Kagoda: Ni Rostam

Kagoda: Ni Rostam

CCM...Just take the back seat, be patient , watch and stay calm when the whole thing is being worked out.

Kubabaika ni body language kuwa .... All is not certain and hamjiamini.

Mtizamo huo utatufanya tujiulize na kufutilia kwa karabu na kwa undani wenye makini makubwa... Kwani nyie ndio mnatusababisha kufanya hivyo.

Au Mnafucha jambo nini?
 
Chiligati atasemaje kuwa kama ni wana ccm wenye Kagoda, walichota hizo fedha kivyaovyao wakati wanachama hao ndio walionunua VX Land crusers muungwana alizokuwa anatumia kuzunguka nchi nzima kuomba kura!! Mpaka sasa Chiligati na genge lake hawajaweza kuwathibitishia wananchi kuwa yale magari ya MAHINDRA toka India yaliyosambazwa nchi nzima mwaka 2005 yalinunuliwa na chama chao na sio kwa kutumia peza za wizi toka BOT!! Onyesheni payment vouchers kama kweli chama chenu ni kisafi.
 
Mpaka sasa Chiligati na genge lake hawajaweza kuwathibitishia wananchi kuwa yale magari ya MAHINDRA toka India yaliyosambazwa nchi nzima mwaka 2005 yalinunuliwa na chama chao na sio kwa kutumia peza za wizi toka BOT!! Onyesheni payment vouchers kama kweli chama chenu ni kisafi.

- Mkuu umechanganya ishus hapo, kuna makosa ya viongozi individually, na ya chama CCM.

- Mahesabu ya vyama vyote vya siasa hufanywa na Msajili wa vyama na yameshafanyika, wewe unaongelea hela zilizoongezwa huko individually, kusaidia CCM , that has nothing to do na CCM as chama cha siasa.

However, bado haya maneno ya Chiligati ni very low minded kutolewa na kiongozi wa level yake ya national level.
 
Mahesabu ya vyama vyote vya siasa hufanywa na Msajili wa vyama na yameshafanyika, wewe unaongelea hela zilizoongezwa huko individually, kusaidia CCM , that has nothing to do na CCM as chama cha siasa.
[/SIZE]

Hesima mbele mkuu.
Naomba tupanue kidogo huu mjadala kuhuisiana na hizi fedha zinazodaiwa kupelekwa CCM kwa ajili ya kampeni.
Kwa mtazamo wangu, hata kama aliyepeleka alikuwa individual, alifanya hivyo kwa lengo la kusaidia kitu fulani-na kitu hicho (kulingana na wakati) ilikuwa ni uchaguzi. Tunajua kuwa ili mtu achaguliwe, anahitaji kuwa nomibnated na chama. nadhani hapo ndipo CCM inapounganika na fedha hizo kwa sababu zililetwa na individual kwa ajili ya mgombea/wagombea wa CCM.
Au, unataka kutueleza kuwa fedha hizo zilizoingizwa na individual zilitumika individually? yaani zilipelekwa ofisi za Mindu badala ya Lumumba?
 
CCM hawana pakutokea na hili sakata la Kagoda. Wanajaribu kila njia kulikimbia lakini kila wanakokimbilia Kagoda ipo tu na 2010 ndiyo inanyemelea taratibu. Wana kazi kubwa sana ya kutafuta njia za kutuzuga Watanzania, lakini safari hii hatupo tayari kuzugika.
 
Hivi tukianza kuwekeana mipaka, hiyo demokrasi itakuwa na maana yeyote? Tukifika mahali pa kuambiwa kipi kinastahili kujadiliwa na kipi hapana, bado tutakuwa na haki ya kujiita demokrasi? Inapofika mahali ambapo sehemu moja ya jamii inaona ina haki ya kuweka mipaka ya discourse katika public sphere, bado tutakuwa na haki ya kusema tuna demokrasia?
 
