Kagoda: Ni Rostam

Kagoda: Ni Rostam

Kauli kama hizi ameshazitoa mkuu wa nchi kama mara mbili. Mara ya kwanza ni pale aliposema wala rushwa anawajua ila anawapa muda wajirekebishe. Tena alipoenda bandarini alisema maofisa wanaosaidia wakwepa kodi pale bandarini anawajua na mbinu wanazotumia anazijua. Lakini ni wangapi aliwachukulia hatua baada ya kauli hiyo? Bandarini hadi kesho mambo ni yale yale, ukiagiza gari lazima iibiwe kifaa. Uzembe uko pale pale na ukwepaji wa kodi uko pale pale.

Kwenye hili DPP alikuwa anaongea kama bosi wake. Maana yake nini? Anawajua hao watu ila wako nje ya wigo wa sheria. Ni watu walio 'above the law'. Ndo maana analeta kizungumkuti cha kuwa walitumwa; kwa kujua tu kuwa walitumwa, waliowatuma anawajua vile vile. Huwezi kusema huyu katumwa halafu hujui aliyemtuma. Sema wote hao ni watu walio juu ya sheria na hao wanajulikana. Ni CCM na genge lao la mafisadi ambao wameshatajwa sana. Sasa kuikamata CCM au kulikamata genge hilo la mafisadi ni jambo lisilowezekana!

Waziri mkuu alishasema hawa ni watu wenye nguvu sana! Wanaweza kuiyumbisha nchi. Ni nani mwenye uwezo huo? Ni CCM na genge lao!
 
Ama kweli matukio mengi nchini huitwa - ONLY in Tanzania.
Hivi kweli umewahi kusikia askari akishindwa kumkamata mwizi kwa sababu mwizi huyo katumwa..
Wezi wengi Ulaya hata ktk Benk hutumwa, master planner hubakia kutazama mchezo unavyokwenda...Wauza unga toka Columbia hutumwa lakini wote hawa hukamatwa na wakafungwa pamoja na kwamba wametumwa. Leo Tanzania mtu alotumwa kuiba sii mwizi..Basi kama kweli ipo sheria hiyo tutaibiwa sana..Na hakika ya maneno haya itafungua ukurasa mpya wa sheria kiasi kwamba kesho mahakamani wezi watashinda kesi zao, kwa sababu WAMETUMWA.

Mkandara,
Kuna usemi usemao watu wakizoea rushwa, inakuwa kama sumu, inabadilisha kila kitu, tabia za watu, hadi yale maadili yanakuwa kinyume. Hata shule zetu zilizokuwa zinatufundisha maadili zimekuwa ni dharau; tumeingiliwa kabisa; hata sheria zetu zote zimekwisha. Kwa nyie mliopo huko nje, sawa kabisa mshukuruni Mungu wenu, maana watoto wenu watanusurika. Huku kwetu Sheria zimeskwisha, maadili yamekwisha, na nchi imekwisha!!
 
Kagoda case closed.
Ukisikia mtu mkubwa kama Feleshi bila aibu anasema tumpelekee habari Kagoda ni nani wakati Mwanakijiji alimpa kila detail, sasa sijui anataka zipi zaidi.
Kamata RA atawataja wote aliokula nao. La sivyo amwache aendelee kutamba na afute kesi zile zingine zote ili sisi ikifika wakati tuamue nini la kuwafanya. Full stop. Wasituchezee akili.
you are absolutely right mkuu.mi naona tunachezeana akili tu na huu upuuzi wa EPA.Vitu viko very clear wanaleta mazingaombwe.Najuuta kuongozwa na JK kama rais wangu .Naona aibu kwa kweli
 
This is a big joke!!!!! there are 100 reasons why Feleshi should be fired! ha-qualify kuwa katika nafasi hiyo! stupid mandingo!!
 
Inasikitisha kuona jamaa anaonagea utumbo kama mtu asieambulia hata darasa moja wakati amesoma tena kwa hela ya kodi za walalahoi, ni mzima kweli huyu feleshi jamaniiii ? mie naona laaana za watanganyika zimeanza kumuingia taratiiiiibu ...
 
Huyu DPP Feleshi amedhihirisha kuwa ni mwoga.

