Mengi, baada ya Rostam kuingia mtegoni, amefungua kesi mahakamani kupitia kwa wanasheria wake.


Rostam aliogopa kwenda mahakamani, lakini hakusita kuwasilisha vielelezo vyake TAKURURU. Mengi, on the other hand, kufungua kesi mahakamani lakini wewe bado umemwandama Mengi, tukueleweje ? Moja Rostam bado anatafuta kubebwa serikalini wakati Mengi anatafuta haki mahakamani, je upo ?

Tusipende mno mteremko. Hatutawang'oa hao tunaowaita mafisadi papa kwa kuita press conference na kutoa general accussations. Tutoe specific allegations na kuzi-substantiate ndiyo kazi itaanza. Na si vinginevyo.

Na mafisadi papa nao hawataweza kujisafisha kwa kuita press conference na kukimbilia TAKURURU - ingekuwa rahisi namna hiyo Richomnd ingekuwa safi kama theluji. Sasa twasubiri TAKURURU imfungulie mashtaka Mengi kwa niaba ya Rostam wakati huko mahakamani kesi nyingine inaendelea - Mengi dhidi ya Rostam.

Amandla...

Rostam alitaka kuikwepa mahakama lakini kwa vyovyote vile kila kitu kinaonekana kitaishia mahakamani - sasa sijui wengine mnatakaje. Rostam alililia wembe na yaonekana akapewa, je atapona kukatwa ? Ninaowahurumia ni vikaragosi wanaocheza ngoma wasioijua na wala hawana habari na sehemu wanapokanyaga.
 
Mag3,

Una ni-disappoint Mkuu. Hiyo kesi aliyoifungua Mengi dhidi ya Rostam inahusu vipi shutuma zake juu ya ufisadi wa Rostam? Yeye pengine ameenda (kama kafungua kweli) kulalamikia kukashifiwa na si masuala ya Kagoda. Rostam kupeleka vielelezo vyake Takukuru hakumzuii kufungua kesi dhidi ya Mengi. Au kuomba kuunganishwa katika kesi ambayo Manji ameishafungua dhidi ya Mengi.

Huyo Mengi mnaemshabikia amekuwa makini katika kutokumhusisha Rostam na shutuma zozote za ufisadi papa zaidi ya kumuita fisadi papa. Kama kweli ana ushahidi wa huo ufisadi papa wa Rostam kwa nini asiseme tu kuwa Mheshimiwa Rostam amehusika hapa na hapa katika kuhujumu uchumi wa nchi yetu? Kigugumizi cha nini? Ati anangoja hadi apelekwe mahakamani ndiko akatoe ushahidi huo wakati akijitetea. Umemshika mwizi, halafu unadai hadharani kuwa unahisi umeibiwa na fulani! Jamaa anapouchuna, unalalamika kwa watu ati kwa nini hajaenda mahakamani kukushtaki ili utoe ushahidi kuwa amekuibia! Ebo! Are we really serious?

Rostam lazima alijua kuwa Mengi ataenda mahakamani. Na anajua mashtaka ya Mengi hayatamnyima usingizi maana yatakuwa ni ya kulalamika kuharibiwa jina tu. Mashabiki mtaachwa tena kwenye mataa.

Mimi sisemi kuwa Rostam ni msafi. Ninachosema ni kuwa kwa mwendo huu hatufiki popote. Mwenye ushahidi dhidi ya Rostam akafungue mashtaka dhidi yake badala ya huu mchezo wa kitoto. Huyo ndiyo kweli atakuwa shujaa, Si huyu Johnny-come- lately Mengi!

Amandla.....
 

Wapi aliposema DPP ni muoga na mzembe sana?
 

a. Mtu anapotoa tuhuma ni nani kisheria ana jukumu la kukusanya ushahidi, kuuchambua na kuona kama ni relevant kwenye kesi?

b. Mengi hajasema ameibiwa na Rostam au kwamba Rostama amemdhulumu kwenye jambo fulani binafsi, kazungumzia kitu kinaitwa "taifa". Sasa serikali inaweza kuja na kusema kuwa serikali haijabiwa kwa hiyo the allegations kuwa kuna mwizi are baseless and unfounded. Serikali inaweza kumaliza.

c. Kama serikali inajua kuwa kuna wizi umetokea na kuna watu wanatajwa kuhusika na wizi huo, ni jukumu la serikali kufanya uchunguzi na kuamua siyo kukaa pembeni na kusema mwenye ushahidi wa wizi atuletee!?

d. Mfano mzuri ni kesi za EPA majina yaliyotajwa na madai yaliyotolewa ya EPA yameandikwa mara nyingi na watu kadhaa walitajwa. Hakuna mahali serikali ilisema kina Slaa walete ushahidi ili uchunguzi ufanyike, waliangalia uzito wa tuhuma na vidokezo vya ukweli wa tuhuma hizo (tarehe, akaunti namba, majina ya watu n.k). Ni serikali ikaamua kuunda Tume ya Mwanyika kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo na ni wao ndio walioenda kukusanya ushahidi wa tuhuma hizo na ni wao waliowafikisha mahakamani. Dr. Slaa wala wengine waliotoa tuhuma hizo hawajatajwa kuwa ni mashahidi!

Kwanini linapokuja la Rostam tunataka Mengi ndiyo alete ushahidi wakati tunayo precedence ya jinsi gani tuhuma kama hizi zimeshughulikiwa na serikali?

e. Kama Mengi amedai kuwa yeye ndiyo kaibiwa (binafsi) au kampuni yake basi ni wazi kuwa ni vizuri kuwapa Polisi mahali pa kuanzia (waoneshe nyumba iliyoibiwa, kilichoibwa, n.k). In this case, it is not personal or is it?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…