Wakati kina Mh.Chiligati wanalelewa na CCM, siasa zake zilikuwa zipi? nani Mwenyekiti? nk..nk. Hebu tulinganishe na sasa.Mh.B.W.M akiwa mwenyekiti wa CCM alisema nini kule Dodoma kuh."Chama kutekwa na Matajiri". Hali halisi sasa hivi ni ipi?
Bwana Chiligati asiubebe mzigo wa kutetea Kagoda.Hana ubavu
 
- Mkuu umechanganya ishus hapo, kuna makosa ya viongozi individually, na ya chama CCM.

- Mahesabu ya vyama vyote vya siasa hufanywa na Msajili wa vyama na yameshafanyika, wewe unaongelea hela zilizoongezwa huko individually, kusaidia CCM , that has nothing to do na CCM as chama cha siasa.

However, bado haya maneno ya Chiligati ni very low minded kutolewa na kiongozi wa level yake ya national level.
[/QUOTE]

Mkuu ni dhahiri unaelewa mambo yalivyokaa kushoto katika kipindi cha JK hasa kuanzia mambo ya list of shame yalipolipuka.Katika hali kama hii ni ngumu mtu kutofautisha kipi kilifanya na chama na kipi kilifanywa na mwanachama individually. Hapa nilitegemea toka kashfa ya EPA kuhusishwa na uchaguzi mkuu tayari mapema CCM ingeshakana kuhusika kwake. Kukaa kwake kimya ni dalili tosha kwamba walihusika.Pili, hata kama wizi ulifanywa individually je ulifanyika kwa faida ya nani? Na kama chama kilipokea kilipokea kikijua zinatoka wapi? Na huyo aliyeiba individually alitumwa na nani maana sijaona uzalendo wa namna hii wa mtu kuiba kwa faida ya chama.Ni lazima mtu huyu alitumwa na akahakikishiwa usalama wake na ndo maana kuna tetesi hawa wezi ni jeuri sana. Hapo inakuwa ngumu kusema kuwa CCM haihusiki.NI NGUMU MNO.
 
Wana JF sasa hivi tunaona kitu kama mfa maji. Kuna watu ndani ya CCM bado wana credibility kubwa machoni mwa watanzania, wana CCM ambao wanasaidia kutoa mwanga kwenye mapambano ya kuikomboa nchi. NI vyema wale ambao hawana credibility wakae kimya walau heshima yao iendelee kuwepo. Sasa hivi baadhi ya wanasiasa wanaogopa hata kuonekana mbele za watu kwa sababu tunafahamu wazi kuwa ni waongo, wanaokumbatia mafisadi na wasiowatakia watanzania maendeleo. Leo kuanza kuuambia umma wa Tanzania kuwa CCM haihusiki na Kagoda sijui lengo nini? ni kutufanya wajinga au ni kujifanya unajua zaidi kuliko wanachojua wengine. Huwezi kuutenganisha mkono kutoka kwenye kiwiliwili, connection kati ya CCM na Kagoda ipo, sasa naona mheshimiwa anataka aanze kuona evidence kama alizooneshwa Kingunge ili ajue kuwa anajiaibisha kwa kauli zake. Vizuri akikaa kimya tu.
 
"Chiligati alisema endapo kuna wanachama wa CCM ndani ya kampuni hiyo wanaotuhumiwa kuchota fedha kinyume cha sheria basi ifahamike kwamba watu hao watakuwa wametenda maovu hayo wao binafsi lakini siyo kwamba wametumwa na CCM. Alisema iwapo wanachama wa CCM wanaotuhumiwa kufanya vitendo vya wizi na ufisadi watabainika basi chama hicho kitawachukulia hatua kutokana na kuwa wamevunja maadili ya chama hicho."

Wanachama wa CCM walioshiriki kukwapua hela hizo Chiligati hawajui?