___________________
Justice delayed is justice denied
 
Huyu DPP anaongea pumba sana...yeye aseme kapewa order ya kuwaacha na bwana mkubwa shauri hela aliyochukua swahiba wake RA zilitumika kwenye kampeni za ccm na asitake kutugeuza watanzania wajinga
 
Hiki ni kituko! Huyu DPP kweli yuko sawasawa? Hao watu waliohusika na KAGODA ni wahalifu kama wahalifu wengine, na walipaswa kukamatwa siku nyingi. Nchi yetu inaendeshwa kwa utawala wa sheria, hivyo kila anayevunja sheria za nchi ni lazima akamatwe na kushitakiwa. Siamini kama waandishi wa habari walim-quote kwa usahihi huyu anayejiita DPP. Lakini kwa kuwa hajawahi kusikika akikanusha basi tunalazimika kuamini kweli alitoa kauli hii ya 'ovyo ovyo'. Akishindwa kuwafungulia mashitaka majambazi hawa wa Kagoda wakiongozwa na RA itambidi kujiuzulu na kumpisha mtu mwenye uchungu na nchi hii.
 
hakuna haja ya kujadili kagoda kama ufisadii kwani kwa ujumla wake CCM na serikali yake ndo waliotufikisha kwenye wizi wa aina hizii (ufisadi wa fedha na madaraka).

tunahitaji kuhamasisha maendeleo ya jumla kama maji safi na salama, elimu, afya, umeme, barabara, utawala bora, kilimo na viwanda na kukemea vipingamizi vyake kama vile uongozi mbovu(wizi, ulafi, uwezo mdogo) na sera na sheria kandamizi (katiba ya wote ipatikane) katika kufikia maendeleo hayooo...

hatuna haja ya kutoa nafasi kubwa ya media kuzungumzia feleshi na kagoda!!! haijengi wa kuhamasisha maendeleo ya msingi kwa mlalahoi..

inawezekana kuleta mabadiliko kwa kuwa na uongozi mbadala kuanzia kijiji hadi taifa..
maendeleo yanawezekana kwani iweje barabara za kuunganisha mikoa zijengwe ndani ya muda mfupi tena baadhi kwa kodi yetu..gafla leo hata umaliziaji wa km 5 (sam mujoma) ni taaabuuuu????

lagosi ilihamia abuja from nothing na leo miundo mbinu ya abuja ni ya kuigwaaa...waliwezajee???

CHANGE WE CAN BELIEVE IN..
wewe kama hujatumwa basi umehusika kwa kiasi kikubwa sana, mawazo yako ni sasa na kutia supu nazi....huwezi kukaa kimya kwenye hili la ufisadi kwa mambo makuu ninayoyaona mimi:tusiposema, tukawataja, tukawachukulia hatua na kuwataka warudishe pesa zetu;
1. tutaendelea kuongozwa na mafisadi na hatutaendelea
2. miradi mingi ya maendelea haitakamilika...pesa za EPA kama zitatumika vizuri zitainua kilimo, je kagoda nao wakirudisha???? tukapeleka kwenye miundombinu unayosema??? au unataka tuendelee kulitia taifa madeni kwa kukopa pesa ambazo zinaliwa na wajanja wachache....hebu tutumie tu hata busara kidogo...
3. Tuna viongozi wasafi ambao wamefunikwa na kashfa za ufisadi, lazima mafisadi watajwe na kufikishwa mbele ya sheria ili tujue pumba nizipi....

LAZIMA VITA YA UFISADI IENDELEE HATA IKIBIDI KUMWAGA DAMU...
 
Nduguzanguni, Felesh hatathubutu kabisa kumtaja au kumshtaki kinara ambaye alihakikisha kuwa anapewa cheo cha DPP kwa lengo mahususi la kulinda maslahi yake. Hebu eti DPP anaotokea au kuzaliwa kanda ipi ya TZ!!!????? Kulaleki!!!!! Ukweli ni kwamba hata hawa EPAz wengine walitumwa na hata kama wengine walitumia makampuni yao halisi kama Njake, but walitumwa kuchukua fedha hizo!!!!! Mtu kama Njake aliitwa kabisa Dar es Salaam kukutana na vinara, baadaye akawa anafuatwa Arusha na vijana na wakawa wanalipiwa gharama zote wakiwa Arusha!!! Ni kwa vile pia wameahidiwa wakae kumya wasiseme mengi ila wakiamua kutapika the government will be in shamble!!! Ila ingekuwa mimi ningetaja, acha liwalo na liwe, mwishowe mahakimu watafuata sheria na watafungwa halafu waliowatuma wanashangilia. Huu ni upuuzi mtupu, sanaa za hovyo hovyo!!!
 
