KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 698
Kauli kama hizi ameshazitoa mkuu wa nchi kama mara mbili. Mara ya kwanza ni pale aliposema wala rushwa anawajua ila anawapa muda wajirekebishe. Tena alipoenda bandarini alisema maofisa wanaosaidia wakwepa kodi pale bandarini anawajua na mbinu wanazotumia anazijua. Lakini ni wangapi aliwachukulia hatua baada ya kauli hiyo? Bandarini hadi kesho mambo ni yale yale, ukiagiza gari lazima iibiwe kifaa. Uzembe uko pale pale na ukwepaji wa kodi uko pale pale.
Kwenye hili DPP alikuwa anaongea kama bosi wake. Maana yake nini? Anawajua hao watu ila wako nje ya wigo wa sheria. Ni watu walio 'above the law'. Ndo maana analeta kizungumkuti cha kuwa walitumwa; kwa kujua tu kuwa walitumwa, waliowatuma anawajua vile vile. Huwezi kusema huyu katumwa halafu hujui aliyemtuma. Sema wote hao ni watu walio juu ya sheria na hao wanajulikana. Ni CCM na genge lao la mafisadi ambao wameshatajwa sana. Sasa kuikamata CCM au kulikamata genge hilo la mafisadi ni jambo lisilowezekana!
Waziri mkuu alishasema hawa ni watu wenye nguvu sana! Wanaweza kuiyumbisha nchi. Ni nani mwenye uwezo huo? Ni CCM na genge lao!