Chama nini? Chama ni jina tu au ni mkusanyiko wa wanachama wanaokiunda chama hicho?,Chama ni wanachama, sasa kama wanachama hao hao wameshiriki ukwapuzi wa pesa za watanzania, chama sisemu hakiwezi hepuka lawama.

Watoto wakiiba mahindi kwenye shamba la kijiji japo si wote kwenye familia, yakaletwa nyumbani yakaliwa na kutatua njaa ya familia, kama baba na mama watashiriki kuyala pasipo kuhoji yalipopatikana mahindi huku wakijua hawana shamba, basi na wao wameshiriki. Ni tatizo la familia nzima!

Wakwapuzi wa pesa za Kagoda ni wana CCM, wamezileta CCM, zikatumiwa na familia nzima huku viongozi wa familia wakikaa kimya pasipo kuhoji chanzo cha pesa hizo.

Wana Jf nielewesheni, hivi DDP hakitetemeka na kusita kuwafikisha wahusika mahakamani na kwa mashitaka husika, hakuna utaratibu wa waendesha mashitaka binafsi kufungua mashita na kuendesha kesi hizo mahakamani, Kama ilivyokuwa kwenye kesi dhidi ya Rais Clinton/Monica L? Hapa hatuwezi? Kesi za EPA/Kagoda ziendeshwe na wateule wa viongozi wa chama kilichoshiriki kwenye ukwapuzi!!!!!!!!!!
 
Mpaka sasa Chiligati na genge lake hawajaweza kuwathibitishia wananchi kuwa yale magari ya MAHINDRA toka India yaliyosambazwa nchi nzima mwaka 2005 yalinunuliwa na chama chao na sio kwa kutumia peza za wizi toka BOT!! Onyesheni payment vouchers kama kweli chama chenu ni kisafi.

- Mkuu umechanganya ishus hapo, kuna makosa ya viongozi individually, na ya chama CCM.

- Mahesabu ya vyama vyote vya siasa hufanywa na Msajili wa vyama na yameshafanyika, wewe unaongelea hela zilizoongezwa huko individually, kusaidia CCM , that has nothing to do na CCM as chama cha siasa.

However, bado haya maneno ya Chiligati ni very low minded kutolewa na kiongozi wa level yake ya national level.

Mkuu sijakuelewa hata chembe.
Fedha inayoongezwa individually kusaidia chama haimo kwenye hesabu ya fedha ya chama. Je hii ina maana kwamba CCM ikiongezewa fedha individually, let say 40,000,000,000.00 kutoka kampuni ya Kakiti Agricultural Co, fedha hiyo has nothing to do with CCM??!!!??!!??

Una maana fedha zinazofanyiwa auditing ni zile zitolewazo toka serikalini tu?au namna gani!!?

If that has nothing to do with with CCM as a party, tutajua vipi chama kinapewa fedha na KGB ,Maharamia wa Somalia, au kinanunuliwa kwa bei chee na wanachama wake ambao ni wahusika wakuu wa wizi wa aina zote serikalini?
Je mtu binafsi akikipa Chama fedha, fedha hiyo haihesabiwi kama source moja ya income ya chama?

Ni katika kutaja kujua tu mkuu, maana kuuliza si ujinga ila kubwatuka ndiyo.
 
CCM hawana pakutokea na hili sakata la Kagoda. Wanajaribu kila njia kulikimbia lakini kila wanakokimbilia Kagoda ipo tu na 2010 ndiyo inanyemelea taratibu. Wana kazi kubwa sana ya kutafuta njia za kutuzuga Watanzania, lakini safari hii hatupo tayari kuzugika.

Haha haha haha!

Uliwahi ona wapi mtu kafanikiwa kukikana au kukikimbia kivuli chake mchana kweupe jua linawaka?

"Haki ya nani hiki si kivuli changu nasingiziwa tu"

Ukikaa kivulini ni kweli kivuli chako kinafichika, lakini ukweli ni kwamba kivuli chako kipo ila matawi ya mti yana kihifadhi kwa muda.