Unapokuwa na DPP ambaye utendaji wake unawajibishwa na Mteule wake unategemea nini?
Madaraka ya rais ni makubwa na hawezi kuyatumia ipazavyo, hiyo ndo tabu. Mtu akihujumu uchumi, mara moja inatakiwa assets zote wafreeze, apelekwe mahakamani. Sio mtu yuko mahakamani kwa tuhuma kama hizo then kampuni zake zilizotumika ktk wizi zinaendelea kufanya kazi, huu ni uwendawazimu!!
 
Hiyo ni mbinu ya kuchelewasha na kusahaulisha watanzania mambo. Huyo atakayesema ametumwa, amwoneshe aliyemtuma ala?!! Wakamatwe wote waliotumwa, watawataja tu mabosi wao. Je upelelezi utakapoisha bila kuwaona hao waliotuma, ndo itakuwaje????
 
Hii ni sirikali, ni panya gani anaweza kumfunga paka kengele?
 
Yaani Feleshi anaweza akasema maneno hovyo hovyo hivi! Siamini.
Nadhani muda umefika ajiondokee tu. Sidhani kama ana nia na nguvu ya kushughulilia masuala ya rushwa kama haya.
 
DPP anaanza kuweweseka kwa majibu ya hovyo, iko siku na siku hiyo yaja, mwenyewe atasema ukweli, ni nani mwizi wa pesa za Watanzania na pesa hiyo ilitokaje na ikafanya kitu gani.
 
Kama DPP bwan Feleshi anasema akimkamata mtu aliyechukua fedha za KAGODA haimsaidii kumpata mtu aliyemtuma mtu aliyechukua fedha basi hakuna haja ya yeye kuwepo kwenye cheo hicho kwa maana HAFAI

Nasolwa na wengineo kwani hadi leo hamjagundua kuwa vilaza wa Tanzania wanakuja katika shepu, maumbile na vyeo tofauti tofauti?
Na kama nivyosema pahala fulani Tanzania mpaka tujikomboe toka kwa hao vilaza tutaendelea kuwa tunaburuzwa buruzwa kila kona!
 
Wanasheria mnisaidie; fedha za EPA kupitia kagoda zimeibiwa Benki Kuu (BOT). Kisai cha Tsh. 40bil zimeibiwa kwa staili ya kuforgi nyaraka. DPP anasema walikuwa wanazichukua hizo fedha wanajulikana ila hawezi kuwashtaki eti walitumwa tu. Sasa anatafuta waliowatuma.
(a) amejuaje kwamba hao jamaa walitumwa?
(b) kama walitumwa si watakuwa wamewataja mabossi wao?
(c) fedha nyingi kiasi hicho si unaweza ku-trace kwa kuangalia bank transactions na kuzifuatilia akaunti husika?
(d) kama aliyewatuma ni Rais, au CCM, DPP atachukua hatua gani? atawaachia hao jamaa anaodai walitumwa
?

Nziku umeuliza maswali ya msingi sana.
Kwa uelewa wangu ni kuwa katika sheria ukimkamata mtu na kitu huyo mtu anakuwa shahidi wa kwanza katika shauri husika.

Mfano, Hao ambao DPP anadai walitumwa wanapaswa kisheria kuisaisia polisi katika upelelezi wao.Pamoja na hilo hao nao wanaingia katika kesi moja kwa moja kwa maana kuwa wanakuwa first suspects.

Siyo kazi ya Feleshi kutuambia kuwa hawa walitumwa, maelezo hayo yanatakiwa yawe sehemu ya utetezi wao mahakamani.Hapo ndipo watakapotakiwa kuwataja waliowatuma.

Anyway, suala la Kagoda kwa nijuavyo mimi limefungwa siku nyingi.Uchaguzi unakuja na chama dola kushaanza kubadili mwelekeo wa kisiasa kwa kutuelekeza kwenye masuala mengine kusudi tusiwe na muda wa kuhoji masuala muhimu.Feleshi anakuwa remote controlled tu na wenye mpini.

Yahiitaji moyo lakini.
 
Sijawahi soma upumbavu kama huu , why not go where the investigation leads you? eti walitumwa kwanini usiwafuate hao waliowatuma.. . Eeeh mungu naomba saidia Tanzania yetu
 
Back
Top Bottom