Kagua salio lako CRDB, kuna pesa hazionekani kwenye akaunti

Kagua salio lako CRDB, kuna pesa hazionekani kwenye akaunti

Boycott the bank!
1000024166.jpg
 
Hawa jamaa mimi siwaelewi. Nashukuru Mungu nilihamisha milioni 2.4 kabla ya siku ya kuboresha huo mfumo, kukabaki na elfu 23 tu.
Juzi nikawa najichanganya nlikua na 1.2m MPESA nikawa naituma huko ikagoma nami nikakausha.

Sasa hivi salio linasoma elfu 25+ hiyo 2,000 iliyoongezeka sijui imetoka wapi.
 
  • Kicheko
Reactions: vnn
Hawa jamaa bado wanazingua vipesa vyetu wanarudisha lini?
 
Mzee wangu kanipigia analalamika kiasi cha pesa kimechotwa kwenye akaunti yake bila taarifa. Imagine wamechota zaidi ya Laki mbili na sehemu si kutiana umaskini huku???
 
Acha kutunza pesa Bank,
Acha kutunza pesa Bank
Acha kutunza pesa Bank
Ukielewa hili utaepuka hizi ngonjera za kitapeli za hawa wamiliki wa mabenk na saccos mnazotunza pesa zenu, tumia bank kupokea pesa ya salary tu then hamisha ktk CRYPTO WALLETS, tunza huko hakuna hata senti itakayopotea wala kuibiwa au kukatwa makato ya KIPUMBAVU, ukiwa mjuzi zaidi pesa yako itaongezeka kwa kununua digital assets zenye thamani kubwa.

NARUDIA TENA 👉 Acha kutunza pesa Bank huu ni muda wa watanzania kuamka kukataa huu utapeli wa hawa Middle Men wa kifedha, elimikeni hamtaibiwa tena.
 
Nadhan mnaelewa tulivo kuwa tunalalamikia siku za hapo nyuma kuhusu hii bank ta CRDB binafsi nishaleta uzi humu kuhusu uwizi wa hii bank na wadau wengine pia walishaleta uzi kama wangu,,nadhani toka niliweka ule ujumbe humu sidhani kama hata mwezi umepita CRDB wanaenda kuanguka kweli tena hii inakuja kuwa kama bank za kawaida tu.
 
Zaidi ya milioni siioni kwenye akaunti yangu ya CRDB.

Mdau kagua na wewe salio lako usije ukawa upo hujui kinachoendelea.

Kesho pakikucha tu natia mguu hapo Holland branch…
Si bora wewe tu milion twako hautuoni, wenzako tu bilion twetu natwo hatuonekani. Sasa sijui tutalipwa au vip
 
Bado Mtandao Haujakaa Sawa, Jana Nimetumiwa Pesa Toka Mpesa , hadi sasa Haijafika.
 
Back
Top Bottom