Uongo ulishindwa kuwasaidia CCM siku nyingi wakakimbilia kwenye ngawira.
Maburunguti ya Tani za noti za Dolali toka BOT nayo yanashindwa kabisa kuisadia CCM.
Kwa ununda wamerudi tena kutegemea uongo wakidhani wataokoka.
CCM sasa hivi kinayumba kama mlevi alo changanya pombe ya Mazi na Gongo, kinawafanya wasisambaratike ni MAburungtu ya tani za noti tu, siyo umoja na mshikamano.

Masikini ya Mungu, CCM hawasomi alama za nyakati.
 
- Mkuu umechanganya ishus hapo, kuna makosa ya viongozi individually, na ya chama CCM.

- Mahesabu ya vyama vyote vya siasa hufanywa na Msajili wa vyama na yameshafanyika, wewe unaongelea hela zilizoongezwa huko individually, kusaidia CCM , that has nothing to do na CCM as chama cha siasa.

However, bado haya maneno ya Chiligati ni very low minded kutolewa na kiongozi wa level yake ya national level.

Mkuu ni dhahiri unaelewa mambo yalivyokaa kushoto katika kipindi cha JK hasa kuanzia mambo ya list of shame yalipolipuka.Katika hali kama hii ni ngumu mtu kutofautisha kipi kilifanya na chama na kipi kilifanywa na mwanachama individually. Hapa nilitegemea toka kashfa ya EPA kuhusishwa na uchaguzi mkuu tayari mapema CCM ingeshakana kuhusika kwake. Kukaa kwake kimya ni dalili tosha kwamba walihusika.Pili, hata kama wizi ulifanywa individually je ulifanyika kwa faida ya nani? Na kama chama kilipokea kilipokea kikijua zinatoka wapi? Na huyo aliyeiba individually alitumwa na nani maana sijaona uzalendo wa namna hii wa mtu kuiba kwa faida ya chama.Ni lazima mtu huyu alitumwa na akahakikishiwa usalama wake na ndo maana kuna tetesi hawa wezi ni jeuri sana. Hapo inakuwa ngumu kusema kuwa CCM haihusiki.NI NGUMU MNO.
[/QUOTE]

Sidhani kama kuna ushahidi wa hayo unayoyasema hapo juu. CCM inastahili kulaumiwa kwa kukubali kunufaika na fedha za wizi lakini hiyo haliwaweki hatiani kwa kushiriki katika wizi. Huenda hayo yatakujaku kuthihirika huko mbeleni lakini mpaka sasa kosa lao kubwa ni kunufaika.
 
- Mkuu umechanganya ishus hapo, kuna makosa ya viongozi individually, na ya chama CCM.

- Mahesabu ya vyama vyote vya siasa hufanywa na Msajili wa vyama na yameshafanyika, wewe unaongelea hela zilizoongezwa huko individually, kusaidia CCM , that has nothing to do na CCM as chama cha siasa.

Si kweli.

Chama kinatakiwa kimpelekee Msajiri ripoti ya akaunti zake ambazo zimeshafanyiwa ukaguzi na chama chenyewe tayari. Na hapo ndio kuna tatizo.

THE POLITICAL PARTIES ACT, 1992-5, Sect. 14 (1)(b)( i )
Submission of Accounts and Declaration of Property

Every political party which has been fully registered shall submit to the Registrar an annual statement of the accounts of the party audited by an auditor registered as an authorised auditor and the auditor’s report on those accounts
 
ZITTO azidi kuwaka, asisitiza Kagoda mali ya CCM

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, bado anasisitiza kuwa Kampuni ya Kagoda ni mali ya chama tawala CCM.
* Adai fedha ilizochotwa EPA zilitumika uchaguzi mkuu 2005

Na Kizitto Noya

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiwezi kukataa uhusiano wake na Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited iliyochota zaidi ya Sh40 bilioni kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

Zitto aliyekuwa anajibu mapigo ya CCM iliyomshutumu juzi kwa kuipaka matope kwa kuihusisha na Kagoda, alisisitiza kuwa CCM haiwezi kujivua gamba la Kagoda kwa kuwa ndiyo inayomiliki kampuni hiyo, ikiwa miongoni mwa kampuni 22 zilizochota jumla ya Sh133 bilioni katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

"CCM ndiyo inayomiliki Kagoda na Kagoda ni ya CCM. Fedha za Kagoda ndizo zilizotumika kwenye kampeni za CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Huu ndio ukweli," alilisitiza Zitto.

Alisema kauli ya chama hicho iliyotolewa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati kuikana kampuni ya Kagoda, ililenga kujisafisha lakini pamoja na jitihada hizo, ukweli utaendelea kubaki kuwa kampuni ya Kagoda ni mali ya CCM.

Kwa mujibu wa Kabwe, endapo CCM inataka kutakata inatakiwa kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua hesabu zake za mwaka 2004/2005 na ieleze wapi ilipata fedha za uchaguzi mkuu mwaka 2005 uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani.

"Kama ni kujisafisha njia nzuri kwao si kutoa matamko, chama hicho kinatakiwa kumruhusu Mkaguzi Mkuu akikague na baadaye waseme fedha walizotumia katika uchaguzi mkuu mwaka 2005 zilizotoka wapi," alisema.

Alisema hakuna mantiki wala uhalali kuwaondoa mafisadi wa EPA katika uhusiano na CCM, kwani sehemu ya fedha iliyochotwa kwenye akaunti hiyo, zilitumiwa na CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2005.

"Mimi nasema hii ni spinning (kupindisha ukweli), kama mtu amechota Sh40 bilioni na sehemu ya fedha hizo zikatumika kwenye uchaguzi wa CCM utawezaje kukiondoa chama hicho kwenye ufisadi huo?" alihoji na kuendela:

"Kama CCM wataweza kuthibitisha kwa ushahidi kwamba hawahusiki na ufisadi huo na kwa ushahidi wa taarifa ya mkaguzi mkuu kuhusu chama hicho, niko tayari kuwajibika na maelezo yangu," alisema.

Katika hatua nyingine Zitto alisema Chadema inatarajia kutoa tamko kuhusu kauli ya Chiligati kwamba vijana wanatakiwa kuacha kuifuatafuata CCM kwa kuwa walizaliwa wakaikuta ikiwa imara na watakufa na kuiacha ikiwa imara.

Alisema kauli hiyo ni hatari kwa usalama wa vijana wa aina yake wanaotetea maslahi ya umma hivyo chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lazima kitoe msimamo wake katika hilo.

"Labda nimalizie kwa kusema kwamba Chiligati anaposema sisi vijana tunaoifuata fuata CCM tutakufa na kuiacha CCM imara ni very serious. Kama chama (Chadema), leo (jana) tutaitolea tamko kauli hiyo kwani tunahisi wanataka kutuua," alisema.

Kabwe alitoa kauli hiyo siku moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoa tamko rasmi kuiruka kampuni ya Kagoda Agricultral Limited ikisema kuwa haina uhusiano nayo.

Chiligati aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa chama hicho hakina uhusiano wa aina yoyote na kampuni hiyo na kwamba hata kama kuna mwanachama anayehusika, ni suala lake binafsi na sio kwa mwavuli wa chama.

Tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiihusisha CCM na Kampuni ya Kagoda inayodaiwa kuchota Sh40 bilioni kwenye akaunti hiyo na miongoni mwa watuhumiwa wa EPA waliokwishafikishwa mahakamani, yumo Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Shaaban Maranda

Juzi Chiligati ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM alitoa tamko la kukisafisha chama hicho na kashfa hiyo akisema haina uhusiano wowote na wala hawaitambui kampuni ya Kagoda.

"Vita dhidi ya ufisadi na rushwa nyingine ielekezwe kwa mtu mmoja mmoja na siyo CCM kwani haiwezekani wana-CCM wote wakaenda benki kuiba fedha hizo pamoja," alisema Chiligati na kuongeza: "kampuni ya Kagoda haina uhusiano wa aina yoyote na CCM na wala CCM hatuijui".

Alisema kwa muda mrefu viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakifanya juhudi za makusudi kutaka kuihusisha kampuni hiyo na CCM na kutoa mfano kwamba, hivi karibuni Kabwe alinukuliwa akisema kwamba kuisha kwa suala la EPA kwa kiwango kikubwa kunategemea Kagoda itakavyochukuliwa hatua za kisheria.

Chiligati alisema Zitto pia alinukuliwa akisema kushindwa kwa serikali kuchukua hatua dhidi ya Kagoda kuna maana moja tu na kwamba kampuni hiyo ndiyo inayoijengea CCM Kaburi.

Katibu mwenezi huyo alisema shutuma zinazotolewa na Zitto na wapinzani wengine ni siasa zenye takataka zinazolenga kuipaka matope CCM na kwamba ni za uzushi na uzandiki.

Alisema CCM ni chama chenye kuheshimika, makini na safi, hivyo vijana wadogo iliowalea kuanza kukipaka matope ni kutafuta laana na njama zao hazitafanikiwa.
 
Nadhani Zitto kaongea vizuri na ana hoja. Kusema kwamba vijana tumezaliwa na kulelewa na ccm ni utani na nadhani Chiligati haypo makini. Sisi ni Watanzania, tumezaliwa na kulelewa na tanzania sio chama ambacho tumekua tukishuhudia kikifanya ufisadi wa hali ya juu na kujidai kuwa kipo upande wetu.

Kunyamza kusema kwa kuogopa 'kulaaniwa' na ccm ni uoga unaowafaa wanaccm tu

Uzalendo kwa nchi hauwezi kufanywa na mtu anayejua kuimba wimbo wa taifa na ccm tu
 
- Kwa kweli inasikitisha sana kama tuna viongozi wanaoweza kusema this kwenye public, hivi hili taifa tumemkosea nini Mungu?

Hivi Chiligati ana mke na watoto ? Maana maneno mengine jamani tuwe tuna angalia nani anasema na hadhi yake katika jamii ? Huyu Mzee kweli ana mke na watoto ?
 
Mhe. Zito ana hoja ya msingi ila issue ya Kagoda ni sealed inside out mbele ya macho- ya kisheria na amini msiamini hakuna atakayefikishwa mahakamani kwa issue hii kwa sababu ni 'void ab initio' yaani batili toka mwanzo, kisheria Kagoda dont exist.
The King Maker -Rostam alimshauri Ben wazo likanunuliwa kampuni ikaundwa kwa fictitios names and adress.
Vimemo vikaztembea kwa Mama Meghji pesa zikatolewa.

Kwa vile wahusika walikuwa fictitios, The King Maker alishaandikishiana caveat na BOT kuwa incase of anything Kagoda interest will be protected.

Kampuni feki, majina feki na pesa zimetolewa ziko benki watazichukuaje.

Wale fictitios names wakaandika kwa msajili wamejiuzulu ugurugenzi. Barua zikaenda benk hizo pesa zihamishiwa akouts mbalimbali na hapo ndipo CCM ilipoingia. Ther are more benefisheries ambao kwa mujibu wa sheria za makapuni, benefisheries are non partisan as long as they are not the players.
Yaani ukiiba hizo pesa ukatoa msaada kujengea zahanati ya kijiji. Hata ukikamatwa zahanati haihusiki katika kosa lako.
Hivyo kisheria Kagoda haipo na hizo Bilioni 40 zimeyeyuka!.
 
Back
Top Bottom